Mwanafunzi ni nani?
Ni mtu ambaye hajui na yuko tayari kujifunza na kufuata yale anayojifunza (kuwa mfuasi). Ni mtu ambaye yuko tayari kuwa chini ya mwalimu ili apokee ujuzi na maarifa mapya. Mfano wanafunzi wa Yesu walikaa chini ya Yesu ili kujifunza mambo yahusuyo ufalme wa Mungu.
Matendo ya Mitume 1:3 "wale aliowadhihirishia nafsi yake, kwa dalili nyingi, baada ya kuteswa kwake, ya kwamba yu hai, akiwatokea muda wa siku arobaini, na kuyanena mambo yaliyouhusu ufalme wa Mungu"
Sifa za mwanafunzi mzuri
- Anajua kwamba hajui
- Yuko tayari kujifunza
- Anamwamini mwalimu wake
- Anajua wajibu wake katika kujifuza
- Anaheshimu maagizo ya mwalimu/waalimu wake
- Ana bidii katika kujifunza
- Anatafuta kujua nyakati zote
- Ni mtunzaji mzuri wa muda
- Ni msafi kimwili na kiroho (si mdhambi)
- Anaiheshimu nafasi ya Mungu
- Anawapenda waalimu pamoja na wanafunzi wenzake.
- Ni mbunifu na mwenye kujiamini
- Ana nidhamu nzuri
- Ana heshima kwa wazazi, waalimu na wenzake
- Hana majivuno hata akifanya vizuri kwenye mitihani
- Ana maono (vision - picture of his/her destiny)
- Anafuata utaratibu uliowekwa au aliojiwekea (punctuality)
- Anatamani wengine wafanikiwe (hana wivu na choyo)
- Anatumia vizuri vipawa (talents) vilivyopo ndani yake
- Anajali afya yake
- Hana ushirikiano na marafiki wabaya (peer groups) 1Kor 15:33
- Anatambua umuhimu wake katika kizazi cha sasa na cha baadaye
- Ni lazima awe mtu msikivu na mvumilivu
- Lazima awe mtu wa kutosheka na kukubali uhalisia wa maisha yake
- Ni lazima ajikubali mwenyewe
- Ni lazima awe na ujasiri wa kuyasimamia maono yake
- Ni lazima awe na marafiki wanaoelekea njia moja naye
- Ana hofu anapokosea (hapendikukosea)
- Anaishi na watu wote kwa upendo
- Msafi wa mwili na mavazi
- Asiyeropoka ovyo, anatunza kinywa chake
- Asiye na mizaha
- Anayependa kucheza na wenzake (wakati wa kucheza)
- Anayefuatilia mambo yanayohusu masomo anayosoma
- Anayefuatilia maswala muhimu ya kitaifa na kimataifa.
- Anayemwamini Mungu
- Mwenye ujasiri (cconfidence)
- Anayejiepusha na dhambi na uovu wa aina yoyote.
- Anayekubali kuadhibiwa akikosea
- Anayezijua haki zake
- Anayeishi vizuri na wazazi wake (Mchapakazi nyumbani)
- Anayefuata ipasavyo mbinu za kusoma na kujisomea anazopewa na waalimu wake.
- Anayejishughulisha na shughuli zote za darasani (anaandika nots, anafanya mazoezi, anafanya mitihani, anauliza maswali, anasoma vitabu nk
No comments:
Post a Comment