Saturday, 7 September 2013

SIRI YA MAISHA

Si jambo rahisi kupata tafsiri ya maisha, japo wengi hufikiri kwamba wanajua sana maisha hasa kwa sababu ya kuwa na Umri mkubwa au kuwa na vitu fulani ambavyo wengine hawana. Je, maisha ni nini? Vijana wengi huondoka vijijini na kwenda mijini wakisema wanakwenda "kutafuta maisha..............." Je maisha hutafutwa?
Maswali haya ndiyo natamani yatujengee mwelekeo mmoja wa kuyaendea maandiko ili tuone ni nini Mungu anasema kuhusu maisha.
Kumb. 4:9 "Lakini, jihadhari nafsi yako, ukailinde roho yako kwa bidii, usije ukayasahau mambo yale uliyoyaona kwa macho yako, yakaondoka moyoni mwako siku zote za maisha yako; bali uwajulishe watoto wako na watoto wa watoto wako"
Zab 9:11 Maana, kwa msaada wangu siku zako zitazidishwa; Na miaka ya maisha yako itaongezwa
Luka 12:23 Kwa kuwa maisha ni zaidi ya chakula, na mwili ni zaidi ya mavazi.
Luka 21:34 Basi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafula, kama mtego unasavyo;
 Mdo 15:26 watu waliohatirisha maisha yao kwa ajili ya jina la Bwana wetu Yesu Kristo.
 Mdo 20:24 Lakini siyahesabu maisha yangu kuwa kitu cha thamani kwangu kama kuumaliza mwendo wangu na huduma ile niliyopokea kwa Bwana Yesu, kuishuhudia Habari Njema ya neema ya Mungu.
1 kor 6:4 Basi, mkiwa na mahali panapohukumiwa mambo ya maisha haya, mwawaweka kuwa waamuzi hao waliohesabiwa kuwa si kitu; katika kanisa?
1 kor 15:19 Kama katika maisha haya tu tumemtumaini Kristo, sisi tu maskini kuliko watu wote.
Filip 1:20 "..................ikiwa kwa maisha yangu, au ikiwa kwa mauti yangu."
1 Pet 4:3 Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali;

NANI KAMA YESU?

1. Alikubali kuuacha utukufu mbinguni na kuja kufa kwaajili ya dhambi zetu wanadamu, akatupatanisha na Mungu.

Wafilipi 2:7 "bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.

Isaya 53:3-5 Alidharauliwa na kukataliwa na watu;.....Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu.....Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.

Warumi 5:6-10...Kwa maana hapo tulipokuwa hatuna nguvu, wakati ulipotimia, Kristo alikufa kwa ajili ya waovu. Kwa kuwa ni shida mtu kufa kwa ajili ya mtu mwenye haki; lakini yawezekana mtu kuthubutu kufa kwa ajili ya mtu aliye mwema.

 Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi. Basi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye. 

Kwa maana ikiwa tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana wake; zaidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika uzima wake. Wala si hivyo tu, ila pia twajifurahisha katika Mungu kwa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa yeye sasa tumeupokea huo upatanisho.

Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi; maana kabla ya sheria dhambi ilikuwamo ulimwenguni, lakini dhambi haihesabiwi isipokuwapo sheria; walakini mauti ilitawala tangu Adamu mpaka Musa, nayo iliwatawala hata wao wasiofanya dhambi ifananayo na kosa la Adamu, aliye mfano wake yeye atakayekuja.  

Lakini karama ile haikuwa kama lile kosa; kwa maana ikiwa kwa kukosa kwake yule mmoja wengi walikufa, zaidi sana neema ya Mungu, na kipawa kilicho katika neema yake mwanadamu mmoja Yesu Kristo kimezidi kwa ajili ya wale wengi. 


Warumi 8:36 Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa.

