Neno Dhambi linadhihirika katika maandiko kama mjumuiko wa uovu, mabaya, hatia, makosa, ukengeufu na
uasi. Vifungu vifuatavyo
katika biblia vinatupa upana wa tafsiri hii:
Zaburi 51:1-9
“Ee Mungu,
unirehemu, Sawasawa na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, Uyafute makosa (Transigressionon)yangu. Unioshe
kabisa na uovu (iniquity) wangu,
Unitakase dhambi (Sin) zangu. Maana
nimejua mimi makosa yangu Na dhambi yangu i mbele yangu daima.
Nimekutenda dhambi Wewe peke yako,
Na kufanya maovu mbele za macho
yako. Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo, Na kuwa safi utoapo hukumu.
Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu; Mama yangu alinichukua mimba hatiani. Tazama, wapendezwa na kweli
iliyo moyoni; Nawe utanijulisha hekima kwa siri, Unisafishe kwa hisopo nami
nitakuwa safi, Unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji. Unifanye kusikia furaha na shangwe, Mifupa
uliyoiponda ifurahi. Usitiri uso wako usitazame dhambi zangu; Uzifute hatia
zangu zote.”
Maneno ya
asili (Ya Kiebrania)yaliyotumika kwenye maneno haya ni
Þ Kwa neno Makosa (transigression) ni neno ‘peša’ likimaanisha ‘rebelliousness’
kufanya kinyume na utaratibu au uasi.
Þ Kwa neno Uovu (Iniquity) limetumika neno ‘hātā’ linalomaanisha ‘moral
misshapennes’ yaani kinyume na maadili ya ki-Mungu kwa makusudi. Neno hili
limetumika mara 580 katika Agano la kale.
Þ
Neno sin limetokana
na neno ‘āwōn’ linalomaanisha
‘shorticomings’Kupungukiwa na utukufu wa Mungu.
Katika Agano jipya yametumika maneno ya Kiyunani mawili:
Neno ‘adikia’ linalomaanisha kufanya makosa (wrongdoing), kinyume na haki
(Unrighteousness), na kinyume na sheria (Injustice). Katika kundi hili, dhambi
inaonekana kuwa kitendo cha hiari anachokifanya mtu, kinachoweza kuleta madhara
au uharibifu kwa mtu mwingine.
Neno jingine ni ‘hamartia’ ambalo limetafsiriwa mara
nyingi kama Dhambi (Sin). Kundi hili la dhambi linajumuisha maneno yote ya
Kiebrania yaliyotumika katika Agano la kale (yaani ‘āwōn’, ‘hātā’ na ‘peša’).
Dhambi (Sin) katika agano Jipya inamaanisha kukosa maadili ya
ki-Mungu (Makosa), maovu na uasi mbele za Mungu.
1 Yoh. 3:4 Kila atendaye dhambi, afanya
uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi (rebellion). Kuasi ni kukiuka kwa makusudi
taratibu au sheria zilizowekwa na mamlaka Fulani, ni kwenda kinyume na maagano
au mapatano. Hili tunaliona kwenye kitabu cha mwanzo pale ambapo Adamu na Eva
waliamua, japo kwa kudanganywa na shetani, kula tunda la mti ambao Mungu
aliwakataza. (Mwanzo 3)
1 Yoh. 5:17 Kila lisilo la haki ni dhambi, na
dhambi iko isiyo ya mauti.
Warumi 14:23 “… Na kila tendo lisilotoka katika imani ni
dhambi.”
Mithali 24:9 Fikira za mpumbavu ni dhambi, Na
mwenye mzaha huwachukiza watu.
Mithali 21:4 Macho yenye kiburi, na moyo wa kutakabari,
Hata ukulima wa waovu, ni dhambi.
Ayubu 23:11 Mguu wangu umeshikamana sana na hatua zake; Njia
yake nimeishika, wala sikukengeuka.
Kumb.11:28 na laana ni hapo msiposikiza
maagizo ya Bwana, Mungu wenu, mkikengeuka katika njia niwaagizayo
leo, kwa kuandama miungu mingine msiyoijua.
Dhambi imetafsiriwa tena kama “Matendo
ya mwili”
Wagalatia 5:19 inasema, “Basi matendo ya
mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu,
uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi,
ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema,
kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo
hawataurithi ufalme wa Mungu.
Tena,
Dhambi
ni Ibada ya sanamu. Wakolosai 3:5 “Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo
katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo
ibada ya sanamu; kwa ajili ya mambo hayo huja ghadhabu ya Mungu.”
Kuna tofauti kati ya dhambi kwenye Agano
la kale na dhambi wakati huu wa Agano la Jipya.
Dhambi katika Agano la kale ilikuwa ni
kule kuvunja sheria (Torati ya Musa), na kwenda kinyume na taratibu za dini ya
Kiyahudi. Amri kumi za Mungu ndizo zilikuwa kielelezo cha Amri zote. Katika
Warumi 4:15 mtume Paulo anatuambia “Kwa sababu sheria ndiyo ifanyayo hasira; maana
pasipokuwapo sheria, hapana kosa.” Kwa hiyo kumbe watu walianza
kuhesabiwa makosa pale sheria ilipowekwa.
