Tuesday, 15 November 2016

JE, NI NINI HUTOKEA MARA TU MTU ANAPOOKOKA?

YAPO MENGI HUTOKEA.
“Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya” 2 Wakorintho 5:17
Ni vema mtu unapoamua kuokoka ukatambua mabadiliko ya msingi ambayo hutoe pao kwa papo ambayo, yanakufanya kuwa mtu wa tofauti na ulivyokuwa mwanzoni. Mtu anapokubali kuokoka, hutokea mabadiliko katika maeneo makuu manne.
A.     Mbinguni (Kwenye Ufalme wa Mungu).
Katika kitabu cha Luka15:10 Nawaambia, Vivyo hivyo kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye” Kwa hiyo kunakuwa na furaha mbinguni juu ya kurejea kwako katika Ufalme wa Mungu (ulikuwa mwana aliyepotea)  Neno linasema “malaika wa mbinguni anafurahia” mtu anapoamua kutubu na kumrudia Mungu.
Jambo jingine ambalo hutokea mbinguni ni, jina kuandikwa katika kitabu cha uzima. Luka 10:20 “Lakini, msifurahi kwa vile pepo wanavyowatii; bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni.” Wanafunzi walipokuwa wanafurahia utendaji kazi wa nguvu za Mungu; Yesu anawakumbusha kwamba jambo la kufurahia zaidi ni kule majina yao kuandikwa mbinguni na sio mapepo kutii. Kumbuka Yesu alikuja ili aturejeshe kwa Mungu, na majina yetu yatambulike tena mbinguni.
Ufunuo 21:27 “Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo. Hapa tunaona wenye fursa ya kuingia mbinguni ni wale tu ambao majina yao yameandikwa kwenye Kitabu cha uzima.
Wafilipi 4:3 “…. na wale wengine waliotenda kazi pamoja nami, ambao majina yao yamo katika kitabu cha uzima.” Mtume Paulo anaongea kwa uhakika kabisa akijua ya kwamba mtu anapoamua kuokoka moja kwa moja jina lake linaandikwa katika kitabu cha Uzima.
Revelation 20:15 “Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.” Hapa tunaona adhabu ya mtu ambaye jina lake halitaonekana kwenye kitabu cha uzima, kwamba atatupwa kwenye ziwa la moto (Jehanamu). Jambo hili linatupa kujipeleleza na kuona kama majina yetu kweli yameandikwa mbinguni.
Je, utajuaje jina langu limeandikwa mbinguni? Ni rahisi tu kujua, kama umetubu kweli na kumkiri Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako na kusimama katika utakatifu basi jina lako litakuwepo kwenye kitabu cha Uzima. Hiki ni kitabu cha watakatifu, yaani wale waliokubali kusafishwa kwa Damu ya Yesu kama tulivyoona kwamba Yesu alijisafishia watu ili wawe milki yake. Tena Roho Mtakatifu wa Mungu atakushuhudi ndani yako.
Tatu, unapata kibali cha kupokea siri na Baraka za rohoni ndani yake Kristo. Mtu anapokuwa hajaokoka anakuwa amefungwa na katika utu wa kale ambao hauna ushirika na Mungu. Hivyo anakuwa hana uwezo wa kurithi Baraka pamoja na Yesu. 1Korintho14 Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.
Kwa hiyo kwa kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wetu, tumefungua mlango wa kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu na kupokea nguvu na karama mbalimbali kutoka kwa Mungu.
Nne, Kumbukumbu za matendo yako mabaya zinafutwa, na kuanza ukurasa mpya wa maisha. Maandiko yanatuthibitishia kwamba hakuna dhambi inayokumbukwa tena, baada ya kutubu kweli na kumwamini Yesu. Katika Isaya 1:18
“Mungu anasema, Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu Sana, zitakuwa nyeupe Kama theluji; zijapokuwa nyekundu Kama bendera, zitakuwa kama sufu”.
Isaya 43: 25 “Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako.”
1Yohana 1:9 “Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.”
Kwa hiyo katika maneno haya tunapata ujasiri wa moja kwa moja kwamba mtu anapokubali kutubu dhambi na kuziacha kisha kumwishia Kristo katika maisha yake yote, maovu na dhambi zote alizozitenda vinafutwa kabisa. Tena, Mungu anasema hatazikumbuka tena na hakutakuwa na hukumu tna juu yake.
Tano, Uhusiano wako na Mungu unarejea upya; Kumbuka Yesu alikuja kufanya upatanisho kati ya mwanadamu mwenye dhambi na Mungu Mtakatifu. 2 Wakorintho 5:19 yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho.
B.     Kwenye mazingira yake (Duniani)
Unakuwa wakili wa Mungu katika dunia hii. Katika 1 Wakorintho 4:1 Paulo anasema, “Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za Mungu.” Tena Mtume Petro anasema, “Kila mmoja kwa kadiri alivyoipokea karama, itumieni kwa kuhudumiana; kama mawakili wema wa neema mbalimbali za Mungu” 1 Petro 4:10. Kwa hiyo ni lazima ujijue kwamba Mungu anataka akutumie kama mwakilishi wake hapa duniani katika eneo alilokuweka.
Unarejeshewa mamlaka ya kutawala na kumiliki pamoja na Kristo Yesu, Ufunuo 5:9-10 “Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.”Kwa hiyo, tunapokuwa ndani ya Kristo tunakuwa tumerejeshewa ile mamlaka tuliyoipoteza kupitia dhambi ya Adamu katika bustani ya Edeni.
Unakuwa adui wa dunia/unatengwa na dunia. 1Yohana 2:15 “Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia. Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele.”
Warumi 8:7 “Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuiti.”
Yakobo 4:4 “Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu.”Kumbe Mungu anatutaka tukajitenge na uovu wa kila namna na kuuvaa utakatifu pamoja na Kristo.