2. Ana upendo wa kweli kwa wote Hana ubaguzi, Yeye anawaita wote waende kwake wapate uzima-kwake hakuna tajiri wala maskini, wa - Ulaya au wa-Afrika, Myahudi au Myunani..Yeye kwake wote wana nafasi.

Mathayo 11:28 Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

Ufunuo wa Yohana 5:9 Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa"

Yohana 6:37 Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe.

Yohana 3:16-17 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye

3. Jina lake linapita majina yote mbinguni, duniani na kuzimu

Wafilipi 2:9 Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina, ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi(kuzimu); na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.

4. Kwa jina lake mambo makuu hufanyika, tunapokea majibu ya maombi yetu na tunapata uzima au wokovu.

Yohana 16:24 Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu


Marko 16:17 Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya, watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.


Luka 10:17 Ndipo wale sabini waliporudi kwa furaha, wakisema, Bwana, hata pepo wanatutii kwa jina lako.



Matendo ya Mitume 4:10 jueni ninyi nyote na watu wote wa Israeli ya kuwa kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, ambaye ninyi mlimsulibisha, na Mungu akamfufua katika wafu, kwa jina hilo mtu huyu anasimama ali mzima mbele yenu.



Matendo ya Mitume 16:18 Akafanya hayo siku nyingi. Lakini Paulo akasikitika, akageuka akamwambia yule pepo, Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu. Akamtoka saa ile ile.

Matendo ya Mitume 4:30 ukinyosha mkono wako kuponya; ishara na maajabu vifanyike kwa jina la Mtumishi wako mtakatifu Yesu.Yohana 20:31 Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake.

Matendo ya Mitume 2:21 Na itakuwa kila atakayeliitia jina la Bwana ataokolewa. (Warumi 10:13)

