1. Alikubali kuuacha utukufu mbinguni na kuja kufa kwaajili ya dhambi zetu wanadamu, akatupatanisha na Mungu.
Wafilipi 2:7 "bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.
Isaya 53:3-5 Alidharauliwa na kukataliwa na watu;.....Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu.....Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.
Warumi 5:6-10...Kwa maana hapo tulipokuwa hatuna nguvu, wakati ulipotimia, Kristo alikufa kwa ajili ya waovu. Kwa kuwa ni shida mtu kufa kwa ajili ya mtu mwenye haki; lakini yawezekana mtu kuthubutu kufa kwa ajili ya mtu aliye mwema.
Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi. Basi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye.
Kwa maana ikiwa tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana wake; zaidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika uzima wake. Wala si hivyo tu, ila pia twajifurahisha katika Mungu kwa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa yeye sasa tumeupokea huo upatanisho.
Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi; maana kabla ya sheria dhambi ilikuwamo ulimwenguni, lakini dhambi haihesabiwi isipokuwapo sheria; walakini mauti ilitawala tangu Adamu mpaka Musa, nayo iliwatawala hata wao wasiofanya dhambi ifananayo na kosa la Adamu, aliye mfano wake yeye atakayekuja.
Lakini karama ile haikuwa kama lile kosa; kwa maana ikiwa kwa kukosa kwake yule mmoja wengi walikufa, zaidi sana neema ya Mungu, na kipawa kilicho katika neema yake mwanadamu mmoja Yesu Kristo kimezidi kwa ajili ya wale wengi.
Warumi 8:36 Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa.
2. Ana upendo wa kweli kwa wote Hana ubaguzi, Yeye anawaita wote waende kwake wapate uzima-kwake hakuna tajiri wala maskini, wa - Ulaya au wa-Afrika, Myahudi au Myunani..Yeye kwake wote wana nafasi.
Mathayo 11:28 Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
Ufunuo wa Yohana 5:9 Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa"
Yohana 6:37 Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe.
Yohana 3:16-17 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye
3. Jina lake linapita majina yote mbinguni, duniani na kuzimu
Wafilipi 2:9 Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina, ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi(kuzimu); na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.
4. Kwa jina lake mambo makuu hufanyika, tunapokea majibu ya maombi yetu na tunapata uzima au wokovu.
Yohana 16:24 Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu
Marko 16:17 Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya, watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.
Luka 10:17 Ndipo wale sabini waliporudi kwa furaha, wakisema, Bwana, hata pepo wanatutii kwa jina lako.
Matendo ya Mitume 4:10 jueni ninyi nyote na watu wote wa Israeli ya kuwa kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, ambaye ninyi mlimsulibisha, na Mungu akamfufua katika wafu, kwa jina hilo mtu huyu anasimama ali mzima mbele yenu.
Matendo ya Mitume 16:18 Akafanya hayo siku nyingi. Lakini Paulo akasikitika, akageuka akamwambia yule pepo, Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu. Akamtoka saa ile ile.
Matendo ya Mitume 4:30 ukinyosha mkono wako kuponya; ishara na maajabu vifanyike kwa jina la Mtumishi wako mtakatifu Yesu.Yohana 20:31 Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake.
Matendo ya Mitume 2:21 Na itakuwa kila atakayeliitia jina la Bwana ataokolewa. (Warumi 10:13)
5. Kuzaliwa kwake hakukuwa kwa kawaida
- Kulitabiriwa: Atazaliwa na bikira (Isaya 7:14), Atakuwa mtoto mwanaume na atakuwa na uweza wa kifalme (Isaya 9:6)
- Alizaliwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu (Hakuwa na baba wa kimwili) - Mathayo 1:20 Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.
- Jina lake lilitolewa na malaika kabla ya kuzaliwa kwake. Mathayo 1:21 Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.
- Kuzaliwa kwake kulitikisa Uyahudi nzima. Mamajusi wa Mashariki - Mathayo 2:1 Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, mamajusi wa mashariki walifika Yerusalemu, Wachungaji wa kondeni - Luka 2:8 Na katika nchi ile ile walikuwako wachungaji wakikaa makondeni na kulinda kundi lao kwa zamu usiku. Pamoja na ufalme mzima wa Mfalme Herode - (Luka 2:12-13)
- Alizaliwa katika mazingira duni sana. Luka 2:7 akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng'ombe, kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.
6. Alifanya mambo ambayo hayakuwahi kufanyika kabla yake tangu kuumbwa kwa ulimwengu.
- Alifufua wafu waliokufa siku nyingi - Lazaro (Siku nne kaburini) na wengine wengi.
- Alitangaza msamaha wa dhambi - Marko 2:5 Naye Yesu, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu, umesamehewa dhambi zako.
- Alikemea pepo zikamtii (Luka 8:29)
- Alitembea juu ya maji (Marko 6:48)
- Aliwalisha watu Elfu tano kwa samaki wawili na mikate mitano (Mathayo 14:17...)
- Aliwaponya wagonjwa wenye magonjwa yaliyoshindikana. Luka 4:40 Na jua lilipokuwa likichwa, wote waliokuwa na wagonjwa wenye maradhi mbali mbali waliwaleta kwake, akaweka mikono yake juu ya kila mmoja akawaponya.
