Wednesday, 21 September 2016

DHAMBI(SIN) NI NINI?


Neno Dhambi linadhihirika katika maandiko kama mjumuiko wa uovu, mabaya, hatia, makosa, ukengeufu na uasi. Vifungu vifuatavyo katika biblia vinatupa upana wa tafsiri hii:
Zaburi 51:1-9
“Ee Mungu, unirehemu, Sawasawa na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, Uyafute makosa (Transigressionon)yangu. Unioshe kabisa na uovu (iniquity) wangu, Unitakase dhambi (Sin) zangu. Maana nimejua mimi makosa yangu Na dhambi yangu i mbele yangu daima. Nimekutenda dhambi Wewe peke yako, Na kufanya maovu mbele za macho yako. Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo, Na kuwa safi utoapo hukumu.
Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu; Mama yangu alinichukua mimba hatiani. Tazama, wapendezwa na kweli iliyo moyoni; Nawe utanijulisha hekima kwa siri, Unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi, Unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji.  Unifanye kusikia furaha na shangwe, Mifupa uliyoiponda ifurahi. Usitiri uso wako usitazame dhambi zangu; Uzifute hatia zangu zote.”
Maneno ya asili (Ya Kiebrania)yaliyotumika kwenye maneno haya ni
Þ    Kwa neno Makosa (transigression) ni neno ‘peša’ likimaanisha ‘rebelliousness’ kufanya kinyume na utaratibu au uasi.
Þ  Kwa neno Uovu (Iniquity) limetumika neno ‘hātā’ linalomaanisha ‘moral misshapennes’ yaani kinyume na maadili ya ki-Mungu kwa makusudi. Neno hili limetumika mara 580 katika Agano la kale.
Þ    Neno sin limetokana na neno ‘āwōn’ linalomaanisha ‘shorticomings’Kupungukiwa na utukufu wa Mungu.
Katika Agano jipya yametumika maneno  ya Kiyunani mawili:
Neno ‘adikia’ linalomaanisha kufanya makosa (wrongdoing), kinyume na haki (Unrighteousness), na kinyume na sheria (Injustice). Katika kundi hili, dhambi inaonekana kuwa kitendo cha hiari anachokifanya mtu, kinachoweza kuleta madhara au uharibifu kwa mtu mwingine.
Neno jingine ni ‘hamartia’ ambalo limetafsiriwa mara nyingi kama Dhambi (Sin). Kundi hili la dhambi linajumuisha maneno yote ya Kiebrania yaliyotumika katika Agano la kale (yaani ‘āwōn’, ‘hātā’ na ‘peša’).

Dhambi (Sin) katika agano Jipya inamaanisha kukosa maadili ya ki-Mungu (Makosa), maovu na uasi mbele za Mungu.

1 Yoh. 3:4 Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi (rebellion). Kuasi ni kukiuka kwa makusudi taratibu au sheria zilizowekwa na mamlaka Fulani, ni kwenda kinyume na maagano au mapatano. Hili tunaliona kwenye kitabu cha mwanzo pale ambapo Adamu na Eva waliamua, japo kwa kudanganywa na shetani, kula tunda la mti ambao Mungu aliwakataza. (Mwanzo 3)
1 Yoh. 5:17 Kila lisilo la haki ni dhambi, na dhambi iko isiyo ya mauti.
Warumi 14:23 “… Na kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi.”

Mithali 24:9 Fikira za mpumbavu ni dhambi, Na mwenye mzaha huwachukiza watu.
Mithali 21:4 Macho yenye kiburi, na moyo wa kutakabari, Hata ukulima wa waovu, ni dhambi.
Ayubu 23:11 Mguu wangu umeshikamana sana na hatua zake; Njia yake nimeishika, wala sikukengeuka.
Kumb.11:28 na laana ni hapo msiposikiza maagizo ya Bwana, Mungu wenu, mkikengeuka katika njia niwaagizayo leo, kwa kuandama miungu mingine msiyoijua.
Dhambi imetafsiriwa tena kama “Matendo ya mwili”
Wagalatia 5:19 inasema, “Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.
Tena, Dhambi ni Ibada ya sanamu. Wakolosai 3:5 “Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu; kwa ajili ya mambo hayo huja ghadhabu ya Mungu.”

Kuna tofauti kati ya dhambi kwenye Agano la kale na dhambi wakati huu wa Agano la Jipya.
Dhambi katika Agano la kale ilikuwa ni kule kuvunja sheria (Torati ya Musa), na kwenda kinyume na taratibu za dini ya Kiyahudi. Amri kumi za Mungu ndizo zilikuwa kielelezo cha Amri zote. Katika Warumi 4:15 mtume Paulo anatuambia “Kwa sababu sheria ndiyo ifanyayo hasira; maana pasipokuwapo sheria, hapana kosa.” Kwa hiyo kumbe watu walianza kuhesabiwa makosa pale sheria ilipowekwa.

Katika Agano la kale sheria na hukumu zake zilikuwa mikononi mwa waalimu wa Dini na Mafarisayo. Na walikuwa na uwezo wa kumhuku mtu yeyote kulingana na sheria hizo. Kwenye Waebrania 10:28 tunasoma “Mtu aliyeidharau sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu.” Kwa hiyo watu wengi walikufa – utaratibu ulikuwa jino kwa jino, atakayeua kwa upanga atauwawa kwa upanga.

Warumi 8:3 Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili
Wakolosai 2:23 Mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana hekima, katika namna ya ibada mliyojitungia wenyewe, na katika kunyenyekea, na katika kuutawala mwili kwa ukali; lakini hayafai kitu kwa kuzizuia tamaa za mwili.

Paulo akizizungumzia taratibu za ibada ya Kiyahudi katika Wakolosai 2:23 akasema, “Mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana hekima, katika namna ya ibada mliyojitungia wenyewe, na katika kunyenyekea, na katika kuutawala mwili kwa ukali; lakini hayafai kitu kwa kuzizuia tamaa za mwili.
 Katika agano jipya dhambi ina upana zaidi.