5. Kuzaliwa kwake hakukuwa kwa kawaida


  • Kulitabiriwa: Atazaliwa na bikira (Isaya 7:14), Atakuwa mtoto mwanaume na atakuwa na uweza wa kifalme (Isaya 9:6)
  • Alizaliwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu (Hakuwa na baba wa kimwili) - Mathayo 1:20 Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.
  • Jina lake lilitolewa na malaika kabla ya kuzaliwa kwake. Mathayo 1:21 Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.
  • Kuzaliwa kwake kulitikisa Uyahudi nzima. Mamajusi wa Mashariki -  Mathayo 2:1 Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, mamajusi wa mashariki walifika Yerusalemu, Wachungaji wa kondeni - Luka 2:8 Na katika nchi ile ile walikuwako wachungaji wakikaa makondeni na kulinda kundi lao kwa zamu usiku. Pamoja na ufalme mzima wa Mfalme Herode - (Luka 2:12-13)
  • Alizaliwa katika mazingira duni sana. Luka 2:7 akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng'ombe, kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.
6. Alifanya mambo ambayo hayakuwahi kufanyika kabla yake tangu kuumbwa kwa ulimwengu.
  • Alifufua wafu waliokufa siku nyingi - Lazaro (Siku nne kaburini) na wengine wengi.
  • Alitangaza msamaha wa dhambi - Marko 2:5 Naye Yesu, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu, umesamehewa dhambi zako.
  • Alikemea pepo zikamtii (Luka 8:29)
  • Alitembea juu ya maji (Marko 6:48)
  • Aliwalisha watu Elfu tano kwa samaki wawili na mikate mitano (Mathayo 14:17...)
  • Aliwaponya wagonjwa wenye magonjwa yaliyoshindikana. Luka 4:40 Na jua lilipokuwa likichwa, wote waliokuwa na wagonjwa wenye maradhi mbali mbali waliwaleta kwake, akaweka mikono yake juu ya kila mmoja akawaponya.
  • Alifundisha kwa mamlaka na kwa utofauti mkubwa. Luka 4:32 wakashangaa mno kwa mafundisho yake, kwa kuwa neno lake lilikuwa na uwezo.
  • Aliukemea upepo ukatii na kuiamuru Bahari ikatulia . Marko 4:39 Akaamka, akaukemea upepo, akaiambia bahari, Nyamaza, utulie. Upepo ukakoma, kukawa shwari kuu.
  • Kwa neno lake samaki walijaa baharini. Luka 5:6 Basi, walipofanya hivyo (Yesu alivyowaagiza) walipata samaki wengi mno, nyavu zao zikaanza kukatika.
7. Alikisema juu mateso, kifo chake na kufufuka kwake, na ikatokea kama alivyosema.
  • Alisema atapata mateso mengi, atasulubiwa na siku ya tatu atafufuka katika wafu. Luka 24:7 akisema, Imempasa Mwana wa Adamu kutiwa mikononi mwa wenye dhambi, na kusulibiwa, na kufufuka siku ya tatu. Mathayo 16:21 Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemu, na kupata mateso mengi kwa wazee na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka.
  • Malaika anashuhudia kufufuka kwake. Mathayo 28:6 Hayupo hapa; kwani amefufuka kama alivyosema. Njoni, mpatazame mahali alipolazwa.
  • 1 Wakorintho 15:4 na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko.
8. Kufa kwake kuliambatana na matukio yasiyo ya kawaida.Luka 23:44 Hapo ilikuwa yapata saa sita, kukawa giza juu ya nchi yote hata saa kenda, jua limepungua nuru yake; pazia la hekalu likapasuka katikati.
  • Dunia ilitiwa giza
  • Kulikuwa na tetemeko kubwa
  • Pazia la hekalu likapasuka
  • Makaburi yakapasuka na wafu waliokuwa ndani yake wakaibuka.
9. Kufufuka kwake kulikuwa dhahiri - alijionyesha kwa watu mbalimbali.  Matendo ya Mitume 1:2-3 hata siku ile alipochukuliwa juu, alipokuwa amekwisha kuwaagiza kwa Roho Mtakatifu wale mitume aliowachagua; wale aliowadhihirishia nafsi yake, kwa dalili nyingi, baada ya kuteswa kwake, ya kwamba yu hai, akiwatokea muda wa siku arobaini, na kuyanena mambo yaliyouhusu ufalme wa Mungu.
1 Wakorintho 15:6 baadaye aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano pamoja; katika hao wengi wanaishi hata sasa, ila baadhi yao wamelala.
10. Alipaa mbinguni na akashuhudiwa  na malaika kwamba atarudi tena (kama alivyoahidi mwenyewe - Yohana 14:1,6)
Matendo ya Mitume 1:9 - 11 Akiisha kusema hayo, walipokuwa wakitazama, akainuliwa, wingu likampokea kutoka machoni pao. Walipokuwa wakikaza macho mbinguni, yeye alipokuwa akienda zake, tazama, watu wawili wakasimama karibu nao, wenye nguo nyeupe, wakasema, Enyi watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni.

Marko 16:19 Basi Bwana Yesu, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu.

Luka 24:51 Ikawa katika kuwabariki, alijitenga nao; akachukuliwa juu mbinguni.
1 Timotheo 3:16 Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu.

Zaidi ya yote Yeye ni Mungu asiyeshindwa, mwaminifu katika ahadi zake; wote waliomwamini wana ushuhuda kuhusu uzuri wake. Ziko shuhuda nyingi za matendo makuu yaliyotendeke ulimwenguni mwote kwa zaidi ya miaka 2000 sasa, na bado mambo yanazidi kutendeka kwa jina la Yesu. Manabii na mitume wengine (Wajumbe wa Mungu) wote waliotajwa katika Biblia wakitatwa majina yao hakuna linaloweza kutendeka. 