- Alifundisha kwa mamlaka na kwa utofauti mkubwa. Luka 4:32 wakashangaa mno kwa mafundisho yake, kwa kuwa neno lake lilikuwa na uwezo.
- Aliukemea upepo ukatii na kuiamuru Bahari ikatulia . Marko 4:39 Akaamka, akaukemea upepo, akaiambia bahari, Nyamaza, utulie. Upepo ukakoma, kukawa shwari kuu.
- Kwa neno lake samaki walijaa baharini. Luka 5:6 Basi, walipofanya hivyo (Yesu alivyowaagiza) walipata samaki wengi mno, nyavu zao zikaanza kukatika.
7. Alikisema juu mateso, kifo chake na kufufuka kwake, na ikatokea kama alivyosema.
- Alisema atapata mateso mengi, atasulubiwa na siku ya tatu atafufuka katika wafu. Luka 24:7 akisema, Imempasa Mwana wa Adamu kutiwa mikononi mwa wenye dhambi, na kusulibiwa, na kufufuka siku ya tatu. Mathayo 16:21 Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemu, na kupata mateso mengi kwa wazee na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka.
- Malaika anashuhudia kufufuka kwake. Mathayo 28:6 Hayupo hapa; kwani amefufuka kama alivyosema. Njoni, mpatazame mahali alipolazwa.
- 1 Wakorintho 15:4 na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko.
8. Kufa kwake kuliambatana na matukio yasiyo ya kawaida.Luka 23:44 Hapo ilikuwa yapata saa sita, kukawa giza juu ya nchi yote hata saa kenda, jua limepungua nuru yake; pazia la hekalu likapasuka katikati.
- Dunia ilitiwa giza
- Kulikuwa na tetemeko kubwa
- Pazia la hekalu likapasuka
- Makaburi yakapasuka na wafu waliokuwa ndani yake wakaibuka.
9. Kufufuka kwake kulikuwa dhahiri - alijionyesha kwa watu mbalimbali. Matendo ya Mitume 1:2-3 hata siku ile alipochukuliwa juu, alipokuwa amekwisha kuwaagiza kwa Roho Mtakatifu wale mitume aliowachagua; wale aliowadhihirishia nafsi yake, kwa dalili nyingi, baada ya kuteswa kwake, ya kwamba yu hai, akiwatokea muda wa siku arobaini, na kuyanena mambo yaliyouhusu ufalme wa Mungu.
1 Wakorintho 15:6 baadaye aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano pamoja; katika hao wengi wanaishi hata sasa, ila baadhi yao wamelala.
10. Alipaa mbinguni na akashuhudiwa na malaika kwamba atarudi tena (kama alivyoahidi mwenyewe - Yohana 14:1,6)
Matendo ya Mitume 1:9 - 11 Akiisha kusema hayo, walipokuwa wakitazama, akainuliwa, wingu likampokea kutoka machoni pao. Walipokuwa wakikaza macho mbinguni, yeye alipokuwa akienda zake, tazama, watu wawili wakasimama karibu nao, wenye nguo nyeupe, wakasema, Enyi watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni.
Marko 16:19 Basi Bwana Yesu, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu.
Luka 24:51 Ikawa katika kuwabariki, alijitenga nao; akachukuliwa juu mbinguni.
1 Timotheo 3:16 Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu.
Zaidi ya yote Yeye ni Mungu asiyeshindwa, mwaminifu katika ahadi zake; wote waliomwamini wana ushuhuda kuhusu uzuri wake. Ziko shuhuda nyingi za matendo makuu yaliyotendeke ulimwenguni mwote kwa zaidi ya miaka 2000 sasa, na bado mambo yanazidi kutendeka kwa jina la Yesu. Manabii na mitume wengine (Wajumbe wa Mungu) wote waliotajwa katika Biblia wakitatwa majina yao hakuna linaloweza kutendeka.
Katika Matendo ya Mitume 4:9-12 tunasoma,
Ndipo Petro, akijaa Roho Mtakatifu, akawaambia, .... jueni ninyi nyote na watu wote wa Israeli ya kuwa kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, ambaye ninyi mlimsulibisha, na Mungu akamfufua katika wafu, kwa jina hilo mtu huyu (aliyekuwa kiwete tangu tumboni) anasimama ali mzima mbele yenu. Yeye ndiye jiwe lile lililodharauliwa na ninyi waashi, nalo limewekwa kuwa jiwe kuu la pembeni. Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.
Leo hii katika makanisa ya kweli, na kwenye mikutano na semina ya waabuduo halisi tunashuhudia mambo makuu sana yakiendelea kutendeka; viwete wanatembea, vipofu wanaona, wagonjwa wanapona, watu wengi wanafunguliwa kutoka katika vifungo vya nguvu za giza na watu wengi wanapokea uweza wa kufanyika watoto wa Mungu na kuachana na dhambi.
"JAMANI--- "NI NANI KAMA YESU??????????????????"
No comments:
Post a Comment