C.     Kwenye maisha binafsi
Unakuwa kiumbe kipya. 2 Wakorintho 5:17 “Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.”Hapa tunaelezwa wazi kabisa kwamba ndani ya Yesu tunakuwa viumbe vipya, tena yale mambo ya kale (ya dunia) yamepita.
Unafanyika mtoto/mwana wa Mungu. Yohana 1:12 “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake.” Warumi 8:16 “Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu.” Ni muhimu sana ukajua kuwa sasa wewe ni mtoto wa Mungu, na Mungu ni Baba yako.
Unapata raha nafsini baada ya kuondolewa mizigo na kusamehewa dhambi. Mathayo 11:29 “Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu” Tena katika Warumi 6:22 Mtume Paulo anazungumza juu ya kuwekwa huru mbali na dhambi, “Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa, na mwisho wake ni uzima wa milele.”
Neema ya kuwekwa huru kutoka kwenye vifungo inakuwa juu yako. Wakolosai 1:13 Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake; ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi” Unapokuwa ndani ya Kristo shetani anakuwa hana tena mamlaka ya kukaa ndani yako, hivyo unakuwa huru mbali na aina zote za vifungo. Japo maombi huwa yanahitajika ili mtu aweze kuwekwa huru kabisa. Yakobo anatupa kanuni moja ya msingi sana katika maisha yetu ya wokovu; anasema, “Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.” Yakobo 4:7
Mfumo wa kufikiria na kuamua unabadilika. Wakolosai 3:2 Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi. Tena Paulo katika Warumi 12:2-3 anatupa ushauri wa msingi sana, unaolenga kutusaidia katika kila maamuzi tunayofanya. “Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu. Kwa maana kwa neema niliyopewa namwambia kila mtu aliyeko kwenu asinie makuu kupita ilivyompasa kunia; bali awe na nia ya kiasi, kama Mungu alivyomgawia kila mtu kiasi cha imani.”
Unakuwa mbali na utumwa wa dhambi. Warumi 8:10 “Na Kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho yenu i hai, kwa sababu ya haki.”
Yohana 8: 31-32, 34-36 “….Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli; tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru. Yesu akawajibu, Amin, amin, nawaambia, Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi. Wala mtumwa hakai nyumbani sikuzote; mwana hukaa sikuzote. Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.”
Mistari hii inatuonyesha kwamba tulikuwa watumwa wa dhambi lakini sasa YESU anatuweka huru kabisa.
Unapokea vipawa na karama, pamoja na nguvu za Roho Mtakatifu. Matendo ya Mitume 2:38 “Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.” Tena kwenye Waefeso 4:8 Paulo anasema, “Hivyo husema, Alipopaa juu aliteka mateka, Akawapa wanadamu vipawa.”
Unaanza mfumo mpya wa mahusiano. Waefeso 2:14 Kwa maana yeye ndiye amani yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja; akakibomoa kiambaza cha kati kilichotutenga.” Hapa tunaona kulikuwa na matengano katikati ya wanadamu, ila Yesu alipokuja akajenga mahusiano upya. Katika Mathayo tano Yesu anatoa kanuni mpya za mahusiano.
Mathayo 5:38-45 “Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino; Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili. Na mtu atakaye kukushitaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia. Na mtu atakayekulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye mbili. Akuombaye, mpe; naye atakaye kukopa kwako, usimpe kisogo. Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako; lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi, ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.”
Mfumo wa uchumi na kazi unabadilika. Mathayo 6:33-34 “Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake. Mathayo 12:30 Mtu asiye pamoja nami yu kinyume changu; na mtu asiyekusanya pamoja nami hutapanya. Kwa hiyo baada ya kuokoka Ufalme wa Mungu unakuwa mbele, na tunakusanya pamoja na Mungu.
Tabia za Mungu zinaanza kudhihirika ndani yako kwa msaada wa Roho mtakatifu, na tabia za kidunia zinakosa nguvu. Wagalatia 5:22 “Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.”
D.    Kuzimu (Kwenye ufalme wa Shetani)
Jina linafutwa kwenye kumbukumbu za shetani. Wakolosai 1:13 Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake. Kuwa katika nguvu za giza maana yake tulikuwa katika himaya ya shetani, kumbukumbu zetu zilionekana kwa shetani. Tunapookoka kibao kinageuka, mambo yote yanafutwa.
Hati ya mashitaka inafutwa.  Katika Wakolosai 2:14 Paulo anasema, “akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani”.
Shetani anatangaza mpango rasmi wa kukutafuta.  1 Petro 5:8 Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze. Kwa hiyo ni muhimu ukatambua kwamba, kuzimu kuna mpango maalumu umekwisha kuwekwa ili kuhakikisha kwamba unarudi tena mikononi mwa shetani. Ni wewe sasa kusimama vizuri na Yesu anayesema, Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe. Yohana 6:37
Kimsingi, Mambo haya yanatuonyesha kuwa kuna mabadiliko makubwa ambayo hutokea mara tu matu anapoamua kuokoka (Kumpa Yesu Kristo maisha yake) Mabadiliko haya ndiyo humfanya mtu aone uhalisia wa wokovu katika maisha yake, na kumpa ujasiri wa kusimama katika upya kila siku. Tunaambiwa kwamba Neema YA Mungu hutufundisha kuukataa ubaya na tama za kidunia kisha tunapata kuishi kwa kiasi, na haki na utauwa katika ulimwengu huu wa sasa. Haya ni mabadiliko makubwa sana.
Katika Mathayo  3:8 “Yohana akawaambia Wayahudi, “Basi zaeni matunda yapasayo toba” Tena Paulo anawaambia Wafilipi “Lakini mwenendo wenu na uwe kama inavyoipasa Injili ya Kristo” (Wafilipi 1:27)
Tena kwenye Waefeso 4:22 anasema, “mvue kwa habari ya mwenendo wa kwanza utu wa zamani, unaoharibika kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya”
2Wakorintho 5:17 inasema, “Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.

Mistari hii inathibitisha zaidi na kukazia swala la kuwa na badiliko kamili na lenye matunda yaliyokusudiwa kwa majira na nyakati. Yaani matunda yaipasayo Toba na matunda yaipasayo Injili.

Wednesday, 21 September 2016

DHAMBI(SIN) NI NINI?