Katika Matendo ya Mitume 4:9-12 tunasoma,
Ndipo Petro, akijaa Roho Mtakatifu, akawaambia, .... jueni ninyi nyote na watu wote wa Israeli ya kuwa kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, ambaye ninyi mlimsulibisha, na Mungu akamfufua katika wafu, kwa jina hilo mtu huyu (aliyekuwa kiwete tangu tumboni) anasimama ali mzima mbele yenu. Yeye ndiye jiwe lile lililodharauliwa na ninyi waashi, nalo limewekwa kuwa jiwe kuu la pembeni. Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.

Leo hii katika makanisa ya kweli, na kwenye mikutano na semina ya waabuduo halisi tunashuhudia mambo makuu sana yakiendelea kutendeka; viwete wanatembea, vipofu wanaona, wagonjwa wanapona, watu wengi wanafunguliwa kutoka katika vifungo vya nguvu za giza na watu wengi wanapokea uweza wa kufanyika watoto wa Mungu na kuachana na dhambi.





"JAMANI--- "NI NANI KAMA YESU??????????????????"


Thursday, 5 September 2013

MWANA INJILI- Bish. MOSES KULOLA


Sijajua ni kwa jinsi gani unaitazama injili ya Yesu Kristo katika maisha yako binafsi, si jambo rahisi kama wengi wanavyodhani! Injili Ya Yesu sio kama yalivyo mbambo mengine yasemwayo. Paulo anasema, "Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia." warumi 1:16

Baba huyu aliamua kuyatumia maisha yake yote katika utumishi wa Injili. Je, wewe na mimi tunafanya nini?

Wednesday, 4 September 2013

WITO WA WOKOVU NI WA WOTE, USIJARIBU KUJITOA.

Kuna watu hujaribu kusema Yesu ni kwa ajili ya watu fulani tu, wengine husema Yesu ni wa Wayahudi, wengine husema ni wa walokole, wengine husema ni wa wakristo tu na madai mengine mengi. 
Kimsingi, Madai haya sio ya kweli kibiblia. Wayahudi walihusika kumpokea Yesu na kuwafungulia mataifa mlango. (Yoh. 1:12), Walokole (jina sahihi ni waliookoka) ni watu walioamua kumpokea Yesu na kuyaishi maisha ya ukristo, Wakristo ni mjumuiko wa watu waliojenga imani kwa Kristo (mmiliki wao ni Kristo-wanaitwa kwa jina lake. Hebu tuone Bibila inavyosema kuhusu Yesu:
Yohana 3:16, .........kila amwaminie asipotee bali awe na uzima wa milele" Hapa Biblia inatumia neno "kila" kumaanisha hakuna asiyestahili katika hili endapo yuko tayari kuamini.
Matendo. 4:12, Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo."
 Naamini unaona jinsi maneno haya yanavyotuambia, kwamba Jina la Yesu ni kwa ajili ya wokovu wetu sisis sote. Katika Yohana 3:16, Yesu anasema, "Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele." Natamani uone tu maneno "kila mtu" kwa hiyo kama wewe ni mtu ujue wokovu unakuhusu
2 Petro 3:9 "Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba" Bado Mungu anasisistiza kwamba yeye hapendi mtu yeyote apotee bali atubu. 
John 6:37 Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe.
Kupitia mistari hii tunaona jinsi Mungu alivyo na makusudi na maisha ya kila mmoja wetu. Katika Math. 11:28 anaita na kusema, "Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha." Je, ni mizigo gani inawatesa na kuwasumbua watu siku za leo? Naamini utakubaliana nami kwamba mizigo hii ni ya shetani na hatutakiwi kuibeba. Ni lazima tukubali kumpa Yesu mizigo hiyo ili sisi tuishi maisha ya uhuru na amani. Mistari hii tuliyoisoma inaonesha hasa kwamba mpango wa Mungu wa wokovu ni kwa wote,
Romans 3:23 "kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;"

Romans 5:12 "Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi;"
Mistari hii inaendelea kueleza juu ya hali ya dhambi tuliyozaliwa nayo, dhambi ile iliyofanya na Adama na Eva. Kuokoka basi ni swala la wote.

