Wednesday, 4 September 2013

WITO WA WOKOVU NI WA WOTE, USIJARIBU KUJITOA.

Kuna watu hujaribu kusema Yesu ni kwa ajili ya watu fulani tu, wengine husema Yesu ni wa Wayahudi, wengine husema ni wa walokole, wengine husema ni wa wakristo tu na madai mengine mengi. 
Kimsingi, Madai haya sio ya kweli kibiblia. Wayahudi walihusika kumpokea Yesu na kuwafungulia mataifa mlango. (Yoh. 1:12), Walokole (jina sahihi ni waliookoka) ni watu walioamua kumpokea Yesu na kuyaishi maisha ya ukristo, Wakristo ni mjumuiko wa watu waliojenga imani kwa Kristo (mmiliki wao ni Kristo-wanaitwa kwa jina lake. Hebu tuone Bibila inavyosema kuhusu Yesu:
Yohana 3:16, .........kila amwaminie asipotee bali awe na uzima wa milele" Hapa Biblia inatumia neno "kila" kumaanisha hakuna asiyestahili katika hili endapo yuko tayari kuamini.
Matendo. 4:12, Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo."
 Naamini unaona jinsi maneno haya yanavyotuambia, kwamba Jina la Yesu ni kwa ajili ya wokovu wetu sisis sote. Katika Yohana 3:16, Yesu anasema, "Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele." Natamani uone tu maneno "kila mtu" kwa hiyo kama wewe ni mtu ujue wokovu unakuhusu
2 Petro 3:9 "Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba" Bado Mungu anasisistiza kwamba yeye hapendi mtu yeyote apotee bali atubu. 
John 6:37 Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe.
Kupitia mistari hii tunaona jinsi Mungu alivyo na makusudi na maisha ya kila mmoja wetu. Katika Math. 11:28 anaita na kusema, "Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha." Je, ni mizigo gani inawatesa na kuwasumbua watu siku za leo? Naamini utakubaliana nami kwamba mizigo hii ni ya shetani na hatutakiwi kuibeba. Ni lazima tukubali kumpa Yesu mizigo hiyo ili sisi tuishi maisha ya uhuru na amani. Mistari hii tuliyoisoma inaonesha hasa kwamba mpango wa Mungu wa wokovu ni kwa wote,
Romans 3:23 "kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;"

Romans 5:12 "Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi;"
Mistari hii inaendelea kueleza juu ya hali ya dhambi tuliyozaliwa nayo, dhambi ile iliyofanya na Adama na Eva. Kuokoka basi ni swala la wote.

 KUOKOKA ni kupatana na Mungu kwa njia ya Yesu Kristo. [kumrudia Mungu]
 Kolosai2:14-15, -[Akaifuta hati ya kutushtaki….]
Effeso.2:14-15,-[Akakibomoa kiambaza cha kati kilichotutenga….]
1yoh.4:10,-………, Akamtuma mwanawe kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu.
2kor.5:19,-..Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake amee, asiwahesabie makosa yao; naye ametia  ndani yetu neno la upatanisho.
1Petr 3:18. {Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja Kwa ajili ya dhambi, mwenye haki Kwa ajili ya wasio haki, ili atulete kwa Mungu; …..}

    KUOKOKA ni Kumkiri Yesu kwa kinywa na kuuamini ufufuo wake.
 Warumi 10:9-10. {Kwa sababu ukimkiri Yesu Kwa kinywa chako ya kuwa Ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu UTAOKOKA. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata HAKI, na kwa kinywa hukiri hata kupata WOKOVU.}

     KUOKOKA ni Kumwamini Yesu [kumpokea Yesu] na kutubu dhambi na kuziacha; na kuupokea uwezo wa  kufanyika mwana wa Mungu. 
Yoh.3:16. {Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili  kila amwaminie asipotee, bali awe na uzima wa milele}
Yoh.1:12. {Bali wote waliompokea aliwapa uwezo WA KUFANYIKA WATOTO WA MUNGU, ndio wale waliaminio Jina Lake.}
KUOKOKA ni kuamini habari za Yesu (Injili) na kubatizwa katika mauti yake. Marko 16:16 Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa. 
Warumi 6:4 Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima. 
Wakolosai 2:12 Mkazikwa pamoja naye katika ubatizo; na katika huo mkafufuliwa pamoja naye, kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua katika wafu.