Neno Dhambi linadhihirika katika maandiko kama mjumuiko wa uovu, mabaya, hatia, makosa, ukengeufu na uasi. Vifungu vifuatavyo katika biblia vinatupa upana wa tafsiri hii:
Zaburi 51:1-9
“Ee Mungu, unirehemu, Sawasawa na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, Uyafute makosa (Transigressionon)yangu. Unioshe kabisa na uovu (iniquity) wangu, Unitakase dhambi (Sin) zangu. Maana nimejua mimi makosa yangu Na dhambi yangu i mbele yangu daima. Nimekutenda dhambi Wewe peke yako, Na kufanya maovu mbele za macho yako. Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo, Na kuwa safi utoapo hukumu.
Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu; Mama yangu alinichukua mimba hatiani. Tazama, wapendezwa na kweli iliyo moyoni; Nawe utanijulisha hekima kwa siri, Unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi, Unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji.  Unifanye kusikia furaha na shangwe, Mifupa uliyoiponda ifurahi. Usitiri uso wako usitazame dhambi zangu; Uzifute hatia zangu zote.”
Maneno ya asili (Ya Kiebrania)yaliyotumika kwenye maneno haya ni
Þ    Kwa neno Makosa (transigression) ni neno ‘peša’ likimaanisha ‘rebelliousness’ kufanya kinyume na utaratibu au uasi.
Þ  Kwa neno Uovu (Iniquity) limetumika neno ‘hātā’ linalomaanisha ‘moral misshapennes’ yaani kinyume na maadili ya ki-Mungu kwa makusudi. Neno hili limetumika mara 580 katika Agano la kale.
Þ    Neno sin limetokana na neno ‘āwōn’ linalomaanisha ‘shorticomings’Kupungukiwa na utukufu wa Mungu.
Katika Agano jipya yametumika maneno  ya Kiyunani mawili:
Neno ‘adikia’ linalomaanisha kufanya makosa (wrongdoing), kinyume na haki (Unrighteousness), na kinyume na sheria (Injustice). Katika kundi hili, dhambi inaonekana kuwa kitendo cha hiari anachokifanya mtu, kinachoweza kuleta madhara au uharibifu kwa mtu mwingine.
Neno jingine ni ‘hamartia’ ambalo limetafsiriwa mara nyingi kama Dhambi (Sin). Kundi hili la dhambi linajumuisha maneno yote ya Kiebrania yaliyotumika katika Agano la kale (yaani ‘āwōn’, ‘hātā’ na ‘peša’).

Dhambi (Sin) katika agano Jipya inamaanisha kukosa maadili ya ki-Mungu (Makosa), maovu na uasi mbele za Mungu.

1 Yoh. 3:4 Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi (rebellion). Kuasi ni kukiuka kwa makusudi taratibu au sheria zilizowekwa na mamlaka Fulani, ni kwenda kinyume na maagano au mapatano. Hili tunaliona kwenye kitabu cha mwanzo pale ambapo Adamu na Eva waliamua, japo kwa kudanganywa na shetani, kula tunda la mti ambao Mungu aliwakataza. (Mwanzo 3)
1 Yoh. 5:17 Kila lisilo la haki ni dhambi, na dhambi iko isiyo ya mauti.
Warumi 14:23 “… Na kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi.”

Mithali 24:9 Fikira za mpumbavu ni dhambi, Na mwenye mzaha huwachukiza watu.
Mithali 21:4 Macho yenye kiburi, na moyo wa kutakabari, Hata ukulima wa waovu, ni dhambi.
Ayubu 23:11 Mguu wangu umeshikamana sana na hatua zake; Njia yake nimeishika, wala sikukengeuka.
Kumb.11:28 na laana ni hapo msiposikiza maagizo ya Bwana, Mungu wenu, mkikengeuka katika njia niwaagizayo leo, kwa kuandama miungu mingine msiyoijua.
Dhambi imetafsiriwa tena kama “Matendo ya mwili”
Wagalatia 5:19 inasema, “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.
Tena, Dhambi ni Ibada ya sanamu. Wakolosai 3:5 “Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu; kwa ajili ya mambo hayo huja ghadhabu ya Mungu.”

Kuna tofauti kati ya dhambi kwenye Agano la kale na dhambi wakati huu wa Agano la Jipya.
Dhambi katika Agano la kale ilikuwa ni kule kuvunja sheria (Torati ya Musa), na kwenda kinyume na taratibu za dini ya Kiyahudi. Amri kumi za Mungu ndizo zilikuwa kielelezo cha Amri zote. Katika Warumi 4:15 mtume Paulo anatuambia “Kwa sababu sheria ndiyo ifanyayo hasira; maana pasipokuwapo sheria, hapana kosa.” Kwa hiyo kumbe watu walianza kuhesabiwa makosa pale sheria ilipowekwa.

Katika Agano la kale sheria na hukumu zake zilikuwa mikononi mwa waalimu wa Dini na Mafarisayo. Na walikuwa na uwezo wa kumhuku mtu yeyote kulingana na sheria hizo. Kwenye Waebrania 10:28 tunasoma “Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu.” Kwa hiyo watu wengi walikufa – utaratibu ulikuwa jino kwa jino, atakayeua kwa upanga atauwawa kwa upanga.

Warumi 8:3 Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili
Wakolosai 2:23 Mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana hekima, katika namna ya ibada mliyojitungia wenyewe, na katika kunyenyekea, na katika kuutawala mwili kwa ukali; lakini hayafai kitu kwa kuzizuia tamaa za mwili.

Paulo akizizungumzia taratibu za ibada ya Kiyahudi katika Wakolosai 2:23 akasema, “Mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana hekima, katika namna ya ibada mliyojitungia wenyewe, na katika kunyenyekea, na katika kuutawala mwili kwa ukali; lakini hayafai kitu kwa kuzizuia tamaa za mwili.
 Katika agano jipya dhambi ina upana zaidi.

Yale yaliyokuwa magumu kwa sababu ya sheria sasa katika Kristo Mungu anayafanya mepesi. Warumi 8:3 inasema “Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili”

Yesu alitangaza mfumo mpya wa maisha ya Kiroho.
Mathayo 5:23-48 “Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako, iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako……….   Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini; lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake……..Imenenwa pia, Mtu akimwacha mkewe, na ampe hati ya talaka; lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila mtimizie Bwana nyapo zako lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa; hata kwa mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu; wala kwa nchi, kwa maana ndiyo pa kuwekea miguu yake; wala kwa Yerusalemu, kwa maana ndio mji wa Mfalme mkuu.

Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi. Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu. Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino; Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili. Na mtu atakaye kukushitaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia. Na mtu atakayekulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye mbili. Akuombaye, mpe; naye atakaye kukopa kwako, usimpe kisogo. Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako; lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi, ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.
 Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo? Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo? Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.

Maeneo yaliyopigiwa mstari yanaonyesha hali ilivyokuwa kipindi cha sheria, lakini tunaona Yesu akitangaza mambo mapya na kusema, “lakini mimi ninasema” Kwa hiyo sasa tunasimama katika yale aliyoyasema Yesu yaani; Kuacha na kukaa mbali kabisa na zinaa, kutokuachana, kutokuapa, kuwapenda maadui na kuwaombea.
Tena katika Mathayo 22:37-39 Yesu akatangaza amri kuu mbili, “Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako.”

Katika sheria ni hapakuwa na kumpenda jirani kama nafsi, wa kukaa naye ni Yule tu ambaye alikuwa amekubalika kutokana na Torati. Kwa sababu hiyo Wayahudi walilazimika kujitenga na wanadamu wengine wote waliokuwa wanaabudu sanamu. Hapakuwa na kuchangamana.
Yesu alipokuja sasa tunaambiwa:
Waefeso 2:14 Kwa maana yeye (Yesu) ndiye amani yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja; akakibomoa kiambaza cha kati kilichotutenga.
2 Wakorintho 5:17 Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.

Wagalatia 2:16 hali tukijua ya kuwa mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria, bali kwa imani ya Kristo Yesu; sisi tulimwamini Kristo Yesu ili tuhesabiwe haki kwa imani ya Kristo, wala si kwa matendo ya sheria; maana kwa matendo ya sheria hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki.
Warumi 8:1 Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.

Warumi 6: 17-23 “Lakini Mungu na ashukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mliitii kwa mioyo yenu ile namna ya elimu ambayo mliwekwa chini yake; na mlipokwisha kuwekwa huru mbali na dhambi, mkawa watumwa wa haki.  ….  Kwa kuwa kama mlivyovitoa viungo vyenu vitumiwe na uchafu na uasi mpate kuasi, vivyo hivyo sasa vitoeni viungo vyenu vitumiwe na haki mpate kutakaswa. Kwa maana mlipokuwa watumwa wa dhambi, mlikuwa huru mbali na haki. Ni faida gani basi mliyopata siku zile kwa mambo hayo mnayoyatahayarikia sasa?
Kwa maana mwisho wa mambo hayo ni mauti. Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa, na mwisho wake ni uzima wa milele. Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.”


Thursday, 8 September 2016

FIKIRI TOFAUTI

KWA NINI NIKO HAPA HAPA? 
(Why Am I  here?)

       Hili ni swali ambalo kila mwenye akili atajiuliza akiona amekaa eneo moja kwa muda mrefu bila kuona mabadiliko chanya yaliyokusudiwa au yaliyotazamiwa. Kuna kipindi wana wa Israeli walifika mahali wakawa wanazunguka milima ya Seiri, tena kwa miaka mingi Mungu aliwatokea na kuwasaidia kwa kuwapa mwelekeo mpya. "Mlivyouzunguka mlima huu vyatosha; geukeni upande wa kaskazini." (Kumbukumbu 2:3)





      Angalia maneno haya aliyoyasema mwanamashahiri mahiri William Shakespeare ‘There is nothing good or bad, but thinking makes it so.’ kwa kiswahili anasema, "Chochote kiwe kibaya au kizuri, ni mawazo au fikra hukifanya hivyo. Hakika vile unavyofikiri ndivyo utakavyojijenga. Kwani maamuzi ya mtu huongozwa na mawazo ya mtu. Mawazo duni husababisha maamuzi duni. Matendo ya mtu ya leo ni matokeo ya mawazo yake ya jana.





     Biblia inazunguimza juu ya vitu ambavyo humtia mtu unajisi. "Kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi. Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati, wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu. Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi." (Marko 7:23), Kwa hiyo kumbe mtu hawezi kuwa mzinzi kama mawazo ya uzinzi hayako ndani yake; tena hawezi kuwa muuaji, mwizi, mkorofi, mlafi nk nk kama hajawahi kuyawaza hayo.





     Hebu nikuulize wewe unawaza nini? Unaweza ukawa unapambana na mambo fulani au tabia fulani ndani ya maisha yako bila mafanikio. Anzia kwenye kubadili jinsi unavyofikiri. Leo nakushauri kama unataka kufanya tofauti, fikiri tofauti. Fikra zako zikiwa zinawaza mambo madhaifu, ugumu, mabaya, maovu na mengine kama hayo bila shaka huweza kuyaepuka mambo haya. Mawazo ya kujidharau yakikutawala hautakaa uheshimike, hashima ya kweli, mafanikio ya kweli huanzia ndani ya mtu. Ili uwaze tofauti kuna mambo ni lazima uyape kisogo, uyaepuke kwa nguvu zote.

Epuka:
1. Kuangalia mambo yaliyopita (your past) na kuvunjika moyo. Huwezi kurudi nyuma kurekebisha makosa ila unweza kujifunza kitu cha kuzalisha (constructive) kutoka kwenye makosa au kufeli huko kulikopita. "Past is past because it has passed, future is future because it is yet to come. Nothing can be changed about past but future is your decision." 
    Kuangalia mambo yaliyopita sio kwamba ni vibaya kwani ni muhimu kuishi maisha ya kujitathmini, tatizo lipo kwenye kuwekeza moyo wako (fikra) zako huko. Waswahili husema, "Yaliyopita si ndwele tugange yajayo" tena wakasema"Maji yakishamwagika hayazoleki" Paulo naye akasema "Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele. (Wafilipi 3:13)

2. Kuwaza mambo manyonge. Mambo makubwa ndiyo yatakayokupa kupanuka kifikra, kiubunifu na hatimaye kiutendaji na Mafanikio. Waza mambo makubwa yanayowezekana, mwamini Mungu na kutenda kwa bidii utafanikiwa.

3. Kuwa na mawazo ya kushindwa. Mawazo ya kushindwa ni sumu ya mafanikio, hata kama umejaribu ukakwama. Jaribu tena na tena hadi uone mafanikio. Mawazo ya kushindwa yatakufanya utangetage hata kukosa kabisa mwelekeo.

