WOKOVU
NI SIRI ILIYOFUNULIWA
"Ninyi (Wafuasi wa Yesu) mmepewa kuzijua siri za ufalme wa Mungu" Luka 8:18
Siri hii ili iwe wazi kwa mtu ni lazima ifunuliwe kwa mtu kupitia “NURU YA INJLI” ili aweze
kuupokea. Ukisoma 2Kor. 3-4 inasema, “Lakini ikiwa Injli yetu imesitirika,
imesitirika kwa hao wanopotea; ambao Mungu wa dunia hii [shetani] AMEPOFUSHA
FIKRA zao wasioamini, isiwazukie nuru a Injili ya utukufu wa Kristo aliye sura
yake Mungu. Kumbe shetani anajua atu wakiielewa INJILI watazukiwa na nuru
itakaowavuta kwenye wokovu, hivyo anafana kazi ya kuhakikisha kwamba anapofusha
fikra za watu hata wakihubiriwa Injili wawe wagumu kuelewa.
Katika 1Kor. 1:18 Paulo anongea
jambo linaofanana na hilo, anasema, “Kwa sababu neno la msalaba (INJILI) kwao
wanaopotea ni UPUUZI, bali kwetu tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.” Kwa
nini anaona ni upuuzi? Ni kwa sababu fikra zimepofushwa, na hawezi kuiona nguvu
ya Munguka tika Injili (NURU YA INJILI). Kiujmla
shetani anatumia mbinu mbalimbai
kupambana na “kweli ya Mungu”(INJILI). Moja kati ya mbinu anazozitumia sana ni
hii ya kupofusha fikra za watu. Japo kwa sehemu amefanikiwa kuwakamata wengi
(Paulo anawaita WANAOPOTEA), bado wako wengi wanaoendelea kusikia Injili na kuokoka
(tunaoamini, tunaoiona nguvu a kuaangaza maisha yetu katika INJILI).
Ndiyo
maana nikaanza kwa kukuuliza kama umeokoka. Sasa nikuulize tena,“Je upo miongoni mwa hawa wanaopotea ambao
shetani amepofusha fika zao? Shetani anafanya juhudi kubwa katika kuteka na
kupofusha fahamu (fikra) za watu wa Mungu ili aendelee kuwatumikisha. Tumesoma
kwamba “anapofusha fika” - KUPOFUSHA FIKRA ni kufunika uwezo wa mtu kuona kwa
kutumia fikra zake (anaondoa uwezo wa kupata ufunuo wa mambo ya kiroho). Kama
wewe ni mshuhudiaji wa habari za Yesu kwa watu (mwinjilisti au mchungaji)
utakubaliana na mimi kwamba kuna watu wengi sana ambao fikra zao zimepofushwa.
Kwa nini? Kwa sababu ya maswali na misimamo utakayoikuta kwa watu wa Mungu
(watu ni wabishi hata kwa mambo yaliyo wazi kabisa).
Paulo
alipokuwa anawaombea watu aliowahubiria INJILI akisema, “Macho ya mioyo yenu yatiwe nuru mpate KUJUA tumaini la wito wake…”
(Waefeso 1:18) Maneno ya msingi hapa ni “MACHO YA MIOYO YATIWE NURU.” Haya
macho ya mioyo ndiyo ambao hutusaidia kuelewa yale tunaojifunza hasa kwenye
neno la Mungu. Kwa hiyo shetani akishafanikiwa kumpofusha mtu, inakuwa vigumu
sana kwa mtu huyo kusikia INJILI (Neno la Mungu). Ni maombi yangu kwamba Mungu
aendelee kufungua macho ya watu wake kila siku ili kupitia INJILI
tunaowahubiria waokoke.
Kusudi la kitabu hiki ni kukupa nafasi ya kuuelewa
japo kwa ufupi “WOKOVU” Kama unavyoonekana kwenye Biblia. Ni maombi yangu kuwa,
Mungu akuwezeshe kwa msaada wa Roho mtakatifu wake, ili upate kuelewa sawasawa
maana ya jambo hili muhimu sana kwa maisha ya kila mwanadamu aliyeko hapa
duniani. Nikukumbushe kwamba huu ndio wakati wako uliokubalika mbele za Mungu,
ili uweze kuyasikia haya. Nami nikusihi, “Kama
ukiisikia sauti ya Mungu leo usiufanye moyo wako kuwa mgumu.”
Mtumishi wa Mungu Tito akahitimisha kusema: Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa; tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu; ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema.(Tito 2:11-14)

No comments:
Post a Comment