Saturday, 21 March 2020

MAARIFA YA MUNGU HULETA MAHUSINO MAZURI KATIKA FAMILIA


Maarifa ni uwezo wa kutumia ufahamu ili kusababisha mabadiliko au matokeo mazuri au mafanikio.  Unaweza ukawa ni ufahamu wa kiroho au ufahamu wa kawaida wa kibinadamu. Kuwa na ufahamu tu hakutoshi, bali ni lazima mtu aweze kuutumia huo ufahamu vizuri kwa ajili ya maisha ya kila siku. Chanzo cha maarifa yote ni uchaji mbele za Mungu (Mithali 1:7) Yaani kuwa na hofu ya Mungu kunakodhihirika katika ibada na utii katika neno lake. Katika maisha yetu yapo mengi yanayohitaji maarifa na hekima ya Mungu. Maarifa huleta hekima na hekima hutuwezesha kuishi vizuri na watu, hivyo kuwa na maisha ya furaha na amani.

Katika Muhubiri 11:8-9 Maandiko yanasema,

Naam, mtu akiishi miaka mingi, na aifurahie yote; lakini na azikumbuke siku zijazo za giza, kwa maana zitakuwa nyingi…..Wewe kijana, uufurahie ujana wako, na moyo wako ukuchangamshe siku za ujana wako, ukaziendee njia za moyo wako, na katika maono ya macho yako, lakini ujue wewe ya kwamba kwa ajili ya hayo yote Mungu atakuleta hukumuni.”

Katika mistari hii tunajifunza kwamba ni mpango wa Mungu tuifurahie miaka yote ya maisha yetu, ikiwepo miaka ya utoto, ujana, utu uzima na uzee. Swali langu ni kwamba, “Ni kwa nini vijana na watoto wengi wanaishi maisha ya huzuni, majuto, maumivu makali moyoni, migogoro, chuki, dhiki nk? Katika kutafakari nikagundua kwamba ipo shida kubwa kwenye mahusiano kati ya watoto/vijana na wazazi/walezi. Watoto wengi wamewaumiza wazazi/walezi wao kwa tabia zao mbaya za dharau na dhambi, kwa upande mwingine nao wazazi/walezi wamewaumiza watoto/vijana kwa kutotimiza wajibu wao na kuwatendea mabaya.

Tena katika Hosea 4:6 Mungu anasema, “Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.” Kukosa maarifa ya Mungu katika kujenga mahusiano ya kifamilia imekuwa ni tatizo kubwa kwa dunia, katika kizazi hiki. Kwa sababu hiyo shetani anazidi kuangamiza kizazi hiki kwa kasi sana.

Kwenye isaya Isaya 5:13 tunasoma matokeo mengine mabaya sana yanayoletwa na kukosa maarifa ya ki-Mungu, hapo tunasoma, “Kwa sababu hiyo watu wangu wamechukuliwa mateka, kwa kukosa kuwa na maarifa; na watu wao wenye cheo wana njaa, na wengi wao waona kiu sana.” Kumbe kwa kukosa maarifa ndipo tunaweza kuona jinsi ambavyo kizazi hiki kimeingia katika uteka wa Ibilisi kupitia mifumo ya kisasa ya maisha. Maeneo mengi watu wanalia kuhusu tabia za watoto wa kizazi hiki.

Wazazi/walezi wamekuwa na wakati mgumu sana katika malezi ya watoto wao. Hapa dawa ni Mungu aingilie kati, maombi na sala pamoja na kuwekeza kwenye kuwajaza maarifa ya Mungu ndilo suluhisho la kudumu. Uteka hauvunjiki kwa vikao na adhabu, au kutishiwa kufungwa gerezani; Mungu ndiye mwenye uwezo wa kuwaweka huru waliosetwa katika mateka ya Ibilisi.

Katika Luka 4:18 Yesu anasema, “Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa” Watoto/vijana wetu wengi wanahitaji mguso wa Mungu watoke katika vifungo vilivyowafunga. Nimeshuhudia matukio mengi katika shule ambazo nimepita, watoto wengi watukutu wanakuwa wana uvamizi wa kipepo ndani yao, si wao katika hali ya kawaida. Kwa maombi yetu na jitihada zetu za kuwafundisha ili wajae maarifa ya kiMungu, ndivyo vitakavyoleta mapinduzi.

Shetani anashughulika kuwazuilia watoto/vijana maarifa ya Mungu ili apate kuwachota kwa urahisi kila siku. Katika Mithali 1:7, tunasoma,  “Kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa” Ukiangalia katika kizazi hiki watoto na vijana wengi wamejaa mambo machafu sana, haya mambo ndiyo yanayochafua kabisa mahusiano na wazazi na kuwafanya watoto/vijana waingie kwenye uteka wa Ibilisi. Maswala ya mitandao yamechochea sana uasherati kwa kizazi hiki, siku hizi ni kawaida kukuta binti mdogo waa shule ya msingi ameshaanza maswala ya mapenzi.

Kwenye Mithali 1:28-29 tunaona matokeo mengine mabaya YA kuyakataa maarifa ya Mungu, Neno linasema, “Ndipo watakaponiita, lakini sitaitika; Watanitafuta kwa bidii, wasinione. Kwa kuwa walichukia maarifa, Wala hawakuchagua kumcha Bwana.” Hakuna mwanadamu asiyemwitaji Mungu katika mambo mbalimbali ya maisha yake. Hapa tunaona hali ya hatari inayojitokeza kizazi kinapokuwa na watu walioyakataa maarifa ya Mungu. Kwanza maombi hayatasikiwa na Mungu, pili, Mungu hawezi kuonekana wakati anahitajika. Hivyo ni lazima kila mtu akajua ana wajibu wa kutafuta maarifa ya Mungu ili kwa hayo tuweze kufanya mambo kwa hekima na ufahamu mzuri.

Wito wangu kwa wazazi, waalimu, viongozi, mitume, wachungaji, manabii, jamii na serikali ni kwamba kila mmoja aiangalie nafasi yake. Tuna jukumu la kuhakikisha kwamba watoto na vijana wetu wanazidi kupata maarifa ya Mungu,wanapoendelea kusoma katika elimu mbalimbali. Tusipuuze mambo ya Mungu; vipindi vya dini mashuleni vipewe nafasi yake. Watoto na vijana wasisitizwe kwenda kwenye nyumba za ibada. Vifaa vya kujifunzia elimu ya kiroho navyo vipatikane kwa wingi. Tena kila mmoja wetu awe mfano bora kwa watoto na vijana wetu. Vijana nao wawe tayari, na waamue kuwekeza muda wao katika kujifunza. Wawaheshimu viongozi na waalimu wa kiroho kama inavyowapasa. Hili litadumisha mahusiano kati yao na Mungu, kisha kati yao na wazazi/walezi.

