Haleluya!
Uimara
ni wa muhimu sana kwa kitu chochote. Kama kitu kitakuwa na sifa
nyingine zote kama vile sura nzuri, muundo mzuri, au hali ya kuvutia
kabisa ni lazima kuulizia kuhusu uimara wake. Kitu imara ni kitu cha kuaminika.
Uimara
ni uwezo wa kudumu kwa muda mrefu, uwezo wa kukabiliana na mazingira,
uwezo wa kustahimili mazingira magumu, uwezo wa kuzalisha
kilichokusudiwa kwa kiwango, kiasi na hali iliyokusudiwa bila kupoteza ubora. Ubora huonakana zaidi wakati wa misukosuko. Kama kitu au mtu hatosimama imara wakati wa kujaribiwa au wa kupitia changamoto basi uimara umekosekana.
Swali: Je, ni muhimu kwa mtu aliyeokoka kuimarika kiroho
Paulo akasema, "Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana sikuzote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana."1 Wakorintho 15:58 Mstari huu ni wa msingi sana kwa maisha ya kila mkristo. Paulo anasema tuimarike, tusitikisike, na tuzidi sana kuitenda kazi ya Mungu. Mpendwa misukosuko ya Imani ni Mingi sana katika ulimwengu huu.
Shetani yupo kila siku kutupiga vita (Waefeso 6:10-12, 1Petro 5:8), tena tunavutwa sana na tamaa zetu wenyewe (Yakobo 1:14). Mungu naye kuna wakati hutujia na kipimo, kuangalia kama tunaweza kuonyesha uthabiti kwa hatua nyingine. (Alifanya hivyo kwa Danieli na wenzake, pia Ayubu). Tusipoimarika hakika hatutaweza kusimama wakati wa kujaribiwa kwetu. Tunapaswa kuwa na Imani thabiti, isiyotikisika wala kubadilika. Yaani tumng'ang'anie Yesu hata kufa.
Kiujumla, Kuimarika huambatana na:
1. Uwezo wa mwamini kustahimili majaribu.
Tena Yakobo katika Yakobo 1:12 anasema, "Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao."Kumbe kuna taji tutakayoipata kwa kustahimili majaribu. Ustahimilivu ni tunda la kuimarika katika imani. Wengi ambao hawajaimarika wamekuwa wepesi wa kukata tamaa na kurudi nyuma. Ni muhimu kuamua kujiimarisha katika Imani ili uweze kustahimili hatamaye ukaipokee taji ya uzima.
Kama Yakobo alivyotangulia kusema, "Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu,
mkiangukia katika majaribu mbalimbali mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa
imani yenu huleta saburi. Saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa
wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno.Yakobo 1:2-4
Sio jambo rahisi kuhesabu ni furaha tupu uwapo kwenye majaribu, unahitajika uimara katika hali ya rohoni ili
kubadilishugumu wa mwilini kuwa wepesi. Wapendwa wengi kwa sababu ya mapito wameamua kujiunga na Imani potofu na kusikiliza mafundisho manyonge yanayosisitiza juu ya mafanikio katika ulimwengu huu bila kujali umilele. Tukiimarika katika Imani hakika tutaweza kufurahi katika mateso na dhiki kwa ajili ya ufalme wa Mungu.
2. Ushujaa na ujasiri katika kuitenda kazi ya Mungu na kulitimiza kusudi Mungu alilokuitia.
Tunda lingine la kuimarika ni ujasiri na ushujaa katika kazi. Mungu anamwambia Joshua, "Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana ni wewe utakayewarithisha watu hawa nchi hii niliyowaapia baba zao ya kwamba nitawapa." (Yoshua1:6) Kazi ya utumishi katika mwili wa Kristo inahitaji ujasiri mwingi. Vita kwa watumishi ni vikali sana, tena kuna wakati wa kupita katika kupepetwa hata kukataliwa. Tumetumwa kamaa kondoo katikati ya mbwa mwitu (Mathayo 10:16)
Mungu ametuita katika mazingira yenye uadui mkubwa kwa kile tulichotumwa kufanya. Tumepewa kuihubiri Injili ya Yesu Kristo ili watu waokolewe na waondoke kwenye mikono ya Ibilisi. Hii si kazi rahisi, tunahitaji roho ya ujasiri na ushujaa mkubwa. Paulo anasema tuwe hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake (Waefeso 6:10).