Yale yaliyokuwa magumu kwa sababu ya sheria sasa katika Kristo Mungu anayafanya mepesi. Warumi 8:3 inasema “Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili”

Yesu alitangaza mfumo mpya wa maisha ya Kiroho.
Mathayo 5:23-48 “Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako, iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako……….   Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini; lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake……..Imenenwa pia, Mtu akimwacha mkewe, na ampe hati ya talaka; lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila mtimizie Bwana nyapo zako lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa; hata kwa mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu; wala kwa nchi, kwa maana ndiyo pa kuwekea miguu yake; wala kwa Yerusalemu, kwa maana ndio mji wa Mfalme mkuu.

Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi. Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu. Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino; Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili. Na mtu atakaye kukushitaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia. Na mtu atakayekulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye mbili. Akuombaye, mpe; naye atakaye kukopa kwako, usimpe kisogo. Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako; lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi, ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.
 Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo? Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo? Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.

Maeneo yaliyopigiwa mstari yanaonyesha hali ilivyokuwa kipindi cha sheria, lakini tunaona Yesu akitangaza mambo mapya na kusema, “lakini mimi ninasema” Kwa hiyo sasa tunasimama katika yale aliyoyasema Yesu yaani; Kuacha na kukaa mbali kabisa na zinaa, kutokuachana, kutokuapa, kuwapenda maadui na kuwaombea.
Tena katika Mathayo 22:37-39 Yesu akatangaza amri kuu mbili, “Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako.”

Katika sheria ni hapakuwa na kumpenda jirani kama nafsi, wa kukaa naye ni Yule tu ambaye alikuwa amekubalika kutokana na Torati. Kwa sababu hiyo Wayahudi walilazimika kujitenga na wanadamu wengine wote waliokuwa wanaabudu sanamu. Hapakuwa na kuchangamana.
Yesu alipokuja sasa tunaambiwa:
Waefeso 2:14 Kwa maana yeye (Yesu) ndiye amani yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja; akakibomoa kiambaza cha kati kilichotutenga.
2 Wakorintho 5:17 Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.

Wagalatia 2:16 hali tukijua ya kuwa mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria, bali kwa imani ya Kristo Yesu; sisi tulimwamini Kristo Yesu ili tuhesabiwe haki kwa imani ya Kristo, wala si kwa matendo ya sheria; maana kwa matendo ya sheria hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki.
Warumi 8:1 Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.

Warumi 6: 17-23 “Lakini Mungu na ashukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mliitii kwa mioyo yenu ile namna ya elimu ambayo mliwekwa chini yake; na mlipokwisha kuwekwa huru mbali na dhambi, mkawa watumwa wa haki.  ….  Kwa kuwa kama mlivyovitoa viungo vyenu vitumiwe na uchafu na uasi mpate kuasi, vivyo hivyo sasa vitoeni viungo vyenu vitumiwe na haki mpate kutakaswa. Kwa maana mlipokuwa watumwa wa dhambi, mlikuwa huru mbali na haki. Ni faida gani basi mliyopata siku zile kwa mambo hayo mnayoyatahayarikia sasa?
Kwa maana mwisho wa mambo hayo ni mauti. Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa, na mwisho wake ni uzima wa milele. Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.”


Thursday, 8 September 2016

FIKIRI TOFAUTI

KWA NINI NIKO HAPA HAPA? 
(Why Am I  here?)

       Hili ni swali ambalo kila mwenye akili atajiuliza akiona amekaa eneo moja kwa muda mrefu bila kuona mabadiliko chanya yaliyokusudiwa au yaliyotazamiwa. Kuna kipindi wana wa Israeli walifika mahali wakawa wanazunguka milima ya Seiri, tena kwa miaka mingi Mungu aliwatokea na kuwasaidia kwa kuwapa mwelekeo mpya. "Mlivyouzunguka mlima huu vyatosha; geukeni upande wa kaskazini." (Kumbukumbu 2:3)





      Angalia maneno haya aliyoyasema mwanamashahiri mahiri William Shakespeare ‘There is nothing good or bad, but thinking makes it so.’ kwa kiswahili anasema, "Chochote kiwe kibaya au kizuri, ni mawazo au fikra hukifanya hivyo. Hakika vile unavyofikiri ndivyo utakavyojijenga. Kwani maamuzi ya mtu huongozwa na mawazo ya mtu. Mawazo duni husababisha maamuzi duni. Matendo ya mtu ya leo ni matokeo ya mawazo yake ya jana.





     Biblia inazunguimza juu ya vitu ambavyo humtia mtu unajisi. "Kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi. Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati, wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu. Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi." (Marko 7:23), Kwa hiyo kumbe mtu hawezi kuwa mzinzi kama mawazo ya uzinzi hayako ndani yake; tena hawezi kuwa muuaji, mwizi, mkorofi, mlafi nk nk kama hajawahi kuyawaza hayo.





     Hebu nikuulize wewe unawaza nini? Unaweza ukawa unapambana na mambo fulani au tabia fulani ndani ya maisha yako bila mafanikio. Anzia kwenye kubadili jinsi unavyofikiri. Leo nakushauri kama unataka kufanya tofauti, fikiri tofauti. Fikra zako zikiwa zinawaza mambo madhaifu, ugumu, mabaya, maovu na mengine kama hayo bila shaka huweza kuyaepuka mambo haya. Mawazo ya kujidharau yakikutawala hautakaa uheshimike, hashima ya kweli, mafanikio ya kweli huanzia ndani ya mtu. Ili uwaze tofauti kuna mambo ni lazima uyape kisogo, uyaepuke kwa nguvu zote.

Epuka:
1. Kuangalia mambo yaliyopita (your past) na kuvunjika moyo. Huwezi kurudi nyuma kurekebisha makosa ila unweza kujifunza kitu cha kuzalisha (constructive) kutoka kwenye makosa au kufeli huko kulikopita. "Past is past because it has passed, future is future because it is yet to come. Nothing can be changed about past but future is your decision." 
    Kuangalia mambo yaliyopita sio kwamba ni vibaya kwani ni muhimu kuishi maisha ya kujitathmini, tatizo lipo kwenye kuwekeza moyo wako (fikra) zako huko. Waswahili husema, "Yaliyopita si ndwele tugange yajayo" tena wakasema"Maji yakishamwagika hayazoleki" Paulo naye akasema "Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele. (Wafilipi 3:13)

2. Kuwaza mambo manyonge. Mambo makubwa ndiyo yatakayokupa kupanuka kifikra, kiubunifu na hatimaye kiutendaji na Mafanikio. Waza mambo makubwa yanayowezekana, mwamini Mungu na kutenda kwa bidii utafanikiwa.