4. Kuwaza  maovu na mambo machafu. Mawazo machafu ni kitovu cha maamuzi mabovu. Tunza fikra zako kwa kutazama, kusoma na kusikiliza vitu vya kujenga ufahamu badala ya vitu vya kipuuzi. Soma vitabu, sikiliza wasomi na watu wenye hekima, tazama mambo mazuri achana na marafiki wabaya.

5. Kuchukulia mambo kikawaida. Kumbuka kuna leo na kesho, fanya mambo kwa umakini na maarifa. Ongeza bidii na juhudi zaidi kila siku.
6. Kufanya mambo vilevile kila siku kila wakati. Tafuta kuboresha jambo lako kila siku, litazame ujiridhishe.





Kumbuka Mungu alipomaliza kuumba ulimwengu na vitu vyote, alitazama na akaona kuwa ni vyema. Na wewe jifunze kuyatazama mambo kwa jicho la tathmini.





NENO LANGU KWAKO MPENDWA: 

"FIKIRI TOFAUTI ILI UWE WA TOFAUTI".
Ili ufikiri tofauti:
1.  Yakumbuke makuu ya Mungu ( Yale uliyofanikiwa) na utiwe moyo kwa hayo.
Daudi alipokuta wana wa Israeli na jeshi lote wamenywea kwa jeshi la wafilisti alifikiri tofauti na hatimaye akafanya tofauti. Alitazama mambo makuu ambayo Mungu alimtendea akatiwa nguvu akasimama kumwangusha Goliati. Unapowekeza muda wako mwing kufikiria juu ya mambo uliyoshindwa ndivyo unavyozidi kujidhoofisha.

Wekeza muda wako kuyakumbuka makuu ya Jehova, utasikia kuinuliwa sana. Kazi kubwa ya waliyoshindwa ni kutengeneza hadithi nzuri juu ya kushindwa kwao, bali waliofanikiwa hutengeneza hadithi mbaya kuonyesha sabababu zilizoshindwa kuwafanya washindwe. Majaribu kwao ni mtaji si mateso.

2. Kataa maovu kama Yusufu aliyofanya.
Uovu na dhambi vimezimisha ndoto za wengi. Wengi wameishia mahali duni na pa kukosa tumaini kwa sababu ya kuendekeza maovu. Hakuna raha wala amani kwa watenda mabaya. Mafanikio ya kweli huambatana na wenye haki, wanaowatanguliza wengine. Yusufu alimkimbia mke wa Potifa akaendelea kushikilia maono yake. Majaribu kama hayo ni mengi nyakati hizi lakini ukiamua kukimbia hakika Mungu atakupeleka kwenye ndoto zako. Uovu na nguvu ya kutawala moyo (nia, hisia, na mawazo).

3. Jifunze kutazama fursa mbalimbali na kuchukua hatua.
Usione fursa zote ni za wengine, kaa mkao kutafuta na kuchangamkia fursa. Daudi alipomwona Goliati alitafuta namna ya kuitumia ile fursa kwa kuulizia wengine. Alipochukua hatua ngumu alipanda thamani ndani ya dakika chache. Na wewe usilale, fanya kitu. Pigana na Goliati wetu nasi tutakupa heshima. Hupaswi kulazimisha kuheshmiwa kama wengi wanavyong'ang'ania heshima za vyeo, fanya kitu heshima yako itapanda yenyewe.

4. Ambatana na watu waliofanikiwa zaidi yako kifikra na kimaendeleo.
Watu waliopiga hatua wakati mwingine huwa sababu ya sisi kuvutwa na kufuata nyao zao. Wengi pia hupenda kuwainua wengine. Watu waliofanikiwa wanaweza kukujenga sana kifikra, kwani wengi huwa hawaamini katika kushindwa. Na huwa na mbinu nyingi na shuhuda zenye kujenga sana. Pia, huwa wanakutana na fursa nyingi sana.

5. Fuatilia mambo yenye kujenga (achana na mambo ya kipuuzi)
Tumia muda wako katika mambo ya kujenga, pata taarifa zenye tija. Mawazo ya wengi yamejaa mambo yasiyo na faida kwa sababu ya kusikiliza, kutazama na kusoma upuuzi. Tafuta kanda, vitabu, magazeti na sikiliza vipindi vya maana. Kuangalia ponografi, kusikiliza manyimbo ya kihuni, kushabikia mipira, kubeti, na mengine kama haya ni kupoteza muda wa thamani wa maisha yako.

6. Soma vitabu na kujifunza kila siku.
Kusoma si lazima uende shule, nunua vitabu vya kiroho, vya uchumi, vya kisiasa na vinginevyo ujiendeleze. Mawazo yako yanaweza kunolewa na watu waliofanikiwa kupitia yale waliyoandika. Usiwe mvivu wa kusoma.

8. Mtegemee Mungu na kusoma neno lake kwa bidii.
Mungu ndiye chanzo cha mafanikio yake. na kumcha yeye ni chanzo cha maarifa yote (Mith 7:7). Mtegemee Mungu, usiamgalie mazingira na kukata tamaa, Ishi ahadi za Mungu na uache kufikiri kinyonge. Mungu akiwa upande wetu hatupaswi kuogopa. 

9. Sikiliza mahubiri na kanda za mambo ya kiroho.
Kusikiliza kuna nguvu kubwa sana. unaposikiliza unajipa fursa ya kufikiri na watu waliofanikiwa kupata fikra njema kutoka kwa Mungu. mahubiri yana siri kubwa sana. Pata muda usikilize na Mungu atakupa kufikiri kwa utofauti.

10. Badilisha marafiki ulionao (Achana na marafiki wasiojitambua)
Katika kitabu cha Mithali tunasoma "Chuma hunoa chuma; Ndivyo mtu aunoavyo uso wa rafiki yake." Mithali 27:17 Marafiki wa umbea, mizaha, masengenyo, wavivu, wenye wivu, walevi, wazinzi, wezi, wahuni ni kaburi wazi la ndoto zako. Hakikisha kama wewe ni chuma (Strong) unatafuta marafiki chuma ili mnoane. Marafiki wabaya huharibu tabia ya mtu mwema. Watakupotezea heshima. Huwezi kuaminika ukiwa na marafiki wasioaminika. 