 KUOKOKA ni kupatana na Mungu kwa njia ya Yesu Kristo. [kumrudia Mungu]
 Kolosai2:14-15, -[Akaifuta hati ya kutushtaki….]
Effeso.2:14-15,-[Akakibomoa kiambaza cha kati kilichotutenga….]
1yoh.4:10,-………, Akamtuma mwanawe kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu.
2kor.5:19,-..Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake amee, asiwahesabie makosa yao; naye ametia  ndani yetu neno la upatanisho.
1Petr 3:18. {Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja Kwa ajili ya dhambi, mwenye haki Kwa ajili ya wasio haki, ili atulete kwa Mungu; …..}

    KUOKOKA ni Kumkiri Yesu kwa kinywa na kuuamini ufufuo wake.
 Warumi 10:9-10. {Kwa sababu ukimkiri Yesu Kwa kinywa chako ya kuwa Ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu UTAOKOKA. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata HAKI, na kwa kinywa hukiri hata kupata WOKOVU.}

     KUOKOKA ni Kumwamini Yesu [kumpokea Yesu] na kutubu dhambi na kuziacha; na kuupokea uwezo wa  kufanyika mwana wa Mungu. 
Yoh.3:16. {Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili  kila amwaminie asipotee, bali awe na uzima wa milele}
Yoh.1:12. {Bali wote waliompokea aliwapa uwezo WA KUFANYIKA WATOTO WA MUNGU, ndio wale waliaminio Jina Lake.}
KUOKOKA ni kuamini habari za Yesu (Injili) na kubatizwa katika mauti yake. Marko 16:16 Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa. 
Warumi 6:4 Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima. 
Wakolosai 2:12 Mkazikwa pamoja naye katika ubatizo; na katika huo mkafufuliwa pamoja naye, kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua katika wafu.

Ni muhimu sana ukaelewa kwamba ubatizo ni tendo la muhimu sana kwa kila mwamini, sio jambo la hiari ni agizo la Mungu kwamba watu wahubiriwe injili na wabatizwe. Mathayo28:19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu. 
Kwa hiyo wokovu wako hauwezi kukamilika kama hujauthibitisha kwa tendo la ubatizo. Katika kitabu cha Marko limewekwa wazi zaidi kwamba "Aaminiye na kubatizwa ataokoka" siyo kuamini tu kama wengi wanavyodai.
 Jambo la muhimu la kujua kuhusu ubatizo pia ni kwamba sio aina zote za ubatizo zinazokubalika mbele za Mungu kutokana na kusudi la ubatizo wa kweli. Ubatizo wa kweli ni ule unaosimamia misingi ya mitume na manabii kama watu waliotumika kuweka misingi ya imani ya kweli. Waefeso 2:20 Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni. Ubatizo waliobatiza mitume ndio ubatizo unaostahili kutumika siku za leo.
Je ubatizo huo ulikuwa na sifa gani?
  1. Ulifanywa na watu waliookoka, mitume na watumishi wengine walioamini hapo kwanza.
  2. Ulifanywa na watu waliojazwa na Roho Mtakatifu
  3. Ulifanywa kwa watu walioamini, wanaojitambua (wenye umri wa kutosha), waliosikia neno, walio tayari kumwishia Yesu.
  4. Ulifanywa kwenye maji mengi, kwa kusudi la kudhihirisha tendo la kuzamishwa likimaanisha kuzikwa na kufufuka pamoja na Kristo.  Warumi 6:3 Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? Yesu mwenyewe kama kielelezo cha imani yetu alibatizwa kwenye mto Yoridani. Marko 1:9 Ikawa siku zile, Yesu alikuja kutoka Nazareti ya Galilaya, akabatizwa na Yohana katika Yordani. Watu wengine pia walibatizwa katika mto huo, Mathayo 3:6 naye akawabatiza katika mto wa Yordani, huku wakiziungama dhambi zao.  Ukijifunza kwenye kitabu cha matendo pia utaliona jambo hili kwa undani zaidi.
Ni muhimu sana ukapeleleza ubatizo uliobatizwa usije ukawa mmoja kati ya watu wayapinduao maandiko. Hakuna dhambi mbaya kama kufundisha uongo na kuwadanganya watu wayaamini mambo yasiyo mapenzi ya Mungu. Kumbuka wokovu ni swala la mtu binafsi, hakikisha unasimama wewe kama wewe na kuyasimamia mapenzi ya Mungu.
  • Wokovu ni mpango wa nani? ``Mwanadamu au Mungu?
     Baadhi ya watu hudhani kwamba ni uamuzi wa wanadamu tu kuzungumza habari za kuokoka duniani, wengine hudiriki kusema, hakuna wokovu duniani.
Je, neno la Mungu linasemaje kuhusu swala la wokovu kwa mwanadamu? [Tazama, wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama, siku ya WOKOVU ndiyo sasa.] 2kor.6:2
Tena Yesu akasemaEnendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ATAOKOKA; asiyeamini, atahukumiwa. Tena katika Zab.16:3-Mungu anasema, Watakatifu walioko duniani ndio walio bora, hao ndio niliopendezwa nao.
    1Pet.1:6-´´Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.``
  •       KWA HIYO:
*    Wokovu ni mpango wa Mugu wa kumvuta na kumtoa  mwanadamu kwenye maangamizo ya dhambi na kumwingiza katika eneo alilolikusudia kwa njia ya imani.
Yeremia 31:3 -Mungu anasema,-´´Naam, nimekupenda kwa upendo wa milele, ndio maana nimekuvuta kwa fadhili zangu.``
Yohana.3:16- “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele”.
       Math.1:21. “………, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.”
      Yoh.1:29-“Tazama Mwanakondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu”.