3. Kuwa na mawazo ya kushindwa. Mawazo ya kushindwa ni sumu ya mafanikio, hata kama umejaribu ukakwama. Jaribu tena na tena hadi uone mafanikio. Mawazo ya kushindwa yatakufanya utangetage hata kukosa kabisa mwelekeo.

4. Kuwaza  maovu na mambo machafu. Mawazo machafu ni kitovu cha maamuzi mabovu. Tunza fikra zako kwa kutazama, kusoma na kusikiliza vitu vya kujenga ufahamu badala ya vitu vya kipuuzi. Soma vitabu, sikiliza wasomi na watu wenye hekima, tazama mambo mazuri achana na marafiki wabaya.

5. Kuchukulia mambo kikawaida. Kumbuka kuna leo na kesho, fanya mambo kwa umakini na maarifa. Ongeza bidii na juhudi zaidi kila siku.
6. Kufanya mambo vilevile kila siku kila wakati. Tafuta kuboresha jambo lako kila siku, litazame ujiridhishe.





Kumbuka Mungu alipomaliza kuumba ulimwengu na vitu vyote, alitazama na akaona kuwa ni vyema. Na wewe jifunze kuyatazama mambo kwa jicho la tathmini.





NENO LANGU KWAKO MPENDWA: 

"FIKIRI TOFAUTI ILI UWE WA TOFAUTI".
Ili ufikiri tofauti:
1.  Yakumbuke makuu ya Mungu ( Yale uliyofanikiwa) na utiwe moyo kwa hayo.
Daudi alipokuta wana wa Israeli na jeshi lote wamenywea kwa jeshi la wafilisti alifikiri tofauti na hatimaye akafanya tofauti. Alitazama mambo makuu ambayo Mungu alimtendea akatiwa nguvu akasimama kumwangusha Goliati. Unapowekeza muda wako mwing kufikiria juu ya mambo uliyoshindwa ndivyo unavyozidi kujidhoofisha.

Wekeza muda wako kuyakumbuka makuu ya Jehova, utasikia kuinuliwa sana. Kazi kubwa ya waliyoshindwa ni kutengeneza hadithi nzuri juu ya kushindwa kwao, bali waliofanikiwa hutengeneza hadithi mbaya kuonyesha sabababu zilizoshindwa kuwafanya washindwe. Majaribu kwao ni mtaji si mateso.

2. Kataa maovu kama Yusufu aliyofanya.
Uovu na dhambi vimezimisha ndoto za wengi. Wengi wameishia mahali duni na pa kukosa tumaini kwa sababu ya kuendekeza maovu. Hakuna raha wala amani kwa watenda mabaya. Mafanikio ya kweli huambatana na wenye haki, wanaowatanguliza wengine. Yusufu alimkimbia mke wa Potifa akaendelea kushikilia maono yake. Majaribu kama hayo ni mengi nyakati hizi lakini ukiamua kukimbia hakika Mungu atakupeleka kwenye ndoto zako. Uovu na nguvu ya kutawala moyo (nia, hisia, na mawazo).

3. Jifunze kutazama fursa mbalimbali na kuchukua hatua.
Usione fursa zote ni za wengine, kaa mkao kutafuta na kuchangamkia fursa. Daudi alipomwona Goliati alitafuta namna ya kuitumia ile fursa kwa kuulizia wengine. Alipochukua hatua ngumu alipanda thamani ndani ya dakika chache. Na wewe usilale, fanya kitu. Pigana na Goliati wetu nasi tutakupa heshima. Hupaswi kulazimisha kuheshmiwa kama wengi wanavyong'ang'ania heshima za vyeo, fanya kitu heshima yako itapanda yenyewe.

4. Ambatana na watu waliofanikiwa zaidi yako kifikra na kimaendeleo.
Watu waliopiga hatua wakati mwingine huwa sababu ya sisi kuvutwa na kufuata nyao zao. Wengi pia hupenda kuwainua wengine. Watu waliofanikiwa wanaweza kukujenga sana kifikra, kwani wengi huwa hawaamini katika kushindwa. Na huwa na mbinu nyingi na shuhuda zenye kujenga sana. Pia, huwa wanakutana na fursa nyingi sana.

5. Fuatilia mambo yenye kujenga (achana na mambo ya kipuuzi)
Tumia muda wako katika mambo ya kujenga, pata taarifa zenye tija. Mawazo ya wengi yamejaa mambo yasiyo na faida kwa sababu ya kusikiliza, kutazama na kusoma upuuzi. Tafuta kanda, vitabu, magazeti na sikiliza vipindi vya maana. Kuangalia ponografi, kusikiliza manyimbo ya kihuni, kushabikia mipira, kubeti, na mengine kama haya ni kupoteza muda wa thamani wa maisha yako.

6. Soma vitabu na kujifunza kila siku.
Kusoma si lazima uende shule, nunua vitabu vya kiroho, vya uchumi, vya kisiasa na vinginevyo ujiendeleze. Mawazo yako yanaweza kunolewa na watu waliofanikiwa kupitia yale waliyoandika. Usiwe mvivu wa kusoma.

8. Mtegemee Mungu na kusoma neno lake kwa bidii.
Mungu ndiye chanzo cha mafanikio yake. na kumcha yeye ni chanzo cha maarifa yote (Mith 7:7). Mtegemee Mungu, usiamgalie mazingira na kukata tamaa, Ishi ahadi za Mungu na uache kufikiri kinyonge. Mungu akiwa upande wetu hatupaswi kuogopa. 

9. Sikiliza mahubiri na kanda za mambo ya kiroho.
Kusikiliza kuna nguvu kubwa sana. unaposikiliza unajipa fursa ya kufikiri na watu waliofanikiwa kupata fikra njema kutoka kwa Mungu. mahubiri yana siri kubwa sana. Pata muda usikilize na Mungu atakupa kufikiri kwa utofauti.

10. Badilisha marafiki ulionao (Achana na marafiki wasiojitambua)
Katika kitabu cha Mithali tunasoma "Chuma hunoa chuma; Ndivyo mtu aunoavyo uso wa rafiki yake." Mithali 27:17 Marafiki wa umbea, mizaha, masengenyo, wavivu, wenye wivu, walevi, wazinzi, wezi, wahuni ni kaburi wazi la ndoto zako. Hakikisha kama wewe ni chuma (Strong) unatafuta marafiki chuma ili mnoane. Marafiki wabaya huharibu tabia ya mtu mwema. Watakupotezea heshima. Huwezi kuaminika ukiwa na marafiki wasioaminika. 