Hatupaswi kuogopa, malango ya kuzimu hayawezi kulishinda kanisa la Mungu. Watumishi wa kweli hawawezi kuogopa wingi wa manabii wa uongo. Tuna ujasiri kama simba, hatuwezi kuogopa dini au dhehebu linalochafua Imani, hatuwezi kuogopa serikali (japo tunaiheshimu) inapoingia kwenye anga za ufalme wa Mungu. Hapa ni ujasiri baada ya kuimarika katika Imani.

3. Furaha na amani katika kuyatimiza mapenzi ya Mungu, si mtu wa kujilaumu.
Tunda lingine la kuimarika ni furaha katika shria ya Mungu. Tumeitwa kufurahi katika Bwana (Wafilipi 4:4) Tena tunapomtumikia Mungu na kuyafanya mapenzi yake tunajisikia furaha na amani hata kama tunayatimiza kwa machozi. Paulo alistahimili vifungo na mapigo mengi akiwa na furaha tele ndani yake Kristo. Hakumlaumu Mungu wakati wa mateso yake; mfano alipokuwa gerezani yeye pamoja na Sila, aliendelea kumsifu Mungu kwa furaha na kuomba. Alifanya yote kwa furaha na amani.
Yesu alikubali kushinda njaa kwa ajili ya kuyasimamia mapenzi ya Mungu. Aliyachukulia mapenzi ya Mungu kama chakula chake. Yesu akawaambia, Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka, nikaimalize kazi yake. Yesu anakazia swala la kumaliza kazi. (Yohana 4:34)

Upendo wetu kwa Mungu haupaswi kuwa wa maneno matupu, bali ni maisha halisi ya kuishi kulingana na maagizo au amri za Mungu. "Kwa maana huku ndiko
kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito."1 Yohana 5:3 Watu ambao hawajaimarika huziona nzito sana sheria za Mungu. Tukiimarika katika Imani hatutaona ugumu kumfuata Mungu. Tutakuwa tayari hata kuyatoa maisha yetu kwa ajili ya kazi ya Mungu. Hatutajilaumu tutakapojikuta tumeachwa peke, au kusalitiwa. PAulo alikutana na wasaliti wengi lakini aliendelea mbele.
4. Tumaini imara kwa Mungu.
Hakuna tumaini kwa watu wenye imani dhaifu au wasio na imani. Kumtumaini au kumngoja au kumtegemea Mungu kunahitaji Imani. Kumbuka Mungu hatumwoni kwa macho ya damu na nyama. Na kila tunachokijua kuhusu Mungu ni kwa njia ya Imani. Tunaokolewa kwa Imani na tunapaswa kuishi kwa Imani (Waebrania 10:38) Haya ni maneno ya mtu mwenye tumaini "Tazama,
Mungu ndiye wokovu wangu; Nitatumaini wala sitaogopa; Maana Bwana
YEHOVA ni nguvu zangu na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu".(Isaya 12:2)
Nabii Isaya anasema "Mtumainini Bwana siku zote Maana Bwana YEHOVA ni mwamba wa milele." (Isaya 26:4) Tumaini hili haliji bila Imani thabiti kwa Mungu. Katika Mithali 14:26 tunasoma, "Kumcha Bwana ni tumaini Imara" Nabii Yeremia naye akasema, "Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni tumaini lake. (Yeremia 17:7)
Tumaini Imara ni udhihirisho wa Imani thabiti. Na
tumaini letu kwa ajili yenu ni imara, tukijua ya kuwa kama vile mlivyo
washiriki wa yale mateso, vivyo hivyo mmekuwa washiriki wa zile faraja. (2 Wakorintho 1:7) Kuaminiana katika utumishi hujenga tumaini imara kati yetu. Na kwa sababu sote tunamtumaini Mungu inakuwa vyepesi kwa Mungu kumtumia kila mmoja wetu kwa ajili ya mwenzake.