Mungu awabariki,

Mwl. Stephen Swai
Simu: +255713511544

JINA LA YESU KRISTO NI ZAIDI YA MAJINA YOTE, UVIKO - 19 (CORONA) ISIWE TISHIO

USIOGOPE! USIOGOPE! USIOGOPE!

Hapa duniani yapo mambo mengi ya kuogopesha, ya kukatisha tamaa, ya kuumiza, hata ya kutufanya tusione kabisa maana ya maisha haya tunayoishi. Katika historia pia yalishatokea matukio ya kutisha, tukikumbuka mambo kama Sunami, Septermber 11, huko Marekani, vimbunga, matetemeko ya ardhi kwa majina yake; vita vya kwanza na vya pili vya dunia; magonjwa kama vile Ebola, UKIMWI, Kansa, na mengine yamekuwa tishio. Mambo haya yalihusisha nguvu za asili, utendaji wa wanadamu na mengine yalisababishwa na vijidudu visivyoweza hata kuonekana (Virusi, bakteria, na vingine). 

Ni Jambo la kushangaza kuona virusi, ambavyo ni wadudu wasioonekana, kuleta taharuki na mtikisiko mkubwa duniani kote.  Virusi vya HIV vimeitikisa dunia kwa muda mrefu sasa; virusi vya Ebola, na sasa hivi tunatikiswa na virusi vinavyosababisha ugonjwa wa UVIKO - 19 (COVID - 19), yaani virusi vya CORONA (CORONA VIRUS).  Ninachotaka kusema hapa ni nini? Nataka kusema kwamba udogo wa virusi hauvipunguzii uwezo wake wa kuleta madhara. Tena uwezo wake unachangiwa zaidi na umbile lake, ijapokuwa ni dogo. Virusi vya CORONA vinasemekana kuwa vina umbo la taji ya kifalme. Umbo lake linasababisha virusi hivi viweze kusambaa kwa haraka kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Madhara yake yameelezwa kuendelea kuwa makubwa siku kwa siku. Hivyo, kama hatuna msimamo thabiti wa imani ni lazima mtikisiko huu utuletee madhara makubwa.

Virusi hivi viligunduliwa na kuanza kusambaa katika mji wa Wuhan huko China. Baada ya muda mfupi usiozidi miezi mitatu tangu vigunduliwe, virusi hivi viliweza kuigusa dunia nzima. Nchi zaidi ya 114 zilikuwa zimeripotiwa kuwa na waathirika wa virusi hivi; huku China, Italia, na Marekani zikiongoza kwa kuwa na waathirika wengi zaidi. Baadhi ya nchi za Afrika nazo zimeripotiwa kuwa na visa vya watu walioambukizwa virusi hivi. Nchi kama Kenya, Tanzania, Afrika Kusini, Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Ghana na nyinginezo. Hakika UVIKO -19 imaitikisa dunia. Ni ukweli usiopingika kwamba hofu na mashaka vimewajaa watu wa kila taifa katika dunia hii. Wengi hawana uhuru tena hata wa kutembea hapa na pale, shule zimefungwa, michezo imesitishwa, kumbi zimefungwa, mikusanyiko imekatazwa nk. Hii yote ni kuonyesha jinsi ambavyo hofu imetanda kwa wanadamu.

  Leo nataka nikuletee habari njema. Na nianze kwa kukuuliza "YANINI KUOGOPA?" Unaweza kunijibu tu kirahisi kwamba unaogopa KIFO. Ni kweli kifo ni kitu cha kuogopesha na hakuna mtu anayependa kufa. Ila jiulize tangu dunia iwepo ni wangapi wamekufa? Jibu ni wengi, hawahesabiki. Kifo kimekuwepo, kipo na kitazidi kuwepo. Habari njema ni hii "TUNAYE YESU KRISTO ALIYESHINDA KIFO NA MAUTI" Yeye ni zaidi ya kila kitu. Jina lake liko juu ya majina yote. Yaani liko juu ya jina la Uviko-19 na mengineyo yote. Tukimwamini Yeye tuna uhakika wa kuishi milele. Yeye ni Alfa na Omega, wa kwanza na wa mwisho. Kwa kupigwa kwake sisi sote tumepata kupona (Isaya 53:5) Kila anayemwana Yesu Kristo hana haja ya kuogopa, Yesu ndiye mkombozi na mwokozi wa maisha yetu.

Ndugu zangu, hatuna haja ya kuogopa ugonjwa huu wa UVIKO-19, tuchukue tahadhari kama tunvyoelekezwa na wataalamu lakini tusiogope kwani Mungu wetu zaidi ya kila kitu. Aliyeko ndani Yetu ni mkuu kuliko walio nje. Maandiko yanasema Kwa Jina lake dunia nzima inapata kuokolewa (Matendo 4:12) Ni vema tukamwamini Mungu kuliko kuogopa. Shetani asitujaze hofu, tujue kwamba uhai wetu uko mikononi mwa Mungu. Anayetulinda usiku na mchana ni Mungu peke yake, hatuwezi kujilinda wenyewe. Nirudie tena, "Hatuna haja ya kuogopa" tuhakikishe tu kwamba tuna ushirika mzuri na Mungu, tuombe kwa bidii na kuendelea kumtumaini Mungu. Hakuna haja ya kukosa tumaini na kuona kwamba huwezi kuishi tena. Kirusi cha KORONA si mwamuzi wa maisha yetu. Mwamuzi wa mwisho wa maisha yetu ni Mungu aliyetuumba.

