Kumcha Mungu kunamaanisha kuwa na hofu ya Mungu (fear of The lord), kumuheshimu Mungu kwa kiwango cha juu, kumpa Mungu nafasi anayostahili. Kumcha Mungu kunajumuisha kumuheshimu(kumwabudu), kumtii, kumtukuza na kumtumikia kama Mungu.
2 Mambo ya Nyakati 19:7 Basi sasa hofu ya Bwana na iwe juu yenu; angalieni mkaifanye; kwa maana kwa Bwana, Mungu wetu, hapana uovu, wala kujali nafsi za watu, wala kupokea zawadi.
Mathayo 10:28 Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika jehanum.(Mungu)
Mithali 22:4 Thawabu ya unyenyekevu ambao ni kumcha Bwana Ni utajiri, na heshima, nayo ni uzima.
KUMCHA MUNGU KUNA FAIDA NYINGI

- Kunatupa mahusiano mazuri na Mungu. Isaya 57:15 "Maana yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye milele; ambaye jina lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo patakatifu; tena pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea, ili kuzifufua roho za wanyenyekevu, na kuifufua mioyo yao waliotubu." Mstari huu unatuweka wazi kwamba, watu wanaoweza kupata nafasi ya kukaa na Mungu ni wale wenye toba na unyenyekevu.
No comments:
Post a Comment