Uwe na marafiki wenye fikra za mafanikio, mawazo ya kujenga, wanaojiamini na wanaoamini katika kufanikiwa, wenye imani katika Mungu. Nawe utafikiri kama wao au zaidi yao na kisha utafanikiwa kama wao au zaidi yao.




Katika haya na mengine utakayojaliwa na Mungu kibinafsi, utaanza kuwaza kwa tofauti na baadaye utaamini kwa tofauti, kisha kufanya kwa tofauti na kufanikiwa kwa tofauti.


Mungu akubariki kwa kuwa sehemu ya blog hii. Karibu kwa masomo mengine.

Mwl. Stephen M. Swai
0713511544

THE TRUTH ABOUT SALVATION

Some people in this world weather due to lack of clear knowledge or any other reason, get confused on the term Salvation. Some say it is not possible for a person to be saved. Some think that to be converted to a certain religion or denomination is the same as Salvation. Now, what is it real?

Wow! I’m sure this is right time for God to talk to you about SALVATION in Jesus Christ. Apostle Paul in 2 Corinthians 6:2 says, “I tell you now is the time of God’s favor, now is the day of salvation.” It might be you have heard about Salvation in one way or the other but today is so special for you to hear this Good news about Jesus Christ. 
Salvation is all about Jesus Christ, that is what made Him to come on earth "TO SAVE THE WORLD" in Matthew 1:21, the Angel of God speaks to Joseph about Mary. The Angel says, "She will have a son, and you will name him Jesus-because He will SAVE his people from their sins" 
Then in John 3:16-18 we read "For God so loved the world, that he gave his only begotten Son, that whosoever believeth in him should not perish, but have everlasting life. For God sent not his Son into the world to condemn the world; but that the world through him might be saved. He that believeth on him is not condemned: but he that believeth not is condemned already, because he hath not believed in the name of the only begotten Son of God."

Here you can the Love of God to us human being, because of our sins Jesus is given as a ransom. In 2Peter 3:9 we read, "
The Lord is not slack concerning his promise, as some men count slackness; but is longsuffering to us-ward, not willing that any should perish, but that all should come to repentance"
Remember we are all sinners!
In Romans 3:23 we read that "We are all sinners and we have fallen short of glory of God" Then under sin:
- We were all died (Ephesian 2:1)
- We were darkness (Ephesian 5:8)
- We were under powers of darkness (Colossians 1:13)

In Ephesian 2:8 we read that:

It is grace of God
It is by faith in Jesus Christ we are all saved
In the book of John 1:12 we read, "But as many as received him, to them gave he power to become the sons of God, even to them that believe on his name"
  • In Jesus, we are new creatures: In 2Corithians 5:17 we read "Any one who is joined to Christ is a new being; the old is gone, the new has come"
  • In Christ we have eternal life: Romans 6:23 we read "For the wages of sin is death; but the gift of God is eternal life through Jesus Christ our Lord"
  • We have moved from dearth to life: John 5:24  says "I am telling you the truth: those who hear my words and believe in him who sent me have eternal life. They will not be judged, but have already passed from death to life"
  • In Jesus we are free from slavery of sin. (John 8:31,34-36)

So, salvation is neither church membership nor religion, but the plan of God to save the lost man from bondage of sin. You may be a faithful member of a certain denomination, religion or church but that doesn't guarantee your salvation. 
Salvation is much about restored relationship between sinful man and Holy God through blood of Jesus shaded at the cross of Calvary.  Jesus came for reconciliation between us and Almighty God 
Now is the time for you to make decision, and accept Jesus as your Lord and Savior. 

Tuesday, 21 July 2015

Masomo/shule na wokovu

 Kikawaida kila mazingira huwa na changamoto za aina yake kwa mtu aliyeokoka, aliyeko kwenye biashara ana za aina yake, aliajiriwa naye vivyo hivyo, iwe ni mjini au kijijini, shuleni au nyumbani. Vilevile mfumo unaoweza kumfanikisha mtu unatofautiana kulingana na mazingira na changamoto; na kila changamoto zina jinsi ya kukabiliana nazo.
Ninaposema masomo namaanisha masomo ya kawaida ya darasani ambayo huwa tunayaita hasa shule. 
Unapokuwa masomoni ni lazima ujue kwamba kusimama katika wokovu kuko palepale, hautaweza kujitetea kwa lolote mbele za Mungu endapo utauacha wokovu. Haijalishi masomo yanaonekana magumu kiasi gani, bado Mungu anatarajia kupata matunda mazuri kutoka kwako katika hatua hiyo ya maisha. 
Katika kipindi hiki tulichonacho cha mapinduzi makubwa ya kisayansi na teknolojia pamoja na kampeni kubwa ya utandawazi (Globalization); vijana wengi walioko masomoni wamepoteza mwelekeo wa maisha yao ya kiroho.

Tuesday, 25 February 2014

UMUHIMU WA KUWA IMARA KATIKA UTUMISHI AU KIROHO

Haleluya!
Uimara ni wa muhimu sana kwa kitu chochote. Kama kitu kitakuwa na sifa nyingine zote kama vile sura nzuri, muundo mzuri, au hali ya kuvutia kabisa ni lazima kuulizia kuhusu uimara wake. Kitu imara ni kitu cha kuaminika.

Uimara ni uwezo wa kudumu kwa muda mrefu, uwezo wa kukabiliana na mazingira, uwezo wa kustahimili mazingira magumu, uwezo wa kuzalisha kilichokusudiwa kwa kiwango, kiasi na hali iliyokusudiwa bila kupoteza ubora. Ubora huonakana zaidi wakati wa misukosuko. Kama kitu au mtu hatosimama imara wakati wa kujaribiwa au wa kupitia changamoto basi uimara umekosekana.

Swali: Je, ni muhimu kwa mtu aliyeokoka kuimarika kiroho

         Paulo akasema, "Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana sikuzote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana."1 Wakorintho 15:58 Mstari huu ni wa msingi sana kwa maisha ya kila mkristo. Paulo anasema tuimarike, tusitikisike, na tuzidi sana kuitenda kazi ya Mungu. Mpendwa misukosuko ya Imani ni Mingi sana katika ulimwengu huu.