Katika jitihada za wanadamu kutafuta tiba ya kutibu ugonjwa huu, hakujawa na matumaini ya kutosha bado. Japo kuna chnjo za aina mbalimbali zimegunduliwa, hakuna hata moja inayoweza kuaminiwa kwa asilimia mia moja. Hii inathibitisha kwamba ni Mungu peke yake anayeweza kutulinda na kutuhifadhi salama mbele ya mjumbe huyu wa shetani aliyetumwa kuitawala dunia. Ni lazima tukatae kukaa chini ya uweza wa kitu chocho, na tuamue kukaa chini ya uweza wa Mungu peke yake. Kwa mwamini wa kweli Uviko-19 haliwezi kuwa tatizo la kusababisha kupoteza matumaini. Bado aliyeanzisha maisha yetu hapa duniani yuko hai na anaweza kutulinda. (Zaburi 127:1)

Mwisho niseme hizi ni nyakati za mwisho, yapo mengi ya kututikisa, huu ni mwanzo tu wa uchungu. Tunapoelekea yatatokea mengine mazito zaidi. Yote haya yalitabiriwa katika maandiko (Mathayo 24), matetemeko, vita, magonjwa, na mengine. Wapendwa ni muda wa kujiandaa, Yesu yu karibu kurudi. Huu si muda wa kuendelea kukusanya mali na kumsahau Mungu, si muda wa kuendekeza mijadala ya kidini isiyo na faida, wala si muda wa kuwaangalia watu; ni muda wa kujichunguza kila mmoja na nafsi yake. Kila mmoja atasimama mbele ya kiti cha hukumu peke yake. Wahubiri: huu si muda wa kuhubiri ili kupata fedha, tena si muda wa kufundisha mafanikio ya kimwili; ni muda wa kusahau nafsi zetu na kuwa dhabihu kwa ajili ya kanisa la Mungu na ulimwengu kwa ujumla.

Tunaelekea kwenye nyakati ambazo dunia inahitaji faraja kutoka kwa Mungu. Na faraja hiyo ni lazima ipitie kwa kanisa lake (yaani mimi na wewe). Kanisa linakwenda kuwa mahali pa makimbilio kwa watu waliojikuta wanaabudu mashetani wakifikiri wanamwabudu Mungu. Utatokea ufunuo usio wa kawaida baada ya siku hizi chache, macho ya wengi yataona nuru lakini waliopewa nuru wengi watakuwa wamepoteana. Tusiviangalie vya dunia hii na kusahau ile amana tuliyowekewa na Mungu kwa ajili ya watu wake. Nafasi ya mtumishi wa Mungu katika dunia hii ni kubwa, japo watu wengi wanafanya mchezo na utumishi. Leo ni Uviko - 19 (Korona) lakini kesho hatujui ni nini kitatokea. Tusimame imara, tusiogope, tuishi kwa kumtegemea Mungu wala tusiangali vitisho vya shetani; hapa duniani hatuna mji udumuo, tuko kwa kitambo kidogo tu.

Nakuombea Mungu akulinde na akuepushe na ugonjwa wa UVIKO 19 (COVID-19); Mungu alilinde taifa letu la Tanzania, pamoja na mataifa mengine. Mungu awaponye wagonjwa walio mahospitalini, na awafariji wote waliofiwa kutokana na  ugonjwa huu. Amina.

Tuesday, 18 February 2020

HONOR GOD WITH YOUR WEALTH

Wealth is defined in Concise Oxford Dictionary as an abundance of valuable possessions or money. Although seeking wealth is the REASON for struggle in this world, it was not the first plan of God since creation. In addition to struggling for wealth, people are struggling for fame (honor) or position and good life. Disregarding the fact that God is the source of everything, many have forgotten the Living God and live a sinful life.  Pastor John Mkumbo, in his sermon titled “Honor God with Your Wealth” referring to Proverbs 3:9, He taught about beginning everything with God for success in the Kingdom of God. Then, he illustrated his sermon by a story about Mr. Mwanseles’s family which ended in serious tragedy.

He said, “Mr. and Mrs. Mwansele were unique couples in Umoja village. They live happily with their three children; Henry, Jane and Grace. They made a very admirable Christian Family. All the people in the village could tell the good story of Mwansele’s family. Mr. Mwansele was a church Elder while Mrs. Mwansele was a chairperson, leading The Women for Christ Fellowship (WCF). They lived in the most beautiful house in the village. Because of his faithfulness in the church, Mr. Mwansele became the closest friend of Pastor Mwakalinga. Their kindness attracted many people to accept the Gospel of Jesus Christ. Indeed, his family was a living testimony for the love of Christ. Now and then, Mr & Mrs Mwansele offered food to the needy. They acted their faith. They knew “It is better to give than to receive.”

By the year 2014, their first born, Henry was in his Advanced level studies, Jane was in Ordinary level and Grace was almost finishing her primary education. During December holidays they all came home to see their parents. What a wonderful moment they had!? Mr. Mwansele decided to take his family out on a picnic. Around evening, he took them to his friend Mustafa, who invited them for a dinner. Henry, Jane and Grace were very happy because they were going to their very close friend who was studying abroad.  On the way, Grace who was very prayerful young girl, started to narrate about a dream she had in the previous night. At first, her brother, who seated close to her in the back seat tried to stop her but she insisted that the dream was so important. “I dreamt of something very terrifying” she said. What is it? Daddy asked. Then confidently, she started narrating.

“I saw a very big snake nearby our house, and then I started shouting for help. You, I mean, you mum, daddy, you and you” opened the door and came out to see what was happening. What shocked me was that the snake started to grow big. In a blink of an eye, it came towards us and started swallowing us.  “Who was swallowed?” Henry interrupted. Jane was first, then dad, when he was trying to kill the snake. I was just crying! Crying loudly calling Jesus to serve us. Then snake started coming towards me, I had nowhere to go, mother had already left. When the snake opened its mouth to swallow me, I don’t know what happened, I found myself seated in my bed trembling. That’s when I realised, it was just a dream. In the morning I wanted to share with you but you were all busy.” “Ah! There must be something, we should keep praying.” The mother added.
By the time they were approaching the friend’s home; their happiness had vanished because of that bad dream. “Oh, My God…Lord Jesus, please! Protect my family” Mrs Mwansele prayed as the car halted at Mr. Mustafa’s parking slot. Oh, Mr. Mwansele! You are warmly welcomed” said Mr. Mustafa, while hugging and laughing joyfully. Is our friend, Kerry back? That day was a highly colourful day for Mustafa’s family, since they were visited by their family friends. On the way back home, Grace seemed to be unhappy. “Are you sick or something?” The brother asked. “No problem” she replied. At the time, Mr Mwansele and his wife were making some funny stories, laughing and laughing.  “Ah! You! Why are you fighting, don’t you love each other?” “Henry is booing me!” Grace replied. “Stop it!” Mr. Mwansele ordered.