Paulo anamwita Mungu wetu, Mungu wa tumaini. Yaani Mungu anayeweza kutumainiwa (ni Mungu wa tumaini letu). Warumi 15:13 "Basi
Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika kuamini,
mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mtakatifu." Hapa neno linatuongezea kitu cha ziada juu tumaini tulilonalo katika Mungu. Mungu hutujaza furaha na amani katika kuamini kwetu. Tena katika nguvu za Roho Mtakatifu tunazidi kuimarika katika tumaini letu kwa Mungu. Tumaini hili linahitaji uimara katika Imani.
5.
Kumzalia Mungu matunda.
Mti hauwezi kuzaa matunda kabla haujakomaa. Ni lazima kwanza uote mizizi na matawi yake yaimarike vya kutosha ndipo utakapotoa maua na hatimaye kuzaa matunda. Vivyo hivyo na sisi katika maisha yeti ya rohoni pamoja na utumishi, hatuwezi kuzaa matunda tukiwa bado wachanga na tusio na mizizi. Tuanatakiwa tuimarike ili tuweze kuzaa matunda kwa ile mbegu ya Neno la Mungu iliyopandwa ndani yetu.
Ona Yesu anavyosema,
"Na zile penye udongo mzuri, ndio wale ambao kwa unyofu na wema wa mioyo yao hulisikia Neno, kisha hulishika; kisha huzaa matunda kwa kuvumilia." (Luka 8:15) Uvumilivu ni tunda la uimara. Mtu ambaye emelegea katika Imani hawezi kuwa na uvumilivu. Kuna misukosuko mingi inayotupata sisi tuliolipokea Neno la Mungu.
Yesu anataja baadhi katika mfano huu wa mpanzi; yaani Ibilisi (Kando ya njia), Ugumu wa moyo (mwamba), shughuli na udanganyifu wa mali. Mambo haya si mepesi, yanahita uthabiti na uimara ili mtu aweze kuyakabili.
Paulo anashauri juu ya mwenendo ambao pia husababishwa na uimara wetu katika Imani. Anasema, "mwenende kama ulivyo wajibu wenu kwa Bwana, mkimpendeza kabisa; mkizaa matunda kwa kila kazi njema, na kuzidi katika maarifa ya Mungu; (Wakolosai 1:10) Tunawajibika kwa mengi katika ufalme wa Mungu. Tunapaswa kuabudu, kutumika, kuujenga mwili wa Kristo kwa karama na vipawa pamoja na kuwapeleka walioitwa kwa sadaka zetu. Haya yanihitaji uimara katika maisha yetu ndani ya Kristo. Vinginevyo tutaishia kuogopa na kulalamika.

Paulo anamwambia Tito, "Watu wetu nao wajifunze kudumu katika matendo mema, kwa matumizi yaliyo lazima, ili wasiwe hawana matunda." Tito 3:14 Hili linatufundisha kujizuia, tabia hii ni kiutu uzima. Watoto katika imani hawawezi kufanya hivyo. Watu walioimarika kwenye Imani wana uwezo wa kusimamia matumizi ya kila walichopewa na Mungu ili kuweza kuzaa matunda.
Katika 1Wakorintho 13:11, Paulo anasema ameyabatilisha "mambo ya kitoto" yaani hafikiri au kufanya tena kama mtoto; ameshakuwa mtu mzima (ameimarika). Mambo kama kuzunguka kwenye vibanda vya maombezi, kukimbia michango kanisani, kuwadharau viongozi, kujivuna kwa sababu ya huduma, kutumia ulaghai kupata fedha na mengine ni mambo ya kitoto. Watu wazima (walioimarika) wanatafuta kazi: yaani wafunge, wajitoe na kujitolea, wakeshe, wahubiri Injili mitaani, waandike vitabu, wapanue huduma (si kugombana na wachungaji) na mengine kama hayo.

No comments:
Post a Comment