        Shetani yupo kila siku kutupiga vita (Waefeso 6:10-12, 1Petro 5:8), tena tunavutwa sana na tamaa zetu wenyewe (Yakobo 1:14). Mungu naye kuna wakati hutujia na kipimo, kuangalia kama tunaweza kuonyesha uthabiti kwa hatua nyingine. (Alifanya hivyo kwa Danieli na wenzake, pia Ayubu). Tusipoimarika hakika hatutaweza kusimama wakati wa kujaribiwa kwetu. Tunapaswa kuwa na Imani thabiti, isiyotikisika wala kubadilika. Yaani tumng'ang'anie Yesu hata kufa.

Kiujumla, Kuimarika huambatana na:

1. Uwezo wa mwamini kustahimili majaribu. 

          Yesu alisema wazi kwamba hapa duniani tutakutana na dhiki (Yohana 16:33) Tena akasema malipo yetu hapa duniani ni mara mia lakini yamechanganyika na udhia (Marko 10:30) Kinachotupa moyo ni kwamba Yeye yupo pamoja nasi. Tena Paulo anatuambia "Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili." 1 Wakorintho 10:13 

Tena Yakobo katika Yakobo 1:12 anasema, "Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao."Kumbe kuna taji tutakayoipata kwa kustahimili majaribu. Ustahimilivu ni tunda la kuimarika katika imani. Wengi ambao hawajaimarika wamekuwa wepesi wa kukata tamaa na kurudi nyuma. Ni muhimu kuamua kujiimarisha katika Imani ili uweze kustahimili hatamaye ukaipokee taji ya uzima.


Kama Yakobo alivyotangulia kusema, "Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi. Saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno.Yakobo 1:2-4 

Sio jambo rahisi kuhesabu ni furaha tupu uwapo kwenye majaribu, unahitajika uimara katika hali ya rohoni ili kubadilishugumu wa mwilini kuwa wepesi. Wapendwa wengi kwa sababu ya mapito wameamua kujiunga na Imani potofu na kusikiliza mafundisho manyonge yanayosisitiza juu ya mafanikio katika ulimwengu huu bila kujali umilele. Tukiimarika katika Imani hakika tutaweza kufurahi katika mateso na dhiki kwa ajili ya ufalme wa Mungu.

2. Ushujaa na ujasiri katika kuitenda kazi ya Mungu na kulitimiza kusudi Mungu alilokuitia.
  
Tunda lingine la kuimarika ni ujasiri na ushujaa katika kazi. Mungu anamwambia Joshua, "Uwe hodari na moyo wa ushujaa, maana ni wewe utakayewarithisha watu hawa nchi hii niliyowaapia baba zao ya kwamba nitawapa." (Yoshua1:6) Kazi ya utumishi katika mwili wa Kristo inahitaji ujasiri mwingi. Vita kwa watumishi ni vikali sana, tena kuna wakati wa kupita katika kupepetwa hata kukataliwa. Tumetumwa kamaa kondoo katikati ya mbwa mwitu (Mathayo 10:16)

Mungu ametuita katika mazingira yenye uadui mkubwa kwa kile tulichotumwa kufanya. Tumepewa kuihubiri Injili ya Yesu Kristo ili watu waokolewe na waondoke kwenye mikono ya Ibilisi. Hii si kazi rahisi, tunahitaji roho ya ujasiri na ushujaa mkubwa. Paulo anasema tuwe hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake (Waefeso 6:10). 

Hatupaswi kuogopa, malango ya kuzimu hayawezi kulishinda kanisa la Mungu. Watumishi wa kweli hawawezi kuogopa wingi wa manabii wa uongo. Tuna ujasiri kama simba, hatuwezi kuogopa dini au dhehebu linalochafua Imani, hatuwezi kuogopa serikali (japo tunaiheshimu) inapoingia kwenye anga za ufalme wa Mungu. Hapa ni ujasiri baada ya kuimarika katika Imani.

3. Furaha na amani katika kuyatimiza mapenzi ya Mungu, si mtu wa kujilaumu.


Tunda lingine la kuimarika ni furaha katika shria ya Mungu. Tumeitwa kufurahi katika Bwana (Wafilipi 4:4) Tena tunapomtumikia Mungu na kuyafanya mapenzi yake tunajisikia furaha na amani hata kama tunayatimiza kwa machozi. Paulo alistahimili vifungo na mapigo mengi akiwa na furaha tele ndani yake Kristo. Hakumlaumu Mungu wakati wa mateso yake; mfano alipokuwa gerezani yeye pamoja na Sila, aliendelea kumsifu Mungu kwa furaha na kuomba. Alifanya yote kwa furaha na amani.

 Yesu alikubali kushinda njaa kwa ajili ya kuyasimamia mapenzi ya Mungu. Aliyachukulia mapenzi ya Mungu kama chakula chake. Yesu akawaambia, Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka, nikaimalize kazi yake. Yesu anakazia swala la kumaliza kazi. (Yohana 4:34)

Upendo wetu kwa Mungu haupaswi kuwa wa maneno matupu, bali ni maisha halisi ya kuishi kulingana na maagizo au amri za Mungu. "Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito."1 Yohana 5:3 Watu ambao hawajaimarika huziona nzito sana sheria za Mungu. Tukiimarika katika Imani hatutaona ugumu kumfuata Mungu. Tutakuwa tayari hata kuyatoa maisha yetu kwa ajili ya kazi ya Mungu. Hatutajilaumu tutakapojikuta  tumeachwa peke, au kusalitiwa. PAulo alikutana na wasaliti wengi lakini aliendelea mbele.

