Wednesday, 21 September 2016

DHAMBI(SIN) NI NINI?


Neno Dhambi linadhihirika katika maandiko kama mjumuiko wa uovu, mabaya, hatia, makosa, ukengeufu na uasi. Vifungu vifuatavyo katika biblia vinatupa upana wa tafsiri hii:
Zaburi 51:1-9
“Ee Mungu, unirehemu, Sawasawa na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, Uyafute makosa (Transigressionon)yangu. Unioshe kabisa na uovu (iniquity) wangu, Unitakase dhambi (Sin) zangu. Maana nimejua mimi makosa yangu Na dhambi yangu i mbele yangu daima. Nimekutenda dhambi Wewe peke yako, Na kufanya maovu mbele za macho yako. Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo, Na kuwa safi utoapo hukumu.
Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu; Mama yangu alinichukua mimba hatiani. Tazama, wapendezwa na kweli iliyo moyoni; Nawe utanijulisha hekima kwa siri, Unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi, Unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji.  Unifanye kusikia furaha na shangwe, Mifupa uliyoiponda ifurahi. Usitiri uso wako usitazame dhambi zangu; Uzifute hatia zangu zote.”
Maneno ya asili (Ya Kiebrania)yaliyotumika kwenye maneno haya ni
Þ    Kwa neno Makosa (transigression) ni neno ‘peša’ likimaanisha ‘rebelliousness’ kufanya kinyume na utaratibu au uasi.
Þ  Kwa neno Uovu (Iniquity) limetumika neno ‘hātā’ linalomaanisha ‘moral misshapennes’ yaani kinyume na maadili ya ki-Mungu kwa makusudi. Neno hili limetumika mara 580 katika Agano la kale.
Þ    Neno sin limetokana na neno ‘āwōn’ linalomaanisha ‘shorticomings’Kupungukiwa na utukufu wa Mungu.
Katika Agano jipya yametumika maneno  ya Kiyunani mawili:
Neno ‘adikia’ linalomaanisha kufanya makosa (wrongdoing), kinyume na haki (Unrighteousness), na kinyume na sheria (Injustice). Katika kundi hili, dhambi inaonekana kuwa kitendo cha hiari anachokifanya mtu, kinachoweza kuleta madhara au uharibifu kwa mtu mwingine.
Neno jingine ni ‘hamartia’ ambalo limetafsiriwa mara nyingi kama Dhambi (Sin). Kundi hili la dhambi linajumuisha maneno yote ya Kiebrania yaliyotumika katika Agano la kale (yaani ‘āwōn’, ‘hātā’ na ‘peša’).

Dhambi (Sin) katika agano Jipya inamaanisha kukosa maadili ya ki-Mungu (Makosa), maovu na uasi mbele za Mungu.

1 Yoh. 3:4 Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi (rebellion). Kuasi ni kukiuka kwa makusudi taratibu au sheria zilizowekwa na mamlaka Fulani, ni kwenda kinyume na maagano au mapatano. Hili tunaliona kwenye kitabu cha mwanzo pale ambapo Adamu na Eva waliamua, japo kwa kudanganywa na shetani, kula tunda la mti ambao Mungu aliwakataza. (Mwanzo 3)
1 Yoh. 5:17 Kila lisilo la haki ni dhambi, na dhambi iko isiyo ya mauti.
Warumi 14:23 “… Na kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi.”

Mithali 24:9 Fikira za mpumbavu ni dhambi, Na mwenye mzaha huwachukiza watu.
Mithali 21:4 Macho yenye kiburi, na moyo wa kutakabari, Hata ukulima wa waovu, ni dhambi.
Ayubu 23:11 Mguu wangu umeshikamana sana na hatua zake; Njia yake nimeishika, wala sikukengeuka.
Kumb.11:28 na laana ni hapo msiposikiza maagizo ya Bwana, Mungu wenu, mkikengeuka katika njia niwaagizayo leo, kwa kuandama miungu mingine msiyoijua.
Dhambi imetafsiriwa tena kama “Matendo ya mwili”
Wagalatia 5:19 inasema, “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.
Tena, Dhambi ni Ibada ya sanamu. Wakolosai 3:5 “Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu; kwa ajili ya mambo hayo huja ghadhabu ya Mungu.”

Kuna tofauti kati ya dhambi kwenye Agano la kale na dhambi wakati huu wa Agano la Jipya.
Dhambi katika Agano la kale ilikuwa ni kule kuvunja sheria (Torati ya Musa), na kwenda kinyume na taratibu za dini ya Kiyahudi. Amri kumi za Mungu ndizo zilikuwa kielelezo cha Amri zote. Katika Warumi 4:15 mtume Paulo anatuambia “Kwa sababu sheria ndiyo ifanyayo hasira; maana pasipokuwapo sheria, hapana kosa.” Kwa hiyo kumbe watu walianza kuhesabiwa makosa pale sheria ilipowekwa.