Katika Agano la kale sheria na hukumu
zake zilikuwa mikononi mwa waalimu wa Dini na Mafarisayo. Na walikuwa na uwezo
wa kumhuku mtu yeyote kulingana na sheria hizo. Kwenye Waebrania 10:28 tunasoma
“Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi
wawili au watatu.” Kwa hiyo watu wengi walikufa – utaratibu ulikuwa jino kwa
jino, atakayeua kwa upanga atauwawa kwa upanga.
Warumi 8:3 Maana yale yasiyowezekana kwa sheria,
kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe
mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi,
aliihukumu dhambi katika mwili
Wakolosai 2:23 Mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana hekima,
katika namna ya ibada mliyojitungia wenyewe, na katika kunyenyekea, na katika
kuutawala mwili kwa ukali; lakini hayafai kitu kwa kuzizuia tamaa za mwili.
Paulo akizizungumzia taratibu za ibada ya
Kiyahudi katika Wakolosai 2:23 akasema, “Mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana
hekima, katika namna ya ibada mliyojitungia wenyewe, na katika kunyenyekea, na
katika kuutawala mwili kwa ukali; lakini hayafai kitu kwa kuzizuia tamaa za
mwili.
Katika agano jipya
dhambi ina upana zaidi.
Yale yaliyokuwa magumu kwa sababu ya
sheria sasa katika Kristo Mungu anayafanya mepesi. Warumi 8:3 inasema “Maana
yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili,
Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na
kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili”
Yesu alitangaza mfumo mpya wa maisha ya
Kiroho.
Mathayo
5:23-48 “Basi
ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno
juu yako, iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na
ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako………. Mmesikia
kwamba imenenwa, Usizini; lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye
mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake……..Imenenwa pia, Mtu
akimwacha mkewe, na ampe hati ya talaka; lakini mimi nawaambia, Kila mtu
amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu
akimwoa yule aliyeachwa, azini.Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape
uongo, ila mtimizie Bwana nyapo zako lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa;
hata kwa mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu; wala kwa nchi, kwa
maana ndiyo pa kuwekea miguu yake; wala kwa Yerusalemu, kwa maana ndio mji wa
Mfalme mkuu.
Wala
usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya unywele mmoja kuwa mweupe au
mweusi. Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo
yatoka kwa yule mwovu. Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino
kwa jino; Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu
akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili. Na mtu atakaye kukushitaki na
kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia. Na mtu atakayekulazimisha mwendo wa
maili moja, nenda naye mbili. Akuombaye, mpe; naye atakaye kukopa kwako, usimpe
kisogo. Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui
yako; lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi, ili
mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake
waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.
Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata
thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo? Tena mkiwaamkia
ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao
hawafanyi kama hayo? Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni
alivyo mkamilifu.
Maeneo yaliyopigiwa mstari
yanaonyesha hali ilivyokuwa kipindi cha sheria, lakini tunaona Yesu akitangaza
mambo mapya na kusema, “lakini mimi ninasema” Kwa hiyo sasa
tunasimama katika yale aliyoyasema Yesu yaani; Kuacha na kukaa mbali kabisa na zinaa,
kutokuachana, kutokuapa, kuwapenda maadui na kuwaombea.
Tena katika Mathayo 22:37-39 Yesu akatangaza amri
kuu mbili, “Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho
yako yote, na kwa akili zako zote. Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza.
Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako.”
Katika sheria ni hapakuwa na kumpenda jirani
kama nafsi, wa kukaa naye ni Yule tu ambaye alikuwa amekubalika kutokana na Torati.
Kwa sababu hiyo Wayahudi walilazimika kujitenga na wanadamu wengine wote
waliokuwa wanaabudu sanamu. Hapakuwa na kuchangamana.
Yesu alipokuja sasa tunaambiwa:
Waefeso 2:14 Kwa maana yeye (Yesu) ndiye
amani yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja; akakibomoa kiambaza
cha kati kilichotutenga.
2 Wakorintho 5:17 Hata imekuwa, mtu akiwa
ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.
Wagalatia 2:16 hali tukijua ya kuwa
mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria, bali kwa imani ya Kristo Yesu;
sisi tulimwamini Kristo Yesu ili tuhesabiwe haki kwa imani ya Kristo, wala
si kwa matendo ya sheria; maana kwa matendo ya sheria hakuna mwenye mwili
atakayehesabiwa haki.
Warumi 8:1 Sasa, basi, hakuna
hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.
Warumi 6: 17-23 “Lakini Mungu na
ashukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mliitii kwa mioyo yenu
ile namna ya elimu ambayo mliwekwa chini yake; na mlipokwisha kuwekwa huru
mbali na dhambi, mkawa watumwa wa haki. ….
Kwa kuwa kama mlivyovitoa viungo vyenu
vitumiwe na uchafu na uasi mpate kuasi, vivyo hivyo sasa vitoeni viungo vyenu
vitumiwe na haki mpate kutakaswa. Kwa maana mlipokuwa watumwa wa dhambi,
mlikuwa huru mbali na haki. Ni faida gani basi mliyopata siku zile kwa mambo
hayo mnayoyatahayarikia sasa?
Kwa maana mwisho wa mambo hayo ni mauti. Lakini sasa mkiisha
kuwekwa huru, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu, mnayo
faida yenu, ndiyo kutakaswa, na mwisho wake ni uzima wa milele. Kwa maana
mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele
katika Kristo Yesu Bwana wetu.”