4. Tumaini imara kwa Mungu.

Hakuna tumaini kwa watu wenye imani dhaifu au wasio na imani. Kumtumaini au kumngoja au kumtegemea Mungu kunahitaji Imani. Kumbuka Mungu hatumwoni kwa macho ya damu na nyama. Na kila tunachokijua kuhusu Mungu ni kwa njia ya Imani. Tunaokolewa kwa Imani na tunapaswa kuishi kwa Imani (Waebrania 10:38) Haya ni maneno ya mtu mwenye tumaini "Tazama, Mungu ndiye wokovu wangu; Nitatumaini wala sitaogopa; Maana Bwana YEHOVA ni nguvu zangu na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu".(Isaya 12:2)

Nabii Isaya anasema "Mtumainini Bwana siku zote Maana Bwana YEHOVA ni mwamba wa milele." (Isaya 26:4) Tumaini hili haliji bila Imani thabiti kwa Mungu. Katika Mithali 14:26 tunasoma, "Kumcha Bwana ni tumaini Imara" Nabii Yeremia naye akasema, "Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni tumaini lake. (Yeremia 17:7)

Tumaini Imara ni udhihirisho wa Imani thabiti. Na tumaini letu kwa ajili yenu ni imara, tukijua ya kuwa kama vile mlivyo washiriki wa yale mateso, vivyo hivyo mmekuwa washiriki wa zile faraja. (2 Wakorintho 1:7) Kuaminiana katika utumishi hujenga tumaini imara kati yetu. Na kwa sababu sote tunamtumaini Mungu inakuwa vyepesi kwa Mungu kumtumia kila mmoja wetu kwa ajili ya mwenzake.

Paulo anamwita Mungu wetu, Mungu wa tumaini. Yaani Mungu anayeweza kutumainiwa (ni Mungu wa tumaini letu). Warumi 15:13 "Basi Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mtakatifu." Hapa neno linatuongezea kitu cha ziada juu tumaini tulilonalo katika Mungu. Mungu hutujaza furaha na amani katika kuamini kwetu. Tena katika nguvu za Roho Mtakatifu tunazidi kuimarika katika tumaini letu kwa Mungu. Tumaini hili linahitaji uimara katika Imani.

5. Kumzalia Mungu matunda.

Mti hauwezi kuzaa matunda kabla haujakomaa. Ni lazima kwanza uote mizizi na matawi yake yaimarike vya kutosha ndipo utakapotoa maua na hatimaye kuzaa matunda. Vivyo hivyo na sisi katika maisha yeti ya rohoni pamoja na utumishi, hatuwezi kuzaa matunda tukiwa bado wachanga na tusio na mizizi. Tuanatakiwa tuimarike ili tuweze kuzaa matunda kwa ile mbegu ya Neno la Mungu iliyopandwa ndani yetu. 

Ona Yesu anavyosema, 
"Na zile penye udongo mzuri, ndio wale ambao kwa unyofu na wema wa mioyo yao hulisikia Neno, kisha hulishika; kisha huzaa matunda kwa kuvumilia." (Luka 8:15) Uvumilivu ni tunda la uimara. Mtu ambaye emelegea katika Imani hawezi kuwa na uvumilivu. Kuna misukosuko mingi inayotupata sisi tuliolipokea Neno la Mungu. 

Yesu anataja baadhi katika mfano huu wa mpanzi; yaani Ibilisi (Kando ya njia), Ugumu wa moyo (mwamba), shughuli na udanganyifu wa mali. Mambo haya si mepesi, yanahita uthabiti na uimara ili mtu aweze kuyakabili.

Paulo anashauri juu ya mwenendo ambao pia husababishwa na uimara wetu katika Imani. Anasema, "mwenende kama ulivyo wajibu wenu kwa Bwana, mkimpendeza kabisa; mkizaa matunda kwa kila kazi njema, na kuzidi katika maarifa ya Mungu; (Wakolosai 1:10) Tunawajibika kwa mengi katika ufalme wa Mungu. Tunapaswa kuabudu, kutumika, kuujenga mwili wa Kristo kwa karama na vipawa pamoja na kuwapeleka walioitwa kwa sadaka zetu. Haya yanihitaji uimara katika maisha yetu ndani ya Kristo. Vinginevyo tutaishia kuogopa na kulalamika.

 Paulo anamwambia Tito, "Watu wetu nao wajifunze kudumu katika matendo mema, kwa matumizi yaliyo lazima, ili wasiwe hawana matunda." Tito 3:14 Hili linatufundisha kujizuia, tabia hii ni kiutu uzima. Watoto katika imani hawawezi kufanya hivyo. Watu walioimarika kwenye Imani wana uwezo wa kusimamia matumizi ya kila walichopewa na Mungu ili kuweza kuzaa matunda. 

Katika 1Wakorintho 13:11, Paulo anasema ameyabatilisha "mambo ya kitoto" yaani hafikiri au kufanya tena kama mtoto; ameshakuwa mtu mzima (ameimarika). Mambo kama kuzunguka kwenye vibanda vya maombezi, kukimbia michango kanisani, kuwadharau viongozi, kujivuna kwa sababu ya huduma, kutumia ulaghai kupata fedha na mengine ni mambo ya kitoto. Watu wazima (walioimarika) wanatafuta kazi: yaani wafunge, wajitoe na kujitolea, wakeshe, wahubiri Injili mitaani, waandike vitabu, wapanue huduma (si kugombana na wachungaji) na mengine kama hayo.

FAIDA ZA KUMCHA MUNGU

Kumcha Mungu kunamaanisha kuwa na hofu ya Mungu (fear of The lord), kumuheshimu Mungu kwa kiwango cha juu, kumpa Mungu nafasi anayostahili. Kumcha Mungu kunajumuisha kumuheshimu(kumwabudu), kumtii, kumtukuza na kumtumikia kama Mungu.
2 Mambo ya Nyakati 19:7 Basi sasa hofu ya Bwana na iwe juu yenu; angalieni mkaifanye; kwa maana kwa Bwana, Mungu wetu, hapana uovu, wala kujali nafsi za watu, wala kupokea zawadi.
Mathayo 10:28 Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika jehanum.(Mungu)
Mithali 22:4 Thawabu ya unyenyekevu ambao ni kumcha Bwana Ni utajiri, na heshima, nayo ni uzima.
KUMCHA MUNGU KUNA FAIDA NYINGI

  1. Kunatupa mahusiano mazuri na Mungu.  Isaya 57:15 "Maana yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye milele; ambaye jina lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo patakatifu; tena pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea, ili kuzifufua roho za wanyenyekevu, na kuifufua mioyo yao waliotubu."  Mstari huu unatuweka wazi kwamba, watu wanaoweza kupata nafasi ya kukaa na Mungu ni wale wenye toba na unyenyekevu. 