As the time went by, their small shop grew into the biggest shop in the village. Apart from Mustafa’s family, no other family you could see a car parked in the afternoon. It was real a successful family. His success pulled his heart back from God. He resigned from being a church elder, the wife also resigned from her position. This happened when the Pastor warned them of their new life style which excluded other believers. Mr Mwansele was no longer the one known for his kindness. For him to give was wastage. He was no longer a pillar in the church because he thought he has contributed more than enough. His wife and children were now modernized. They were no longer, villagers. They were all uprooted from the roots of their culture and faith. At the end He stopped going to the church. He spent his time in drinking beer and committing adultery.

    Because of his contribution to the church, Pastor kept going to his house to convince him back to the church. He refused, and he even insulted him. His wife was then something else. She was no longer such a polite and quite woman. When Mr Mwansele came home drunkard, she used to beat him and ‘there was no service in the bed room’ they slaves in their own home. Children were all confused; Jerry decided to join his mother while the little girls were with their father. The family had turned into battle field. Families tried to intervene and reconcile but nothing worked. Mr. Mwansele started selling his possessions, including his car, the shop was closed. At last they ended up in divorce, all HIV positive, children chased from good schools coming back to the village. What a tragedy!”

    Despite that God spoke to them through dream of their daughter, Grace, no one could hear. They were all after their own desires. Moses warned the Israelites of not forgetting their God after they had succeeded. Here he says, Make certain that you do not forget the LORD your God; do not fail to obey any of his laws that I am giving you today. When you have all you want to eat and have built good houses to live in and when your cattle and sheep, your silver and gold, and all your other possessions have increased, be sure that you do not become proud and forget the LORD your God who rescued you from Egypt, where you were slaves.” (Deut. 8:11-13 GNB) Yes, we must put our God first (Math. 6:33), and have fear of the Lord (Prov.22:4) then God in His appointed time will prosper us according to His will.

Tuesday, 11 February 2020

GOD'S JUSTIFICATION ACCORDING TO THE BOOK OF ROMANS 3:24

GOD'S JUSTIFICATION
Justification is referred to as “remission of sin and absolution from guilt and punishment; or an act of free grace by which God pardons the sinner and accepts him as righteous, on account of the atonement of Christ.” (Webster’s 1828 Dictionary) Apostle Paul makes this statement to how our justification occurs. “[We] are justified freely by his grace” (Romans 3:24). In this verse, there three very important ideas to be understood by every Christian; these are words “freely”, “grace”, and the word “justified”.

Beginning with the word “freely” In IST, the righter says “He justifies us freely: This is not from yourselves, it is the gift of God – not by works so that no one can boast (Ephesians 2:8) (Lasley 2015, 195) Paul says “Now to someone who works, wages are not considered a gift but an obligation. (Romans 4:4 ISV) So, we are treated as just not because of our works of law or any qualification, but because of what God has done for us in Jesus Christ our savior. We don’t pay anything for justification; it’s just to believe in Jesus Christ who took our sins on the Cross of Calvary.

It is by “grace” which means “unmerited favour from God”, is not by works of law. As Charles R. Erdman, in his Exposition of The Epistle of Paul to the Romans says, “This is due to no merit on the part of man. The source of this “justification” is the ‘unmerited favour of God’. Men are justified freely by His grace. However, this justifying act on the part of God is not due to any indifferent to sin, nor to his failure to observe moral distinctions. God has made it possible at infinite cost.” (Erdman 1966, 58)

            So, nobody deserves this justification on his own. It is God who declares us righteous after we have accepted Jesus Christ our savior. That is why Paul says, “Knowing that a man is not justified by the works of the law, but ‘by the faith of Jesus Christ’, even we have believed in Jesus Christ, that we might be justified by the faith of Christ, and not by the works of the law: for by the works of the law shall no flesh be justified.”  (Galatians 2:16 KJV)

To be “justified” in Good News Bible is translated as “to be put right with God” and as we have seen no one can be put right with God (or justified) by doing what law requires. It is through redemption that is in Jesus Christ. That’s why Paul concludes, “But by the “free gift of God's grace” all are put right with him through Christ Jesus, who sets them free. God offered him, so that by his blood he should become the means by which people's sins are forgiven through their faith in him.” (Romans 2:23-25 GNB)

            Thus, Justification is by the ‘free gift of God’s grace’ and we are justified (put right with God) or God’s approval (GW) through the redemption that is in Jesus Christ (v.24). In Acts 13: 38-39 Paul says to the Jews, "that through him the forgiveness of sins is proclaimed to you, and that everyone who believes in him is justified and freed from everything that kept you from being justified by the Law of Moses.” 

Luther’s doctrine is one of unconditional justification based on the free grace of God through the creation of faith in the sinner who hears the Gospel and to whom Christ and his righteousness are made present in faith so that Christ’s righteousness is imputed to the believer. (Persons, Michael Jones, Keith G. 2012, 32)

Thursday, 6 February 2020

JIFUNZE KUMTUMAINI MUNGU

"Wanaomtegemea Mwenyenzi - Mungu, wako kama mlima Siyoni, ambao hautikisiki bali wabaki imara Daima" (Zaburi 125 BHN)

Kila aliyeamua kuishi maisha ya kumwamini Mungu ni lazima aidhihirishe Imani yake katika tumaini kwa Mungu siku zote. Mtu asiye na Tumaini ni mtu ambaye hana imani thabiti kwa Mungu. Biblia aintufundisha mengi kuhusu tumaini au tegemeo:
Mfano "Usizitegemee akili zako mwenyewe" (Mithali 3:5), usiwatumainie wanadamu (Yeremia 17:5), usiwatumainie wakuu (viongozi) (Zaburi 146:3), usizitumainie mali (1Timotheo 6:17) na mengine kama hayo. Mungu anataka tumtumaini Yeye peke yake, hili ni la muhimu sana katika maisha ya wokovu. Ni kweli wanadamu wanaweza kukusaidia lakini haikupaswi kuwatumainia. Acha Mungu awatumie kwa wakati wake ili kama ikitokea hawapo wewe uzidi kusonga mbele. Kila siku useme “Bwana ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu nitakayemtumaini.” (Zaburi 91:2)

Hakika “VITA NI VYA BWANA” baada ya kuokoka, wewe ni sehemu ya ufalme wa Mungu duniani (tueingizwa kwenye ufalme wa Mwana wa pendo la Mungu (Wakolosai 1:13) . Hivyo tunalindwa na jeshi la ufalme wa Mungu (Zaburi 34:7), tena tunalindwa na nguvu za Mungu (1Petro 1:5). Ukilielewa hili utakuwa na maisha ya wokovu yenye mafanikio makubwa kiroho na kimwili.