Katika Agano la kale sheria na hukumu zake zilikuwa mikononi mwa waalimu wa Dini na Mafarisayo. Na walikuwa na uwezo wa kumhuku mtu yeyote kulingana na sheria hizo. Kwenye Waebrania 10:28 tunasoma “Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu.” Kwa hiyo watu wengi walikufa – utaratibu ulikuwa jino kwa jino, atakayeua kwa upanga atauwawa kwa upanga.

Warumi 8:3 Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili
Wakolosai 2:23 Mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana hekima, katika namna ya ibada mliyojitungia wenyewe, na katika kunyenyekea, na katika kuutawala mwili kwa ukali; lakini hayafai kitu kwa kuzizuia tamaa za mwili.

Paulo akizizungumzia taratibu za ibada ya Kiyahudi katika Wakolosai 2:23 akasema, “Mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana hekima, katika namna ya ibada mliyojitungia wenyewe, na katika kunyenyekea, na katika kuutawala mwili kwa ukali; lakini hayafai kitu kwa kuzizuia tamaa za mwili.
 Katika agano jipya dhambi ina upana zaidi.

Yale yaliyokuwa magumu kwa sababu ya sheria sasa katika Kristo Mungu anayafanya mepesi. Warumi 8:3 inasema “Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili”

Yesu alitangaza mfumo mpya wa maisha ya Kiroho.
Mathayo 5:23-48 “Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako, iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako……….   Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini; lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake……..Imenenwa pia, Mtu akimwacha mkewe, na ampe hati ya talaka; lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila mtimizie Bwana nyapo zako lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa; hata kwa mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu; wala kwa nchi, kwa maana ndiyo pa kuwekea miguu yake; wala kwa Yerusalemu, kwa maana ndio mji wa Mfalme mkuu.

Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi. Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu. Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino; Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili. Na mtu atakaye kukushitaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia. Na mtu atakayekulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye mbili. Akuombaye, mpe; naye atakaye kukopa kwako, usimpe kisogo. Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako; lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi, ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.
 Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo? Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo? Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.

Maeneo yaliyopigiwa mstari yanaonyesha hali ilivyokuwa kipindi cha sheria, lakini tunaona Yesu akitangaza mambo mapya na kusema, “lakini mimi ninasema” Kwa hiyo sasa tunasimama katika yale aliyoyasema Yesu yaani; Kuacha na kukaa mbali kabisa na zinaa, kutokuachana, kutokuapa, kuwapenda maadui na kuwaombea.
Tena katika Mathayo 22:37-39 Yesu akatangaza amri kuu mbili, “Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako.”

Katika sheria ni hapakuwa na kumpenda jirani kama nafsi, wa kukaa naye ni Yule tu ambaye alikuwa amekubalika kutokana na Torati. Kwa sababu hiyo Wayahudi walilazimika kujitenga na wanadamu wengine wote waliokuwa wanaabudu sanamu. Hapakuwa na kuchangamana.
Yesu alipokuja sasa tunaambiwa:
Waefeso 2:14 Kwa maana yeye (Yesu) ndiye amani yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja; akakibomoa kiambaza cha kati kilichotutenga.
2 Wakorintho 5:17 Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.

Wagalatia 2:16 hali tukijua ya kuwa mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria, bali kwa imani ya Kristo Yesu; sisi tulimwamini Kristo Yesu ili tuhesabiwe haki kwa imani ya Kristo, wala si kwa matendo ya sheria; maana kwa matendo ya sheria hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki.
Warumi 8:1 Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.

Warumi 6: 17-23 “Lakini Mungu na ashukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mliitii kwa mioyo yenu ile namna ya elimu ambayo mliwekwa chini yake; na mlipokwisha kuwekwa huru mbali na dhambi, mkawa watumwa wa haki.  ….  Kwa kuwa kama mlivyovitoa viungo vyenu vitumiwe na uchafu na uasi mpate kuasi, vivyo hivyo sasa vitoeni viungo vyenu vitumiwe na haki mpate kutakaswa. Kwa maana mlipokuwa watumwa wa dhambi, mlikuwa huru mbali na haki. Ni faida gani basi mliyopata siku zile kwa mambo hayo mnayoyatahayarikia sasa?
Kwa maana mwisho wa mambo hayo ni mauti. Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa, na mwisho wake ni uzima wa milele. Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.”


No comments:

Post a Comment

MWANAUME KWENYE NAFASI YA "MUME"

Mume ni mwanaume aliyeoa kwa kuzingatia vigezo na taratibu za kijamii, kishria na za kiroho. Mume si rafiki wa kiume (boyfriend), hawara, wa...

Powered By Blogger