Uwe na marafiki wenye fikra za mafanikio, mawazo ya kujenga, wanaojiamini na wanaoamini katika kufanikiwa, wenye imani katika Mungu. Nawe utafikiri kama wao au zaidi yao na kisha utafanikiwa kama wao au zaidi yao.




Katika haya na mengine utakayojaliwa na Mungu kibinafsi, utaanza kuwaza kwa tofauti na baadaye utaamini kwa tofauti, kisha kufanya kwa tofauti na kufanikiwa kwa tofauti.


Mungu akubariki kwa kuwa sehemu ya blog hii. Karibu kwa masomo mengine.

Mwl. Stephen M. Swai
0713511544

THE TRUTH ABOUT SALVATION

Some people in this world weather due to lack of clear knowledge or any other reason, get confused on the term Salvation. Some say it is not possible for a person to be saved. Some think that to be converted to a certain religion or denomination is the same as Salvation. Now, what is it real?

Wow! I’m sure this is right time for God to talk to you about SALVATION in Jesus Christ. Apostle Paul in 2 Corinthians 6:2 says, “I tell you now is the time of God’s favor, now is the day of salvation.” It might be you have heard about Salvation in one way or the other but today is so special for you to hear this Good news about Jesus Christ. 
Salvation is all about Jesus Christ, that is what made Him to come on earth "TO SAVE THE WORLD" in Matthew 1:21, the Angel of God speaks to Joseph about Mary. The Angel says, "She will have a son, and you will name him Jesus-because He will SAVE his people from their sins" 
Then in John 3:16-18 we read "For God so loved the world, that he gave his only begotten Son, that whosoever believeth in him should not perish, but have everlasting life. For God sent not his Son into the world to condemn the world; but that the world through him might be saved. He that believeth on him is not condemned: but he that believeth not is condemned already, because he hath not believed in the name of the only begotten Son of God."

Here you can the Love of God to us human being, because of our sins Jesus is given as a ransom. In 2Peter 3:9 we read, "
The Lord is not slack concerning his promise, as some men count slackness; but is longsuffering to us-ward, not willing that any should perish, but that all should come to repentance"
Remember we are all sinners!
In Romans 3:23 we read that "We are all sinners and we have fallen short of glory of God" Then under sin:
- We were all died (Ephesian 2:1)
- We were darkness (Ephesian 5:8)
- We were under powers of darkness (Colossians 1:13)

In Ephesian 2:8 we read that:

It is grace of God
It is by faith in Jesus Christ we are all saved
In the book of John 1:12 we read, "But as many as received him, to them gave he power to become the sons of God, even to them that believe on his name"
  • In Jesus, we are new creatures: In 2Corithians 5:17 we read "Any one who is joined to Christ is a new being; the old is gone, the new has come"
  • In Christ we have eternal life: Romans 6:23 we read "For the wages of sin is death; but the gift of God is eternal life through Jesus Christ our Lord"
  • We have moved from dearth to life: John 5:24  says "I am telling you the truth: those who hear my words and believe in him who sent me have eternal life. They will not be judged, but have already passed from death to life"
  • In Jesus we are free from slavery of sin. (John 8:31,34-36)

So, salvation is neither church membership nor religion, but the plan of God to save the lost man from bondage of sin. You may be a faithful member of a certain denomination, religion or church but that doesn't guarantee your salvation. 
Salvation is much about restored relationship between sinful man and Holy God through blood of Jesus shaded at the cross of Calvary.  Jesus came for reconciliation between us and Almighty God 
Now is the time for you to make decision, and accept Jesus as your Lord and Savior. 

Tuesday, 21 July 2015

Masomo/shule na wokovu

 Kikawaida kila mazingira huwa na changamoto za aina yake kwa mtu aliyeokoka, aliyeko kwenye biashara ana za aina yake, aliajiriwa naye vivyo hivyo, iwe ni mjini au kijijini, shuleni au nyumbani. Vilevile mfumo unaoweza kumfanikisha mtu unatofautiana kulingana na mazingira na changamoto; na kila changamoto zina jinsi ya kukabiliana nazo.
Ninaposema masomo namaanisha masomo ya kawaida ya darasani ambayo huwa tunayaita hasa shule. 
Unapokuwa masomoni ni lazima ujue kwamba kusimama katika wokovu kuko palepale, hautaweza kujitetea kwa lolote mbele za Mungu endapo utauacha wokovu. Haijalishi masomo yanaonekana magumu kiasi gani, bado Mungu anatarajia kupata matunda mazuri kutoka kwako katika hatua hiyo ya maisha. 
Katika kipindi hiki tulichonacho cha mapinduzi makubwa ya kisayansi na teknolojia pamoja na kampeni kubwa ya utandawazi (Globalization); vijana wengi walioko masomoni wamepoteza mwelekeo wa maisha yao ya kiroho.

Tuesday, 25 February 2014

UMUHIMU WA KUWA IMARA KATIKA UTUMISHI AU KIROHO

Haleluya!
Uimara ni wa muhimu sana kwa kitu chochote. Kama kitu kitakuwa na sifa nyingine zote kama vile sura nzuri, muundo mzuri, au hali ya kuvutia kabisa ni lazima kuulizia kuhusu uimara wake. Kitu imara ni kitu cha kuaminika.

Uimara ni uwezo wa kudumu kwa muda mrefu, uwezo wa kukabiliana na mazingira, uwezo wa kustahimili mazingira magumu, uwezo wa kuzalisha kilichokusudiwa kwa kiwango, kiasi na hali iliyokusudiwa bila kupoteza ubora. Ubora huonakana zaidi wakati wa misukosuko. Kama kitu au mtu hatosimama imara wakati wa kujaribiwa au wa kupitia changamoto basi uimara umekosekana.

Swali: Je, ni muhimu kwa mtu aliyeokoka kuimarika kiroho

         Paulo akasema, "Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana sikuzote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana."1 Wakorintho 15:58 Mstari huu ni wa msingi sana kwa maisha ya kila mkristo. Paulo anasema tuimarike, tusitikisike, na tuzidi sana kuitenda kazi ya Mungu. Mpendwa misukosuko ya Imani ni Mingi sana katika ulimwengu huu.