Mara nyingi watu hukwama kwa sababu ya kukosa maarifa (Hosea 4:6). Shetani akijua hatujui haki zetu katika Bwana, atatumia mwanya huo kutuyumbisha kiimani. Nafurahi kwa sababu leo umeshajua kwamba ni haki yako kulindwa na Mungu, usimpe ibilisi nafasi. (Waefeso 4: 27). Mtumaini Mungu hata wakati wa vita. Usilie kama waliavyo wasio na Mungu. Wewe ni mteule wa Mungu, simama imara katika kusudi la Mungu. Watu wanaweza kukuacha lakini Mungu hawezi kukuacha. Yeye anasema, "Nimekuchora katika viganja vyangu; kuta zako naziona daima mbele yangu"  Hakuna asiloliweza Mungu.

Wednesday, 8 January 2020

USAFI KATIKA NDOA YA KIKRISTO


NDOA INAHITAJI USAFI WA ROHO NA MWILI

Uchafu ni kitu cha kuchukiza sana. Hakuna mtu yeyote anayeweza kuchukuliana na mazingira machafu labda awe hana akili. Usafi ni asili ya Mungu, Mungu hachangamani na uchafu wa aina yoyote. Usafi wa kiroho kwa lugha nyingine ni utakatifu. Mungu wetu ni Mtakatifu, chochote kinachotokana naye ni kitakatifu. Yeye alikusudia kila alichokifanya kidumu katika utakatifu. 

Ndiyo maana akakamilisha kazi yake yote ya uumbaji katika utakatifu (dhambi ilikuwa haijaingia duniani). Ndoa ya kwanza ilifungwa na Mungu mwenyewe, na ilifanyika katika usafi wote (Adamu na Eva walikuwa safi walipounganishwa na Mungu) na Mungu akawaagiza waendelee kudumu katika usafi na kuepuka kula atunda ya mti wa mema na mabaya.

