TANZANIA NA INJILI

 INJILI ILIVYOKIATUFIKIA
Naomba nianze kwa kueleza kwa kifupi, nini maana ya Injili
Injili (gospel) - Ni habari njema za Yesu Kristo, habari hizi zimebeba kuzaliwa, kufa, kufufuka na kurudi kwa Yesu mara ya pili kulichukua kanisa. Habari hizi zimeandikwa kwenye vitabu vinne vya kwanza vya agano jipya na kwa ujumla wake huitwa "VITABU VYA INJILI". Japo unaweza kuzipata pia japo kwa kifupi kwenye nyaraka mbali mbali za mitume na kitabu cha MATENDO YA MITUME
Mtume Paulo kwenye waraka kwa Warumi 1:16 anasema "Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia."
Habari hizi za Yesu (Injili) zikiaminiwa huleta matokeo makubwa kwenye maisha ya mtu, matokeo haya huitwa wokovu. Injili ni uweza au nguvu ya Mungu ya kumwokoa mwanadamu kupitia mauti na kufufuka kwa Yesu.
1 Wakorintho 1:18 Kwa sababu neno la msalaba (Injili) kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni NGUVU ya Mungu.
Mtu anayepeleka Injili huitwa Mwinjilisti (Evangelist), huyu ni mtu maalumu aliyepewa huduma (kibali maalumu cha kusimama kwenye eneo hili) japo swala la kuwahubiria watu ni jukumu la wakristo wote; sio wote waliopewa huduma hii ya Uinjilisti.


Nirudi sasa katika kukuwekea mambo bayana:
Napenda ukumbuke kwamba, "Katika dunia hii kila jambo huwa na mwanzo wake!" Kuna kipindi duniani hapakuwa na jina Tanzania ila baadaye lilianza; kuna wakati vitu tunavyoviona havikuwepo ila sasa vimekuwepo.
Nimeyasema haya ili kukuleta kwenye jambo hili muhimu lenye historia ya aina yake tangu na kabla ya kuanzishwa kwa taifa liitwalo Tanzania.

No comments:

Post a Comment

MWANAUME KWENYE NAFASI YA "MUME"

Mume ni mwanaume aliyeoa kwa kuzingatia vigezo na taratibu za kijamii, kishria na za kiroho. Mume si rafiki wa kiume (boyfriend), hawara, wa...

Powered By Blogger