*    Wokovu ni mpango wa Mungu kumtoa mwanadamu Kwenye  mauti na kumwingiza kwenye uzima. Warumi 6:23,            “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.”
Yoh.5:24. Yesu akasema, “………, yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka yu na uzima wa milele; wala  haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani.
Yoh.8:51, “Amin, Amin, nawaambia , mtu akilishika neno langu, hataona mauti milele.”
1pet.3:18, “Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu…..”

*   Wokovu ni mpango wa Mungu kumtoa mwanadamu kwenye ufalme wa giza [Utumwani]: penye dhiki, mateso, laana, vifungo, na maonezi yote ya ibilisi, na kumwingiza kwenye ufalme wake ulio chini ya Kristo Yesu ili apate kuwa huru.
Wakolosai.1:13, “Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika katika ufalme wa mwana wa pendo lake.``
Yoh.8:36, “Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.”
Yoh.8:34,- Yesu anasema,-Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.``
1Yoh.3:8,-´´Atendaye dhambi ni wa ibilisi, kwa kuwa ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za ibilisi.``

*   Wokovu ni mpango wa Mungu kumponya, kumfinyanga , kumtakasa , na kumfanya mwanadamu mwenye tabia ya asili  kwa upya kabisa kwa kumtoa Yesu ili awe fidia ya dhambi zote alizozitenda; na kumfanya kiumbe kipya chenye nafasi ya kuitwa Mwana [mototo]  wa Mungu .
Isaya.53:5, Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, alichubuliwa kwa maovu yetu. Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.” >> 1pet.2:24.
Yoh.1:12, “Bali wote waliompokea aliwapa uweyo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake.” 
2kor.5:17, “Hata imekuwa mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.”

                 MKUBALI YESU LEO AKUOKOE!!!

MWANAUME KWENYE NAFASI YA "MUME"

Mume ni mwanaume aliyeoa kwa kuzingatia vigezo na taratibu za kijamii, kishria na za kiroho. Mume si rafiki wa kiume (boyfriend), hawara, wa...

Powered By Blogger