Usafi (wa rohoni na mwilini) ni nguzo ya ndoa. Ikiwa wanandoa hawajasimama katika huo, hakuna uwezekano wa kufika mbali. Uchafu husababisha maradhi, harufu mbaya, na kudharauliwa. Heshima ya ndoa inategemea jinsi ambavyo wanandoa watadumu katika usafi. Uchafu wa rohoni hudhihirika kwenye matendo, maneno na mawazo; uchafu wa mwilini hudhihirika kwenye mwili, malazi, mavazi na kwenye mazingira (ndani ya nyumba na nje). Mtu anaweza kuwa na:
1.                  Midomo michafu.
Hii ni ile hali ya kutoa maneno machafu ambayo husababishwa na yale yalioyoko moyoni. Isaya aliuona uchafu huu alipomwambia Mungu mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nami ninakaa kati ya watu wenye midomo michafu” (Isaya 6:5). Bila shaka utaelewa kwamba midomo michafu hapa haimaanishi midomo ambayo haijasafishwa (hajapiga mswaki); maana yake ni kule kuwa na maneno machafu, kunena mabaya (uovu, masengenyeo, matusi na mengine). Ili ndoa isimame inahitaji maneno mazuri yenye kujenga, maneno ya kutia moyo, maneno matamu, maneno ya staha, maneno yaliyojaa neema ya Mungu. Ndoa nyingi zimeharibika kwa sababu ya midomo michafu.
Ukikuta mke ni mtukanaji, au ni msengenyaji au ni mgomvi asubuhi, mchana na jioni, ujue hakuna ndoa hapo. Hata kama ataishi na mume, yatakuwa maisha ya taabu sana. Mithali inasema “Ni afadhali kukaa katika nchi ya nyika; Kuliko na mwanamke mgomvi, mchokozi. (Mithali 21:19) Unaona, nchi ya nyika ni mahali pa shida (hapana maji, jua kali, hapana chakula) ila mateso yake hayafikii mateso ya kukaa ndani na mwanamke mgomvi na mchokozi. Je, mdomo wako unautumiaje? Kusudi la Mungu ni kwamba wanandoa watiane moyo, wajadili mambo yao kwa upendo, wapeane maneno yenye kujenga. Siyo kutukanana, kuitana majina ya wanyama, kugombana, na kuchokozana.
Mwanaume anayeutumia mdomo wake kama silaha ya kumpiga mke wake naye haijengi ndoa yake. Mwanaume ni mshauri wa familia, ni mwalimu, ni baba, ni kiongozi na ni mlinzi wa mke na watoto. Maneno ya ukali na matusi au ugomvi, hurarua mioyo ya watoto na mke. Ni muhimu mwanaume kujifunza Kwa Mungu, Baba. Yeye ni Mungu wa Upendo, hata wanawe tukikosea  huturidi (hutuadhibu) kwa upendo. Kila wakati anatuwazia yaliyo mema, hajawahi kuwaza kutuumiza au kutuangamiza. Hata tukimkosea atakasirika lakini tukishuka na kumwomba msamaha yeye hutusamehe.
Hivyo ni muhimu tukahakikisha midomo yetu ni misafi, yaani tunaongea maneno mema siku zote. Paulo anasema “Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea munyu, mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu.” (Wakolosai 4:6)   Mke akijua jinsi ya kumjibu mumewe na mume akajua jinsi ya kuongea na mkewe na wote wakaungana kuongea na Mungu maisha yatakuwa mazuri sana. Hata mwenzi wako akikosea, ongea naye kwa maneno ya kujenga. Maneno yana uwezo wa kubomoa kabisa mahusiano, kumbuka Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake. (Mithali 18:21). Maneno yanaweza kuua au kuhuisha ndoa yako, Mwombe Mungu akitakase kinywa chako kama ukiona kina shida.
2.                  Moyo uliojaa uchafu.
 Maandiko yanasema, “Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano” (Mathayo 15:19). Moyoni mwa mtu ndimo mlimo hisia, mawazo, na maamuzi, hivyo ili maisha ya mtu yawe salama ni lazima moyo uwe salama. Kwenye mithali tunasoma, “Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima. (Mithali 4:23. Moyo uliochafuka ni makao ya shetani, kila aina ya uharibifu utatoka ndani yake. Kama mwanadoa mmoja wapo ataacha moyo wake wazi na shetani akaujaza uchaffu wake (chuki, husuda, matukano, uzinzi, uasherati, uongo na mengine) ndoa haitaweza kusimama.
Upendo wa kweli huletwa na Roho Mtakatifu ndani ya mtu, hivyo kama moyo ni mchafu Roho Mtakatifu hawezi kukaa na upendo wa kweli hauna nafasi. Suluhisho ni kurudi msalabani na kumtwika Yesu mizigo ili kupata raha moyoni (nafsini) – Mathayo 11:28. Moyo wa mtu hujazwa kwa vile anavyovisikia, anavyovisoma na kuviona. 
Je, huwa unasoma nini? Huwa unasikiliza nini? Huwa unatazama nini kwenye runinga au ‘smartphone’ au kipakatilishi chako? Moyo wako ndio uliobeba ndoa yako, na ukilemewa na uchafu hakika utaiharibu ndoa. Dhambi ilipowalemea Adamu na Eva, walianza kulaumiana mbele za Mungu. Linda moyo wako, linda ndoa yako.
Dunia hufanya kazi katika mfumo hatari ambao hauwezi kutusaidia kudumu katika mahusiano. Kimsingi, dunia huhamasisha ubinfsi, chuki, kiburi na tamaa ambavyo ni hatari sana kwa ndoa. Yohana anasema, “Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia. (1Yohana 2:16). Mambo haya yaani “taama ya mwili, tama, na kiburi” kazi yake ni kuvuta uharibifu na kututenga na Mungu.
Uasherati ni uchafu mbaya, unaua roho na kuharibu mwili; ni lazima kujiepusha nao kama kijana unayempenda Mungu. Mabinti wanaojua thamani ya ubinti wao na vijana wanaojitambua hujilinda kabisa na uchafu huu. Ndoa nyingi zimevurugika kwa sababu ya uasherati ambao wanandoa waliufanya kabla ya ndoa. Wengine katika uasherati wao wakapata watoto ambao wamekuwa chanzo cha vurugu na chuki katika ndoa. Uchafu wa uasherati huchochea uzinzi katika ndoa, japo si mara zote. Ila mara nyingi watu ambao hawakuwa waaminifu kabla ya ndoa hushindwa kuwa waaminifu kwenye ndoa.
Usifanye tendo la ndoa kabla ya ndoa, na baada ya ndoa baki na mume wako kama Mungu alivyoamuru; ndoa yako haitatikisika.
Ni muhimu sana wanandoa wakadumisha usafi mioyo yao, na wasijichafue kabisa kwa uzinzi au picha za ngono. Kuaminiana huletwwa na usafi. Kila mmoja akikubali na kuamua kwa moyo wa dhati kumtii Mungu na kuwa wasafi na waaminifu kwa ndoa yake, maisha ya ndoa yatakuwa ya Baraka sana. Usafi ni msingi wa muhimu sana katika ndoa.
3.                 Mikono (michafu) iliyojaa damu. 
Unaitumiaje mikono yako? Wengine wameitumia kuwapiga wenzi wao. Wengine wameitumia kubeba vitu ambavyo ni hatarishi kwa wenzi wao. Je, mikono yako ni salama? Mungu ametupa mikono ili kwamba tuweze kujipatia kipato kwayo, tena tuitumie kuwasaidia wengine sio kuwaumiza. Mume au mke ambaye mikono yake ni myepesi kuleta madhara hawezi kuishi na ndoa yake kwa usalama. Mtume Yakobo akasema, “Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.” Hapa anazunggumza juu ya kuitakasa mikono na mioyo ili kuweza kuwa karibu na Mungu. Usafi huu ni wa muhimu sana.
4.                  Mwili na mavazi. 
Usafi wa mwili na mavazi una uzito sana kwenye mahusiano. Tuliyoyaona hapo juu ni mambo ya rohoni, hivyo matokeo yake huja taratibu na ni ya ndani. Swala la mwili na mavazi ni la wazi na halifichiki. Watu wengi wamevuruga mahusiano yao ya ndoa kwa sababu ya uchafu. Baadhi ya maeneo ya kutilia mkazo zaidi ni:
-          Nguo za ndani yani brazia, chupi, boksa, soksi, vesti n.k. hakuna kitu chenye kero kama harufu mbaya. Na kwenye ndoa ule ukaribu wa wanandoa huweza kuathirika sana kama kutakuwa na harufu mbaya inayotoka kwa mmoja wapo. Kukimbiana na kutokufurahiana huanzia hapo, mwisho michepuko hubisha hodi. Usafi wa mavazi ni kivutio kikubwa sana kwa mwenzi wako, usikubali kuwa mchafu bila sababu za msingi.
-          Mwili: Sehemu za siri, kinywa, kwapa nk; Haya nayo yamevuruga ndoa nyingi. Mume au mke ni mtu wa karibu sana na mara nyingi meneo haya kwake ni ya msingi, hasa kwenye eneo la tendo la ndoa. Hivyo yakiwa machafu yanamsababisha anapata haaki yake kwwa mateso badala ya furaha. Mwisho anaweza kupoteza kiu kabisa au akafanya kama wajibu tu bila kuonyeha furaha na kuridhika. Hii ni hatari kwa ndoa.
5.                  Mazingira ya ndani na nje.
Haya nayo yana umuhimu wake, kimsingi nyumba yenye mandhari masafi ni bustani yenye kuvutia kwa wanandoa. Usafi huleta unadhifu na hamasa kwa wanandoa wenyewe na wageni. Maeneo ya msingi ya kuangalia kwenye eneo la usafi wa ndani na nje ni:
-          Usafi wa nyumba na mpangilio wake. Nyumba ikisafishwa na kupangiliwa vizuri huwavutia sana wanaume, wanawake nao hufurahia kuona wanakaa na waume zao nyumbani ili kujenga ndoa. Usafi na mpangilio mzuri wa nyumba ndiyo siri ya mafanikio katika hili.
-          Chumba na malazi; Chumba cha wanandoa ni cha muhimu sana, yaani ni mahali ambapo wanashikiana katika tendo la ndoa. Hivyo ni mahali wanapafurahia kuliko pahali pengine pote. Ni bustani ya amani na furaha kwa wandoa.
Usafi wa chumbani ni wa msingi sana. Na hili linawahusu wanandoa wote japo mke ndiye msimamizi mkuu wa jukumu hili. Mashuka yafuliwe kwa wakati, chumba kisafishwe, neti ifuliwe, vitu vipangiliwe vizuri, pawepo na kapafyumu kazuri, yaani mambo yatakuwa mazuri sana. Mke usikubali mumeo atamani kukaa chini ya miti kwa sababu chumbani hapakaliki. Jitahidi kwa uwezo ulionao ufanye usafi.
-          Maandalizi ya chakula na vyombo: Chakula kilichoandaliwa katika mazingira safi na kutengwa kweye vyombo visafi, ni kivutio kikubwa. Hata hamu ya kula huja ghafla kwa ule usafi tu. Ndoa inaguswa na eneo hili pia, ili mume au mke ale na afurahie chakula usafi unahitajika.
-          Chooni na bafuni na Mazingira ya nje, nayo pia yanahitaji usafi ili kuifanya nyumba iwe ya kuvutia zaidi. Watoto hujifunza sana kwa wazazi, hivyo usafi ukitiliwa mkazo utawajengea watoto tabia njema na utajenga sifa njema kwa ndoa.
Kumbuka uchafu wa aina yoyote ile huleta dharau, hakuna mwanandoa yeyote anayependa kudharauliwa kwa sababu ya mwenzake. Mume hupenda kusifiwa kwa sababu ya mkw wake na mke vivyo hivyo. Kiujumla, usafi ni msingi wa muhimu sana kwa wanandoa. Ona mstari huu unavyosema Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.” Waebrania 13:4. Katika mafundisho ya Paulo kwa Timotheo, Paulo alikazia sana kuhusu usafi pia (1Timotheo 4:12), hivyo usafi ni lazima utiliwe mkazo kwa vijana, ili wakafanye vizuri kwenye ndoa zao pia.