Ni muhimu sana ukaelewa kwamba ubatizo ni tendo la muhimu sana kwa kila mwamini, sio jambo la hiari ni agizo la Mungu kwamba watu wahubiriwe injili na wabatizwe. Mathayo28:19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu. 
Kwa hiyo wokovu wako hauwezi kukamilika kama hujauthibitisha kwa tendo la ubatizo. Katika kitabu cha Marko limewekwa wazi zaidi kwamba "Aaminiye na kubatizwa ataokoka" siyo kuamini tu kama wengi wanavyodai.
 Jambo la muhimu la kujua kuhusu ubatizo pia ni kwamba sio aina zote za ubatizo zinazokubalika mbele za Mungu kutokana na kusudi la ubatizo wa kweli. Ubatizo wa kweli ni ule unaosimamia misingi ya mitume na manabii kama watu waliotumika kuweka misingi ya imani ya kweli. Waefeso 2:20 Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni. Ubatizo waliobatiza mitume ndio ubatizo unaostahili kutumika siku za leo.
Je ubatizo huo ulikuwa na sifa gani?
  1. Ulifanywa na watu waliookoka, mitume na watumishi wengine walioamini hapo kwanza.
  2. Ulifanywa na watu waliojazwa na Roho Mtakatifu
  3. Ulifanywa kwa watu walioamini, wanaojitambua (wenye umri wa kutosha), waliosikia neno, walio tayari kumwishia Yesu.
  4. Ulifanywa kwenye maji mengi, kwa kusudi la kudhihirisha tendo la kuzamishwa likimaanisha kuzikwa na kufufuka pamoja na Kristo.  Warumi 6:3 Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? Yesu mwenyewe kama kielelezo cha imani yetu alibatizwa kwenye mto Yoridani. Marko 1:9 Ikawa siku zile, Yesu alikuja kutoka Nazareti ya Galilaya, akabatizwa na Yohana katika Yordani. Watu wengine pia walibatizwa katika mto huo, Mathayo 3:6 naye akawabatiza katika mto wa Yordani, huku wakiziungama dhambi zao.  Ukijifunza kwenye kitabu cha matendo pia utaliona jambo hili kwa undani zaidi.
Ni muhimu sana ukapeleleza ubatizo uliobatizwa usije ukawa mmoja kati ya watu wayapinduao maandiko. Hakuna dhambi mbaya kama kufundisha uongo na kuwadanganya watu wayaamini mambo yasiyo mapenzi ya Mungu. Kumbuka wokovu ni swala la mtu binafsi, hakikisha unasimama wewe kama wewe na kuyasimamia mapenzi ya Mungu.
  • Wokovu ni mpango wa nani? ``Mwanadamu au Mungu?
     Baadhi ya watu hudhani kwamba ni uamuzi wa wanadamu tu kuzungumza habari za kuokoka duniani, wengine hudiriki kusema, hakuna wokovu duniani.
Je, neno la Mungu linasemaje kuhusu swala la wokovu kwa mwanadamu? [Tazama, wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama, siku ya WOKOVU ndiyo sasa.] 2kor.6:2
Tena Yesu akasemaEnendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ATAOKOKA; asiyeamini, atahukumiwa. Tena katika Zab.16:3-Mungu anasema, Watakatifu walioko duniani ndio walio bora, hao ndio niliopendezwa nao.
    1Pet.1:6-´´Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.``
  •       KWA HIYO:
*    Wokovu ni mpango wa Mugu wa kumvuta na kumtoa  mwanadamu kwenye maangamizo ya dhambi na kumwingiza katika eneo alilolikusudia kwa njia ya imani.
Yeremia 31:3 -Mungu anasema,-´´Naam, nimekupenda kwa upendo wa milele, ndio maana nimekuvuta kwa fadhili zangu.``
Yohana.3:16- “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele”.
       Math.1:21. “………, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.”
      Yoh.1:29-“Tazama Mwanakondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu”.

*    Wokovu ni mpango wa Mungu kumtoa mwanadamu Kwenye  mauti na kumwingiza kwenye uzima. Warumi 6:23,            “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.”
Yoh.5:24. Yesu akasema, “………, yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yu na uzima wa milele; wala  haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani.
Yoh.8:51, “Amin, Amin, nawaambia , mtu akilishika neno langu, hataona mauti milele.”
1pet.3:18, “Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu…..”

*   Wokovu ni mpango wa Mungu kumtoa mwanadamu kwenye ufalme wa giza [Utumwani]: penye dhiki, mateso, laana, vifungo, na maonezi yote ya ibilisi, na kumwingiza kwenye ufalme wake ulio chini ya Kristo Yesu ili apate kuwa huru.
Wakolosai.1:13, “Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika katika ufalme wa mwana wa pendo lake.``
Yoh.8:36, “Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.”
Yoh.8:34,- Yesu anasema,-Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.``
1Yoh.3:8,-´´Atendaye dhambi ni wa ibilisi, kwa kuwa ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za ibilisi.``

*   Wokovu ni mpango wa Mungu kumponya, kumfinyanga , kumtakasa , na kumfanya mwanadamu mwenye tabia ya asili  kwa upya kabisa kwa kumtoa Yesu ili awe fidia ya dhambi zote alizozitenda; na kumfanya kiumbe kipya chenye nafasi ya kuitwa Mwana [mototo]  wa Mungu .
Isaya.53:5, Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, alichubuliwa kwa maovu yetu. Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.” >> 1pet.2:24.
Yoh.1:12, “Bali wote waliompokea aliwapa uweyo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake.” 
2kor.5:17, “Hata imekuwa mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.”

                 MKUBALI YESU LEO AKUOKOE!!!

No comments:

Post a Comment

MWANAUME KWENYE NAFASI YA "MUME"

Mume ni mwanaume aliyeoa kwa kuzingatia vigezo na taratibu za kijamii, kishria na za kiroho. Mume si rafiki wa kiume (boyfriend), hawara, wa...

Powered By Blogger