Saturday, 7 September 2013

SIRI YA MAISHA

Si jambo rahisi kupata tafsiri ya maisha, japo wengi hufikiri kwamba wanajua sana maisha hasa kwa sababu ya kuwa na Umri mkubwa au kuwa na vitu fulani ambavyo wengine hawana. Je, maisha ni nini? Vijana wengi huondoka vijijini na kwenda mijini wakisema wanakwenda "kutafuta maisha..............." Je maisha hutafutwa?
Maswali haya ndiyo natamani yatujengee mwelekeo mmoja wa kuyaendea maandiko ili tuone ni nini Mungu anasema kuhusu maisha.
Kumb. 4:9 "Lakini, jihadhari nafsi yako, ukailinde roho yako kwa bidii, usije ukayasahau mambo yale uliyoyaona kwa macho yako, yakaondoka moyoni mwako siku zote za maisha yako; bali uwajulishe watoto wako na watoto wa watoto wako"
Zab 9:11 Maana, kwa msaada wangu siku zako zitazidishwa; Na miaka ya maisha yako itaongezwa
Luka 12:23 Kwa kuwa maisha ni zaidi ya chakula, na mwili ni zaidi ya mavazi.
Luka 21:34 Basi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafula, kama mtego unasavyo;
 Mdo 15:26 watu waliohatirisha maisha yao kwa ajili ya jina la Bwana wetu Yesu Kristo.
 Mdo 20:24 Lakini siyahesabu maisha yangu kuwa kitu cha thamani kwangu kama kuumaliza mwendo wangu na huduma ile niliyopokea kwa Bwana Yesu, kuishuhudia Habari Njema ya neema ya Mungu.
1 kor 6:4 Basi, mkiwa na mahali panapohukumiwa mambo ya maisha haya, mwawaweka kuwa waamuzi hao waliohesabiwa kuwa si kitu; katika kanisa?
1 kor 15:19 Kama katika maisha haya tu tumemtumaini Kristo, sisi tu maskini kuliko watu wote.
Filip 1:20 "..................ikiwa kwa maisha yangu, au ikiwa kwa mauti yangu."
1 Pet 4:3 Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali;

NANI KAMA YESU?

1. Alikubali kuuacha utukufu mbinguni na kuja kufa kwaajili ya dhambi zetu wanadamu, akatupatanisha na Mungu.

Wafilipi 2:7 "bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.

Isaya 53:3-5 Alidharauliwa na kukataliwa na watu;.....Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu.....Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona.

Warumi 5:6-10...Kwa maana hapo tulipokuwa hatuna nguvu, wakati ulipotimia, Kristo alikufa kwa ajili ya waovu. Kwa kuwa ni shida mtu kufa kwa ajili ya mtu mwenye haki; lakini yawezekana mtu kuthubutu kufa kwa ajili ya mtu aliye mwema.

 Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi. Basi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye. 

Kwa maana ikiwa tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana wake; zaidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika uzima wake. Wala si hivyo tu, ila pia twajifurahisha katika Mungu kwa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa yeye sasa tumeupokea huo upatanisho.

Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi; maana kabla ya sheria dhambi ilikuwamo ulimwenguni, lakini dhambi haihesabiwi isipokuwapo sheria; walakini mauti ilitawala tangu Adamu mpaka Musa, nayo iliwatawala hata wao wasiofanya dhambi ifananayo na kosa la Adamu, aliye mfano wake yeye atakayekuja.  

Lakini karama ile haikuwa kama lile kosa; kwa maana ikiwa kwa kukosa kwake yule mmoja wengi walikufa, zaidi sana neema ya Mungu, na kipawa kilicho katika neema yake mwanadamu mmoja Yesu Kristo kimezidi kwa ajili ya wale wengi. 


Warumi 8:36 Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa.

2. Ana upendo wa kweli kwa wote Hana ubaguzi, Yeye anawaita wote waende kwake wapate uzima-kwake hakuna tajiri wala maskini, wa - Ulaya au wa-Afrika, Myahudi au Myunani..Yeye kwake wote wana nafasi.

Mathayo 11:28 Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

Ufunuo wa Yohana 5:9 Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa"

Yohana 6:37 Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe.

Yohana 3:16-17 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye

3. Jina lake linapita majina yote mbinguni, duniani na kuzimu

Wafilipi 2:9 Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina, ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi(kuzimu); na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.

4. Kwa jina lake mambo makuu hufanyika, tunapokea majibu ya maombi yetu na tunapata uzima au wokovu.

Yohana 16:24 Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu


Marko 16:17 Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya, watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.


Luka 10:17 Ndipo wale sabini waliporudi kwa furaha, wakisema, Bwana, hata pepo wanatutii kwa jina lako.



Matendo ya Mitume 4:10 jueni ninyi nyote na watu wote wa Israeli ya kuwa kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, ambaye ninyi mlimsulibisha, na Mungu akamfufua katika wafu, kwa jina hilo mtu huyu anasimama ali mzima mbele yenu.



Matendo ya Mitume 16:18 Akafanya hayo siku nyingi. Lakini Paulo akasikitika, akageuka akamwambia yule pepo, Nakuamuru kwa jina la Yesu Kristo, mtoke huyu. Akamtoka saa ile ile.

Matendo ya Mitume 4:30 ukinyosha mkono wako kuponya; ishara na maajabu vifanyike kwa jina la Mtumishi wako mtakatifu Yesu.Yohana 20:31 Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake.

Matendo ya Mitume 2:21 Na itakuwa kila atakayeliitia jina la Bwana ataokolewa. (Warumi 10:13)