        Shetani yupo kila siku kutupiga vita (Waefeso 6:10-12, 1Petro 5:8), tena tunavutwa sana na tamaa zetu wenyewe (Yakobo 1:14). Mungu naye kuna wakati hutujia na kipimo, kuangalia kama tunaweza kuonyesha uthabiti kwa hatua nyingine. (Alifanya hivyo kwa Danieli na wenzake, pia Ayubu). Tusipoimarika hakika hatutaweza kusimama wakati wa kujaribiwa kwetu. Tunapaswa kuwa na Imani thabiti, isiyotikisika wala kubadilika. Yaani tumng'ang'anie Yesu hata kufa.

Kiujumla, Kuimarika huambatana na:

1. Uwezo wa mwamini kustahimili majaribu. 

          Yesu alisema wazi kwamba hapa duniani tutakutana na dhiki (Yohana 16:33) Tena akasema malipo yetu hapa duniani ni mara mia lakini yamechanganyika na udhia (Marko 10:30) Kinachotupa moyo ni kwamba Yeye yupo pamoja nasi. Tena Paulo anatuambia "Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili." 1 Wakorintho 10:13 

Tena Yakobo katika Yakobo 1:12 anasema, "Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao."Kumbe kuna taji tutakayoipata kwa kustahimili majaribu. Ustahimilivu ni tunda la kuimarika katika imani. Wengi ambao hawajaimarika wamekuwa wepesi wa kukata tamaa na kurudi nyuma. Ni muhimu kuamua kujiimarisha katika Imani ili uweze kustahimili hatamaye ukaipokee taji ya uzima.


Kama Yakobo alivyotangulia kusema, "Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi. Saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno.Yakobo 1:2-4 

Sio jambo rahisi kuhesabu ni furaha tupu uwapo kwenye majaribu, unahitajika uimara katika hali ya rohoni ili kubadilishugumu wa mwilini kuwa wepesi. Wapendwa wengi kwa sababu ya mapito wameamua kujiunga na Imani potofu na kusikiliza mafundisho manyonge yanayosisitiza juu ya mafanikio katika ulimwengu huu bila kujali umilele. Tukiimarika katika Imani hakika tutaweza kufurahi katika mateso na dhiki kwa ajili ya ufalme wa Mungu.

2. Ushujaa na ujasiri katika kuitenda kazi ya Mungu na kulitimiza kusudi Mungu alilokuitia.
  
Tunda lingine la kuimarika ni ujasiri na ushujaa katika kazi. Mungu anamwambia Joshua, "Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana ni wewe utakayewarithisha watu hawa nchi hii niliyowaapia baba zao ya kwamba nitawapa." (Yoshua1:6) Kazi ya utumishi katika mwili wa Kristo inahitaji ujasiri mwingi. Vita kwa watumishi ni vikali sana, tena kuna wakati wa kupita katika kupepetwa hata kukataliwa. Tumetumwa kamaa kondoo katikati ya mbwa mwitu (Mathayo 10:16)

Mungu ametuita katika mazingira yenye uadui mkubwa kwa kile tulichotumwa kufanya. Tumepewa kuihubiri Injili ya Yesu Kristo ili watu waokolewe na waondoke kwenye mikono ya Ibilisi. Hii si kazi rahisi, tunahitaji roho ya ujasiri na ushujaa mkubwa. Paulo anasema tuwe hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake (Waefeso 6:10). 

Hatupaswi kuogopa, malango ya kuzimu hayawezi kulishinda kanisa la Mungu. Watumishi wa kweli hawawezi kuogopa wingi wa manabii wa uongo. Tuna ujasiri kama simba, hatuwezi kuogopa dini au dhehebu linalochafua Imani, hatuwezi kuogopa serikali (japo tunaiheshimu) inapoingia kwenye anga za ufalme wa Mungu. Hapa ni ujasiri baada ya kuimarika katika Imani.

3. Furaha na amani katika kuyatimiza mapenzi ya Mungu, si mtu wa kujilaumu.


Tunda lingine la kuimarika ni furaha katika shria ya Mungu. Tumeitwa kufurahi katika Bwana (Wafilipi 4:4) Tena tunapomtumikia Mungu na kuyafanya mapenzi yake tunajisikia furaha na amani hata kama tunayatimiza kwa machozi. Paulo alistahimili vifungo na mapigo mengi akiwa na furaha tele ndani yake Kristo. Hakumlaumu Mungu wakati wa mateso yake; mfano alipokuwa gerezani yeye pamoja na Sila, aliendelea kumsifu Mungu kwa furaha na kuomba. Alifanya yote kwa furaha na amani.

 Yesu alikubali kushinda njaa kwa ajili ya kuyasimamia mapenzi ya Mungu. Aliyachukulia mapenzi ya Mungu kama chakula chake. Yesu akawaambia, Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka, nikaimalize kazi yake. Yesu anakazia swala la kumaliza kazi. (Yohana 4:34)

Upendo wetu kwa Mungu haupaswi kuwa wa maneno matupu, bali ni maisha halisi ya kuishi kulingana na maagizo au amri za Mungu. "Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito."1 Yohana 5:3 Watu ambao hawajaimarika huziona nzito sana sheria za Mungu. Tukiimarika katika Imani hatutaona ugumu kumfuata Mungu. Tutakuwa tayari hata kuyatoa maisha yetu kwa ajili ya kazi ya Mungu. Hatutajilaumu tutakapojikuta  tumeachwa peke, au kusalitiwa. PAulo alikutana na wasaliti wengi lakini aliendelea mbele.