Wednesday, 20 November 2019

DEAD BUT LEADING


What are you going to leave behind you, when you die?

After death most people disappear, living nothing behind them than troubles and  cries. One author said "It is passing on this earth like a Shadow" Some with unique accomplishments, use to leave behind them a tremendous impact to millions and millions of people in different generations. 


From Biblical context we can see people like Noah, Abraham, Joshua, David, Jacob, Daniel, Paul, Peter, and most important Jesus Christ.  Their impact has been in countless generations. Many who lived with these people are not even remembered. It is simply because they lived life for themselves. If you live a life for others, even after your death people will find you alive in their lives.

What is your life vision and mission? What are struggling to accomplish before you die? What are you going to be accountable before God on Judgement day? In all aspects of life, we have people leading us, though long dead. The people like Isaac Newton, Martin Luther (the protestant), Mother Teresa, Mahatma Gandi, Martin Luther King, Mwl. J. K. Nnyerere and many others. 

These people decided to live a life for others. Although they had different faiths, their genuine hearts and burning passion to help others meant success. Their ideas and lives have added something to humanity.


Monday, 30 July 2018

JIFUNZE KUNYENYEKEA

UNYENYEKEVU (HUMBLENESS/HUMILITY)

Dunia imejaa watu wanaotamani ukuu, utajiri na umaarufu; huzuni ni kwamba wengi hawajaelewa siri iliyopo kwenye kuinuliwa kwa mtu. Jitihada za kuonekana (kuwa maarufu), kuwa na fedha au mengine zimewakaa sana wanadamu. Na hii ni kawaida ya wanadamu, tumeumbwa lili tuishi kwa utukufu wa Mungu. Mafanikio yetu, hasa yanayotokana na Mungu yanaonesha utukufu wa Mungu.

Mambo ya msingi ya kujua:

A. Utajiri na heshima ya kweli hutokana na Mungu: Maandiko katika 1 Samweli 2:7 yanasema, "Bwana hufukarisha mtu, naye hutajirisha; Hushusha chini, tena huinua juu." Tena katika Mithali 8:18 tunasoma, "Utajiri na heshima ziko kwangu, Naam, utajiri udumuo, na haki pia."
Hivyo bila Mungu mtu akipata utajiri, hauwezi kuwa wa kudumu. Tena utajiri unaoambatana na heshima ni ule unaotoka kwa Mungu.
Kwenye Mithali 22:4 inatuweka sawa zaidi "Thawabu ya unyenyekevu ambao ni kumcha Bwana Ni utajiri, na heshima, nayo ni uzima." 

Kunyenyekea (Kumcha Mungu), kumeelezwa kuwa na matokeo makubwa matatu:
Utajiri: kumiliki au kuwa na mali nyingi
Heshima: kuwa na thamani kwa watu wanaokuzunguka
Uzima: kuwa na uhai au maisha.

Jumla ya mambo haya ni maisha bora (Maisha ya mafanikio). Mtu yeyote ambaye ni mnyenyekevu mbele za Mungu ana nafasi kubwa ya kuweza kufanikiwa katika Mungu.

Utajiri wa kweli hutokana na baraka za Mungu. Mithali 10:22 "Baraka ya Bwana hutajirisha, Wala hachanganyi huzuni nayo." Tukinyenyekea kwake atatuinua. 1 Petro 5:6 Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake;

B. Kufanya kazi kwa bidii na uaminifu ni sehemu ya unyenyekevu. Mtu aliyejaa kiburi, mbinafsi hawezi kufanya kazi kwa mafanikio. Mtu mwenye bidii katika kazi ana nafasi kuwa sana ya kufanikiwa (wakati mwingine hata kama hana uhusiano mzuri na Mungu). 

Shida ya kufanikiwa nje ya Mungu, ni maisha kuwa katika hatari. Haiwezekani kudumu katika utajiri, heshima na uzima bila kuwa na Mungu. Labda mtu aamue kuyauza maisha yake kwa shetani, napo shetani ni mwivi, aibaye na kuharibu na kuchinja (Yohana 10:10)

C. Kunyenyekea na kuwaheshimu wazazi kunaleta mafanikio na maisha marefu. Kumb. 5:16 Waheshimu baba yako na mama yako; kama Bwana, Mungu wako, alivyokuamuru, siku zako zipate kuzidi, nawe upate kufanikiwa katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako.

Watu wengi wamekwama kwa sababu ya kuonyesha kiburi kwa wazazi wao. Ni kweli unaweza kuwa umesoma kuliko wao, au una imani kuliko wao au umewazidi kiuchumi; bado ni haki yao kupata heshima kutoka kwako. Uwasikilize na utii katika yale yanayompendeza Mungu. Kushindana na wazazi hakuna baraka, ni laana.