5. Kuzaliwa kwake hakukuwa kwa kawaida


  • Kulitabiriwa: Atazaliwa na bikira (Isaya 7:14), Atakuwa mtoto mwanaume na atakuwa na uweza wa kifalme (Isaya 9:6)
  • Alizaliwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu (Hakuwa na baba wa kimwili) - Mathayo 1:20 Basi alipokuwa akifikiri hayo, tazama, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema, Yusufu, mwana wa Daudi, usihofu kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.
  • Jina lake lilitolewa na malaika kabla ya kuzaliwa kwake. Mathayo 1:21 Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.
  • Kuzaliwa kwake kulitikisa Uyahudi nzima. Mamajusi wa Mashariki -  Mathayo 2:1 Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, mamajusi wa mashariki walifika Yerusalemu, Wachungaji wa kondeni - Luka 2:8 Na katika nchi ile ile walikuwako wachungaji wakikaa makondeni na kulinda kundi lao kwa zamu usiku. Pamoja na ufalme mzima wa Mfalme Herode - (Luka 2:12-13)
  • Alizaliwa katika mazingira duni sana. Luka 2:7 akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng'ombe, kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.
6. Alifanya mambo ambayo hayakuwahi kufanyika kabla yake tangu kuumbwa kwa ulimwengu.
  • Alifufua wafu waliokufa siku nyingi - Lazaro (Siku nne kaburini) na wengine wengi.
  • Alitangaza msamaha wa dhambi - Marko 2:5 Naye Yesu, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu, umesamehewa dhambi zako.
  • Alikemea pepo zikamtii (Luka 8:29)
  • Alitembea juu ya maji (Marko 6:48)
  • Aliwalisha watu Elfu tano kwa samaki wawili na mikate mitano (Mathayo 14:17...)
  • Aliwaponya wagonjwa wenye magonjwa yaliyoshindikana. Luka 4:40 Na jua lilipokuwa likichwa, wote waliokuwa na wagonjwa wenye maradhi mbali mbali waliwaleta kwake, akaweka mikono yake juu ya kila mmoja akawaponya.
  • Alifundisha kwa mamlaka na kwa utofauti mkubwa. Luka 4:32 wakashangaa mno kwa mafundisho yake, kwa kuwa neno lake lilikuwa na uwezo.
  • Aliukemea upepo ukatii na kuiamuru Bahari ikatulia . Marko 4:39 Akaamka, akaukemea upepo, akaiambia bahari, Nyamaza, utulie. Upepo ukakoma, kukawa shwari kuu.
  • Kwa neno lake samaki walijaa baharini. Luka 5:6 Basi, walipofanya hivyo (Yesu alivyowaagiza) walipata samaki wengi mno, nyavu zao zikaanza kukatika.
7. Alikisema juu mateso, kifo chake na kufufuka kwake, na ikatokea kama alivyosema.
  • Alisema atapata mateso mengi, atasulubiwa na siku ya tatu atafufuka katika wafu. Luka 24:7 akisema, Imempasa Mwana wa Adamu kutiwa mikononi mwa wenye dhambi, na kusulibiwa, na kufufuka siku ya tatu. Mathayo 16:21 Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemu, na kupata mateso mengi kwa wazee na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka.
  • Malaika anashuhudia kufufuka kwake. Mathayo 28:6 Hayupo hapa; kwani amefufuka kama alivyosema. Njoni, mpatazame mahali alipolazwa.
  • 1 Wakorintho 15:4 na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko.
8. Kufa kwake kuliambatana na matukio yasiyo ya kawaida.Luka 23:44 Hapo ilikuwa yapata saa sita, kukawa giza juu ya nchi yote hata saa kenda, jua limepungua nuru yake; pazia la hekalu likapasuka katikati.
  • Dunia ilitiwa giza
  • Kulikuwa na tetemeko kubwa
  • Pazia la hekalu likapasuka
  • Makaburi yakapasuka na wafu waliokuwa ndani yake wakaibuka.
9. Kufufuka kwake kulikuwa dhahiri - alijionyesha kwa watu mbalimbali.  Matendo ya Mitume 1:2-3 hata siku ile alipochukuliwa juu, alipokuwa amekwisha kuwaagiza kwa Roho Mtakatifu wale mitume aliowachagua; wale aliowadhihirishia nafsi yake, kwa dalili nyingi, baada ya kuteswa kwake, ya kwamba yu hai, akiwatokea muda wa siku arobaini, na kuyanena mambo yaliyouhusu ufalme wa Mungu.
1 Wakorintho 15:6 baadaye aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano pamoja; katika hao wengi wanaishi hata sasa, ila baadhi yao wamelala.
10. Alipaa mbinguni na akashuhudiwa  na malaika kwamba atarudi tena (kama alivyoahidi mwenyewe - Yohana 14:1,6)
Matendo ya Mitume 1:9 - 11 Akiisha kusema hayo, walipokuwa wakitazama, akainuliwa, wingu likampokea kutoka machoni pao. Walipokuwa wakikaza macho mbinguni, yeye alipokuwa akienda zake, tazama, watu wawili wakasimama karibu nao, wenye nguo nyeupe, wakasema, Enyi watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni.

Marko 16:19 Basi Bwana Yesu, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu.

Luka 24:51 Ikawa katika kuwabariki, alijitenga nao; akachukuliwa juu mbinguni.
1 Timotheo 3:16 Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu.

Zaidi ya yote Yeye ni Mungu asiyeshindwa, mwaminifu katika ahadi zake; wote waliomwamini wana ushuhuda kuhusu uzuri wake. Ziko shuhuda nyingi za matendo makuu yaliyotendeke ulimwenguni mwote kwa zaidi ya miaka 2000 sasa, na bado mambo yanazidi kutendeka kwa jina la Yesu. Manabii na mitume wengine (Wajumbe wa Mungu) wote waliotajwa katika Biblia wakitatwa majina yao hakuna linaloweza kutendeka. 

Katika Matendo ya Mitume 4:9-12 tunasoma,
Ndipo Petro, akijaa Roho Mtakatifu, akawaambia, .... jueni ninyi nyote na watu wote wa Israeli ya kuwa kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, ambaye ninyi mlimsulibisha, na Mungu akamfufua katika wafu, kwa jina hilo mtu huyu (aliyekuwa kiwete tangu tumboni) anasimama ali mzima mbele yenu. Yeye ndiye jiwe lile lililodharauliwa na ninyi waashi, nalo limewekwa kuwa jiwe kuu la pembeni. Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.

Leo hii katika makanisa ya kweli, na kwenye mikutano na semina ya waabuduo halisi tunashuhudia mambo makuu sana yakiendelea kutendeka; viwete wanatembea, vipofu wanaona, wagonjwa wanapona, watu wengi wanafunguliwa kutoka katika vifungo vya nguvu za giza na watu wengi wanapokea uweza wa kufanyika watoto wa Mungu na kuachana na dhambi.





"JAMANI--- "NI NANI KAMA YESU??????????????????"


A Strong Marriage vs. A Good Family: Understanding God's Order

In many Christian homes, there is a deep desire to build a good family. Parents work hard to provide for their children, maintain a peaceful...

Powered By Blogger