4. Tumaini imara kwa Mungu.

Hakuna tumaini kwa watu wenye imani dhaifu au wasio na imani. Kumtumaini au kumngoja au kumtegemea Mungu kunahitaji Imani. Kumbuka Mungu hatumwoni kwa macho ya damu na nyama. Na kila tunachokijua kuhusu Mungu ni kwa njia ya Imani. Tunaokolewa kwa Imani na tunapaswa kuishi kwa Imani (Waebrania 10:38) Haya ni maneno ya mtu mwenye tumaini "Tazama, Mungu ndiye wokovu wangu; Nitatumaini wala sitaogopa; Maana Bwana YEHOVA ni nguvu zangu na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu".(Isaya 12:2)

Nabii Isaya anasema "Mtumainini Bwana siku zote Maana Bwana YEHOVA ni mwamba wa milele." (Isaya 26:4) Tumaini hili haliji bila Imani thabiti kwa Mungu. Katika Mithali 14:26 tunasoma, "Kumcha Bwana ni tumaini Imara" Nabii Yeremia naye akasema, "Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni tumaini lake. (Yeremia 17:7)

Tumaini Imara ni udhihirisho wa Imani thabiti. Na tumaini letu kwa ajili yenu ni imara, tukijua ya kuwa kama vile mlivyo washiriki wa yale mateso, vivyo hivyo mmekuwa washiriki wa zile faraja. (2 Wakorintho 1:7) Kuaminiana katika utumishi hujenga tumaini imara kati yetu. Na kwa sababu sote tunamtumaini Mungu inakuwa vyepesi kwa Mungu kumtumia kila mmoja wetu kwa ajili ya mwenzake.

Paulo anamwita Mungu wetu, Mungu wa tumaini. Yaani Mungu anayeweza kutumainiwa (ni Mungu wa tumaini letu). Warumi 15:13 "Basi Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mtakatifu." Hapa neno linatuongezea kitu cha ziada juu tumaini tulilonalo katika Mungu. Mungu hutujaza furaha na amani katika kuamini kwetu. Tena katika nguvu za Roho Mtakatifu tunazidi kuimarika katika tumaini letu kwa Mungu. Tumaini hili linahitaji uimara katika Imani.

5. Kumzalia Mungu matunda.

Mti hauwezi kuzaa matunda kabla haujakomaa. Ni lazima kwanza uote mizizi na matawi yake yaimarike vya kutosha ndipo utakapotoa maua na hatimaye kuzaa matunda. Vivyo hivyo na sisi katika maisha yeti ya rohoni pamoja na utumishi, hatuwezi kuzaa matunda tukiwa bado wachanga na tusio na mizizi. Tuanatakiwa tuimarike ili tuweze kuzaa matunda kwa ile mbegu ya Neno la Mungu iliyopandwa ndani yetu. 

Ona Yesu anavyosema, 
"Na zile penye udongo mzuri, ndio wale ambao kwa unyofu na wema wa mioyo yao hulisikia Neno, kisha hulishika; kisha huzaa matunda kwa kuvumilia." (Luka 8:15) Uvumilivu ni tunda la uimara. Mtu ambaye emelegea katika Imani hawezi kuwa na uvumilivu. Kuna misukosuko mingi inayotupata sisi tuliolipokea Neno la Mungu. 

Yesu anataja baadhi katika mfano huu wa mpanzi; yaani Ibilisi (Kando ya njia), Ugumu wa moyo (mwamba), shughuli na udanganyifu wa mali. Mambo haya si mepesi, yanahita uthabiti na uimara ili mtu aweze kuyakabili.

Paulo anashauri juu ya mwenendo ambao pia husababishwa na uimara wetu katika Imani. Anasema, "mwenende kama ulivyo wajibu wenu kwa Bwana, mkimpendeza kabisa; mkizaa matunda kwa kila kazi njema, na kuzidi katika maarifa ya Mungu; (Wakolosai 1:10) Tunawajibika kwa mengi katika ufalme wa Mungu. Tunapaswa kuabudu, kutumika, kuujenga mwili wa Kristo kwa karama na vipawa pamoja na kuwapeleka walioitwa kwa sadaka zetu. Haya yanihitaji uimara katika maisha yetu ndani ya Kristo. Vinginevyo tutaishia kuogopa na kulalamika.

 Paulo anamwambia Tito, "Watu wetu nao wajifunze kudumu katika matendo mema, kwa matumizi yaliyo lazima, ili wasiwe hawana matunda." Tito 3:14 Hili linatufundisha kujizuia, tabia hii ni kiutu uzima. Watoto katika imani hawawezi kufanya hivyo. Watu walioimarika kwenye Imani wana uwezo wa kusimamia matumizi ya kila walichopewa na Mungu ili kuweza kuzaa matunda. 

Katika 1Wakorintho 13:11, Paulo anasema ameyabatilisha "mambo ya kitoto" yaani hafikiri au kufanya tena kama mtoto; ameshakuwa mtu mzima (ameimarika). Mambo kama kuzunguka kwenye vibanda vya maombezi, kukimbia michango kanisani, kuwadharau viongozi, kujivuna kwa sababu ya huduma, kutumia ulaghai kupata fedha na mengine ni mambo ya kitoto. Watu wazima (walioimarika) wanatafuta kazi: yaani wafunge, wajitoe na kujitolea, wakeshe, wahubiri Injili mitaani, waandike vitabu, wapanue huduma (si kugombana na wachungaji) na mengine kama hayo.

FAIDA ZA KUMCHA MUNGU

Kumcha Mungu kunamaanisha kuwa na hofu ya Mungu (fear of The lord), kumuheshimu Mungu kwa kiwango cha juu, kumpa Mungu nafasi anayostahili. Kumcha Mungu kunajumuisha kumuheshimu(kumwabudu), kumtii, kumtukuza na kumtumikia kama Mungu.
2 Mambo ya Nyakati 19:7 Basi sasa hofu ya Bwana na iwe juu yenu; angalieni mkaifanye; kwa maana kwa Bwana, Mungu wetu, hapana uovu, wala kujali nafsi za watu, wala kupokea zawadi.
Mathayo 10:28 Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika jehanum.(Mungu)
Mithali 22:4 Thawabu ya unyenyekevu ambao ni kumcha Bwana Ni utajiri, na heshima, nayo ni uzima.
KUMCHA MUNGU KUNA FAIDA NYINGI

  1. Kunatupa mahusiano mazuri na Mungu.  Isaya 57:15 "Maana yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye milele; ambaye jina lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo patakatifu; tena pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea, ili kuzifufua roho za wanyenyekevu, na kuifufua mioyo yao waliotubu."  Mstari huu unatuweka wazi kwamba, watu wanaoweza kupata nafasi ya kukaa na Mungu ni wale wenye toba na unyenyekevu. 

A Strong Marriage vs. A Good Family: Understanding God's Order

In many Christian homes, there is a deep desire to build a good family. Parents work hard to provide for their children, maintain a peaceful...

Powered By Blogger