D. Wazazi wa kiroho nao ni watu wa muhimu sana (Paulo anawaita wazee au watu waliotutangulia katika Imani). Mchungaji au mtu yeyote ambaye Mungu amemweka mbele yako akusaidie katika maisha yako ya kiroho, huwezi kuishi naye bila unyenyekevu. 

Yohana 13:14 "Basi ikiwa mimi, niliye Bwana na Mwalimu, nimewatawadha miguu, imewapasa vivyo kutawadhana miguu ninyi kwa ninyi." Hapa Yesu anatufundisha somo kubwa la kunyenyekeana sisi kwa sisi. Hii ndiyo njia ya kuwa wakuu kuliko wengine. Yesu anasema mkuu lazima awe mtumwa wa wengine. Marko 10:44 na mtu anayetaka kuwa wa kwanza wenu, atakuwa mtumwa wa wote.

E. Kunyenyekea kwa viongozi ni njia ya kumweshimu Mungu aliyewaweka katika hiyo mamlaka. Kama umeajiriwa au unaishi katika nchi au eneo fulani. Unyenyekevu ndiyo njia ya kupata kibali kwa wakuu. Ajikwezaye hushushwa. Uwe mnyenyekevu huku ukitimiza majukumu yako kwa moyo. Ukiona watu wananyenyekea kwa raisi usiwashangae, wameng'amua siri ya kufanikiwa. Kunyenyekea si kujipendekeza. Ni kumpa heshima anayestahili heshima.

Mwisho Petro anasema"Waheshimuni watu wote. Wapendeni ndugu. Mcheni Mungu. Mpeni heshima mfalme."1 Petro 2:17 

JE, UNATAKA KUFANIKIWA KATIKA MUNGU? JIFUNZE KUNYENYEKEA. UTAFANIKIWA.

Na. Mwl. S.S.Michael
Simu: 0713511544 (Whatsapp)

Sunday, 8 July 2018

SOTE TUPIGE KELELE


 "ZIMWI HILI HALIJAFA"


Ama kweli rushwa zimwi, tena zimwi kwelikweli
Lazidi hata ukimwi, upungufu kinga za mwili
Kama moto halizimwi, kila kona watu chali
Zimwi linatutafuna, sote tupige kelele

Halichomwi Kwa mkuki , kwa risasi halitoki
Chunguni halipikiki, ni gumu halikatiki
Adui wa kila haki, kuchafua halichoki
Zimwi linatutafuna, sote tupige kelele

Tena halijabagua, kwa yeyote linapita
Rangi yake yavutia, kila mtu kumvuta
Mjini kijiji pia, kotekote talipata
Zimwi linatutafuna, sote tupige kelele

Wengi walio kitini, wamekwisha kuvamiwa
Ni wema sana machoni, moyoni ni kama chawa
Aingiapo mwilini, hataki kuondolewa
Zimwi linatutafuna, sote tupige kelele

Nyangumi pia dagaa, wote limewafikia
Mashilingi wayazoa, nyumba zao kujengea
Hoja wanazozitoa, uongo tamu kolea
Zimwi linatutafuna, sote tupige kelele

Wako kama hayawani, hawataki makatazo
Kila kitu mfukoni, wanazidisha ujazo
Utu kwao ndio nini, Rushwa kwao ndiyo chanzo
Zimwi linatutafuna, sote tupige kelele

Wangine kiomboleza, wao kwao ni tulizo
Hukumu kuigeuza, hilo kwao si tatizo
Haki nazo kuziuza, kila kona ni uozo
Zimwi linatutafuna, sote tupige kelele

Yatima hata wajane, wamekuwa kama ngazi
Wanapopanda  wengine, kukanyagwa ndiyo kazi
Wakisema wayanene, mwisho wake ni machozi
Zimwi linatutafuna, sote tupige kelele

Huko nako barabara, nao wamo mtegoni
Wamebaki na mkwara, nacho kidogo pembeni
Japo wana mshahara, wataka na mkononi
Zimwi linatutafuna, sote tupige kelele

Kanisani ‘sikitini, zimwi linajipenyeza
Tuulize kulikoni, nako tume kuchunguza
Hawa watu wa Imani, Mola hajawatuliza?
Zimwi linatutafuna, sote tupige kelele

Masikini hatiani, matatani kibindoni
Makosani hukumuni, mtieni gerezani
Nguvuni afanye nini, mhaini wa kitini?
Zimwi linatutafuna, sote tupige kelele

Hili zimwi tangu kale, halina wa kulitaka
Sio hawa wala wale, kauli ni toka toka
Kwa hatua na kelele, zimwi hili tatimka
Zimwi linatutafuna, sote tupige kelele

Zimwi hili ni laana, lachafua nchi yote
Tena halina maana, adui wa watu wote
Linaleta kuumana, na vilio kotekote
Zimwi linatutafuna, sote tupige kelele

Hongera kwa wateule, wapigao makelele
Maisha yasiwe yale, ya hadithi tangu kale
Uzalendo utawale, tamaa tutupe kule
Zimwi linatutafuna, sote tupige kelele

Tusitazame usoni, tukitaka ua nyani
Wahuni na waumini, vitini uraiani
Bungeni nako chamani, mkoani wilayani
Zimwi linatutafuna, sote tupige kelele

Majumbani mashuleni, televisheni redioni
Barabani mtaani, mjini na vijijini
Jijini mtandaoni, Gazetini  vitabuni
Zimwi linatutafuna, sote tupige kelele

Mahakamani barazani, Jeshini sipitalini
Ofisini mashambani, makampuni sokoni
Mashuleni na vyuoni, kusini kaskazini
Zimwi linatutafuna, sote tupige kelele

Hata nako vitabuni, zimwi hili ni chukizo
Chukizo kwa Maanani, kwalo hataki mchezo
Hasa wale wa enzini, wasiotaka katazo
Zimwi linatutafuna, sote tupige kelele

Chonde chonde wanakwetu, tusimmunye maneno
Sote tubebe mtutu, tuanzishe fungamano
Nchi yetu haki zetu, tusongeshe mpambano
Zimwi linatutafuna, sote tupige kelele

A Strong Marriage vs. A Good Family: Understanding God's Order

In many Christian homes, there is a deep desire to build a good family. Parents work hard to provide for their children, maintain a peaceful...

Powered By Blogger